COVID-19
Dondoo Kuhusu Korona
Shinikizo la Juu La Damu (Presha) lina madhara makubwa kiafya. Ni miongoni mwa magonjwa machache yanayosababisha vifo Tanzania. Inakadiriwa kuwa kwa kila watu 10 watu 4 wana shinikzo la juu la damu. Presha haina dalili na sababu hiyo hufanya kuchelewa kugundulika. Presha inadhibitika kama ikifahamika mapema na kuanza matibabu. Hivyo inashauriwa mtu apime mara kwa mara kama ana sababu hatarishi za kupata presha.