Pulse Oximeter: Ufanyaji kazi na matumizi

Ili kuishi, mwanadamu huitaji Oxygen. Mwanadamu hupumua kupitia mapafu ambapo Oxygen huingia kwenye damu na Carbon dioxide hutolewa nje. Ukiwa una matatizo katika mfumo wa mapafu –mfano kuwa na magonjwa kama TB, Pneumonia, matatizo ya Moyo nk.- Oxygen hupungua mwilini. Hatahivyo, kuna kifaa ambacho huweza kupima kiwango cha Oxygen mwilini kijulikanacho kama Pulse Oximetry (PO2)

Upumuaji

Bila shaka unafahamu kwamba viumbe hai, ikiwemo binaadamu, huitaji hewa ya Oxygen (O2) ili kuishi. Na pia hutoa hewa Carbon Dioxide (CO2) kama uchafu. Hewa hizi hubebwa katika damu. Binadamu huvuta hewa ya O2 kwa kutumia pua. Hewa hii huingia katika mapafu. O2 hutoka kwenye mapafu na huingia katika damu na kupelekwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo ubongo. Katika damu, Oxygen na CO2 hubebwa na hemoglobini. Unaweza fikiria kwamba O2/CO2 ni abiria,  hemoglobini ni gari na mishipa ya damu ni barabara. CO2 hutoka katika damu na kuingia kwenye mapafu na kupumuliwa nje ya mwili. 

Ugonjwa wowote unaoathiri mfumo wa upumuaji hupunguza kiwango cha O2 na hivyo kuhatarisha uhai wa mtu. Magonjwa kama pumu, moyo, vichomi (pneumonia), TB na hivi sasa Corona, kwa uchache huathiri mfumo wa upumuaji.

Namna P02 inavyofanya kazi

P02 hutumia miale ya mwanga kupima kiwango cha oxygen kilichobebwa na hemoglobin. Mianga iko ya aina mbili, ile ya kupima kiwango cha oxygen kwenye hemoglobin na mingine hupima kiwango cha CO2 kwenye hemoglobini

Je, nahitaji P02 nyumbani?

Pulse oximeters ni (1) Kifaa kinachotumika nje ya mwili (non invasive); (2) Bei nafuu (cheap to buy and use); (3) Kinagundua kwa haraka upungufu wa hewa ya oxygen (hypoxaemia) 

 

Kama wewe ni mgonjwa wa Moyo, ulishapata shinikizo la moyo; pumu; TB ama tatizo linaloathiri upumuaji ni MUHIMU kwako kuwa na P02 nyumbani.

OFFER OFFER OFFER!

Kwasasa tumetoa punguzo. Utapata pulse Oximeter moja kwa 55,000/=

Offer hii inaisha tarehe 30 November 2020

bonyeza link hii kuweka oda sasa!:  https://afyatechtz.com/product/pulse-oximeter-033/

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Pulse Oximeter: Ufanyaji kazi na matumizi?
Mimi ni Dr. Adinan