Kuwa na Amani: Dhibiti Presha na Madhara Yake Kikamilifu

Kipimo cha presha na kipimo cha uwiano wa uzito na urefu

Presha Inaua Kimya Kimya

𝐉𝐞, 𝐮𝐧𝐚𝐣𝐮𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐬𝐡𝐢𝐧𝐢𝐤𝐢𝐳𝐨 𝐥𝐚 𝐣𝐮𝐮 𝐥𝐚 𝐝𝐚𝐦𝐮 (Presha)? bila kuonesha dalili? Shinikizo la juu la damu (𝐏𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚) unajulikana kama  𝐦𝐮𝐮𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐦𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐦𝐲𝐚. Imeitwa hivi kwasababu haina dalili kama vile magonjwa mengine! Hivyo watu wengi wamekuwa wakipata madhara kama kiharusi na kupata ulemavu wa kudumu na wengine kufa kwa sababu ya presha. Nani yuko katika hatari ya kupata presha?

Niko Kwenye Hatari ya Kupata Presha?

Tafiti zinaonesha ukiwa na umri kuanzia miaka 30 na kuendelea hatari ya kupata presha inaongezeka. Tafiti zinaonesha kuwa w𝐚𝐭𝐮 𝟑𝟎 𝐤𝐚𝐭𝐢 𝐲𝐚 𝟏𝟎𝟎 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐩𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚 𝐋𝐀𝐊𝐈𝐍𝐈 𝐰𝐚𝐭𝐮 𝟐𝟓 huendelea kupata madhara ya presha kwasababu tu 𝐡𝐚𝐰𝐚𝐟𝐚𝐡𝐚𝐦𝐮 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐮𝐠𝐨𝐧𝐣𝐰𝐚 𝐡𝐮𝐮!

Wewe unaweza kuepuka haya kwa njia moja tu! Kupima!

 

Kipimo Kitanisaidiaje Kudhibiti Presha na Madhara Yake?

Wewe unaweza kuepuka haya kwa njia moja tu! Kupima! Ukijua mapema hali yako ya presha itakusaidia kuepuka gharama kubwa za matibabu mbeleni ukilinganisha na mwenzako aliyesubiri mpaka akapata madhara. 

Presha inadhibitika. Nafahamu wengi wanafikiri ni dawa tuu ndo inadhibiti presha. Changamoto ingine ni kwamba wengi hawapendi dawa, hata mimi! Sasa ufanyaje?

Kwanza, fahamu kwamba dawa ni mojawapo ya tiba. Yani, kuna tiba zingine ambazo hudhibiti presha. Kwa kujua mapema hali yako ya presha Utaidhibiti presha kwa njia nyengine kama kuchagua vyakula na kupunguza uwiano wa zito na kimo. Hapa simaanishi kupunguza uzito tuu! Kifaa hichi kitakusaidia kufikia lengo lako la afya. 

Tumepanga Kukusaidiaje?

Tumedhamiria kukusaidia kufikia lengo lako la kuwa na afya bora kwa kufanya mambo yafuatayo.

  1. Tayari tumeshakupa elimu kuhusu umuhimu wa kupima presha
  2. Tunataka kukuona bado una afya na isijokutokea kama inavyowatokea watu wengi 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐨𝐠𝐮𝐧𝐝𝐮𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐩𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚 ukiwa tayari 𝐭𝐚𝐲𝐚𝐫𝐢 𝐰𝐚𝐦𝐞𝐬𝐡𝐚𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐦𝐚𝐝𝐡𝐚𝐫𝐚 𝐲𝐚 𝐮𝐠𝐨𝐧𝐣𝐰𝐚 𝐡𝐮𝐮 𝐡𝐚𝐭𝐚𝐫𝐢: kama vile moyo kuwa mkubwa, kiharusi, na figo kufeli.
  3. Tunakupa uwezo wa kuweza kufahamu hali yako ya afya haraka tena ukiwa nyumbani na uweze kuchukua hatua stahili haraka. Wiki hii tutakupatia BP machine kwa bei ya punguzo na kifaa kimoja cha kukusaidia kudhibiti uwiano wa uzito na urefu. Tutakupatia vifaa hivi kwa shilingi 109,000 wiki hii. Bei ya kawaida ni 140,00/=. 

Fahamau faida ya kuwa na vifaa hivi

Kipimo cha Presha cha digitali

Kifaa: Kipimo cha Presha

Kipimo cha Shinikizo la damu (BP Machine): Takwimu zinaonesha kwa kati ya watu 10, wanne wana shinikizo la juu la damu. Pia, hatari ya kupata Shinikizo la juu la damu huongezeka zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 30 na zaidi.

Faida ya kuwa na kipimo cha presha ni kama ifuatavyo:

  • Epuka madhara yatokanayo na presha kwa kugundua mapema zaidi – Kuna Njia moja tu ya kuweza kutambua kama unashinikizo la juu la damu (presha) kujipima tu!
  • Fahamu maendeleo yako katika kudhibiti presha yako
  • Epuka msongamano hospitali – jipime ukiwa nyumbani
  • Unaweza kujipima presha ukiwa popote sasa. Kinabebeka na chaji inadumu   

Kifaa: Kipimo cha Uwiano wa Uzito na Urefu

  • Fahamu uziito wako kwa uhakika
  • Epuka madhara ya uzito mkubwa kwa kuchukua hatua stahiki mapema
  • Tathmini kama njia unazotumia kupunguza uzito zinafanya kazi kama ulivyotegemea
  • Unaweza kutumia muda wowote na haihitaji nishati yeyote
  • Unaweza kwenda nayo popote
Kipimo cha Uwiano wa Uzito na Urefu

Usisubiri mpaka upate kiharusi au figo kufeli. Pata mashine ya kupima presha LEO! 

Shopping Cart