Tunakuhakikishia Huduma Bora

Tunaimani kwamba utafurahia huduma yetu na bidhaa zetu zitachangia kuboresha afya yako. Kama kawaida tutakuelekeza na kukupa elimu na ushauri bila kuchoka, endapo utapkapokuwa na swali lolote, tafdhali tuulize tutakuwa tayari kukusikiliza.

Kama mteja wetu unaagiza tukutumie bidhaa sehemu ambayo hatuna ofisi zetu, tutaendelea kuhakikisha tunakutondolea hofu na kukupa uwezo wa kuweza kujaribu kifaa chako kama kinafanya kazi kama iilivyokusudiwa. 

Health Equipment Solutions inakupa fursa ya kulipa baada ya kupata kifaa. Utachagua kama utataka kulipa kabla au baada ya kupokea kifaa wakati unaweka order kwenye website yetu. Lengo letu ni kutunza uaminifu huku tukiamini nawe mteja wetu ni mwaminifu- Kwamba utalipa ndani ya lisaa limoja (1) baada ya kupokea kifaa ulichokiagiza 

Kwa Wateja wanolipa baada ya kupokea

Kwa kutaka kulipa baada ya kupokea kifaa, mteja  anakubaliana na Kampuni ya AFYATech kufanya yafuatayo:

  1. Mteja ataweka oda kwa kutumia webisite yetu, au kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii
  2. Mteja atatakiwa pia kutuma ujumbe wa kuweka oda kwa namba yake iliyosajiliwa na NIDA.
  3. Namba itakayotumika kutuma SMS inatakiwa ifanane na namba iliyojazwa kwenye website wakati wakuweka oda
  4. Mteja atatuma vitambulisho vyake viwili vyenye majina sawa ikiwemo yale majina yanayosomeka kwenye kitambulisho cha NIDA.
  5. Mteja atalipia gharama za usafiri  
  6. Mteja atalipa ndani ya lisaa limoja baada ya kupokea kifaa chake

Kushindwa kutimiza mahitaji haya (1-4) kutawezesha AFYATech kutokutuma kifaa, kuchelewa kutuma kifaa.

Na kama kifaa kitakuwa kimekwishatumwa, ila mteja akakiuka kubaliano la 5, AFYATech itafuata hatua za kisheria kudai stahiki zake. 

Warranty

Vifaa vyetu vyote vina warranty ya kuanzia mwaka mmoja mpaka mitatu.

Kwa wanafunzi wa kozi za afya, warrranty ni mpaka wamalize shule.

Ili ustahiki kurejeshewa, ni lazima bidhaa yako isitumike na katika hali sawa na uliyoipokea. Ni lazima pia kuwa katika ufungaji wa awali.

Ili kukamilisha urejeshaji wako, tunahitaji risiti au uthibitisho wa ununuzi kwenye website.

Kurudisha bidhaa na kurejeshewa pesa

Sera yetu ya kurejesha pesa na kurejesha hudumu kwa siku 30. Ikiwa siku 30 zimepita tangu ununuzi wako, hatuwezi kukurejeshea pesa kamili au kubadilishana.

Ili ustahiki kurejeshewa, ni lazima bidhaa yako isitumike na katika hali sawa na uliyoipokea. Ni lazima pia kuwa katika ufungaji wa awali.

Ili kukamilisha urejeshaji wako, tunahitaji risiti au uthibitisho wa ununuzi kwenye website.

Kubadilisha bidhaa

Tunabadilisha bidhaa ikiwa na kasoro au kuharibika tu.

Iwapo unahitaji kuibadilisha na kupata bidhaa sawa, tutumie barua pepe kwa {sale@afyatechtz.com} au tuandikie kwa WhatsApp +255 783 552 959

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Terms and Conditions?
Mimi ni Dr. Adinan