Epuka Madhara Ya Kisukari
Vifaa 3 vitakusaidia kudhibiti na kuepuka madhara ya kisukari. Ukiwanavyo unaweza kufahamu kama uko kwenye hatari ya kupata vidonda na madhara mengine.
Kwanini ufahamu kuhusu vipimo vya kufanywa wakati hii ni kazi ya daktari? Hili ni swali zuri lakini jiulize hivi, ukiumwa wewe ni nani anadhurika? Bila shaka si daktari. Unafahamu jibu.
Madhara yote ya kisukari yanazuilika kama ukifahamu vitu viwili: madhara yanavyotokea na hali yako ya sasa ya afya. Huwezi jua hali yako ya sasa kama hujapima.
Madhara ya ugonjwa wa kisukari si tu yanakatisha uhai na kusababisha ulemavu kwa watu wengi bali pia husababisha msongo wa mawazo kwa wanaougua ugonjwa huu-hawana raha.
Madhara ya kisukari ni matokeo ya uharibifu unaofanywa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye mishipa ya damu midogo na mikubwa, mishipa ya fahamu na katika kudhoofisha kinga ya mwili.
Madhara yote haya unaweza kuyadhibiti kama utachukua tahadhari katika muda muafaka.
Kabla ya kufahamu ufanye nini na upi ni wakati muafaka inabidi ufahamu kisukari husababishaje madhara haya.
Sukari inatakiwa ihifadhiwe kwenye tishu, isikae ndani ya damu. Inapokaa kwenye damu kwa kiwango kikubwa husababisha sumu inayofanya uharibifu kwa namna tatu.
1. Kwanza huaribu mishipa ya fahamu na hivyo hutoweza kuhisi. Kwa kuharibu mishipa ya fahamu husababisha sehemu zinazotegemea mishipa hii kutokufanya kazi kwa ufasaha.
Kwa mfano, upungufu / kosefu wa hisia miguuni husababisha mwenye kisukari kutokufahamu kama mguu umekandamizwa kama kubanwa na kiatu na hivyo kusababisha vidonda.
Vile vile kupungua ufanisi wa kazi za mishipa ya fahamu kwenye mishipa ya damu husababisha wangonjwa wa kisukari kupata matatizo ya presha kushuka na upungufu wa nguvu za kiume.
2. Kisukari pia huaribu mishipa ya damu na -kama tulivyoona- kusababisha hali inayoitwa artherosclerosis. Hatimaye mishipa ya damu huziba haswa ile ya pembeni ya mwili kama vile miguu.
Kukosekana kwa damu maana yake sehemu husika hukosa chakula, hewa safi na kinga. Hivyo sehemu hiyo hufa na kama utapata maambukizi hutapona kwa urahisi. Mara nyingi hii imekuwa sababu kubwa ya wagonjwa wa kisukari kukatwa miguu.
Mishipa mingine ya viungo muhimu vya mwili huathiriwa na kusababisha mdahara yafuatayo:
3. Njia ya tatu, sukari huathiri kinga ya mwili kwa kuharibu na kupunguza muda wa kuishi wa seli zinazopambana na magonjwa. Hali hii husababisha mgonjwa wa kisukari kuwa katika hatari ya kupata magonjwa hasa ya kuambukiza kwa urahisi na kushindwa kutibika kwa wakati.
Ni muhimu kukumbuka pia, kwakuwa unaugua sukari na unapambana kuishusha, unaweza kupata madhara mengine yatokanayo na tiba-kupungua kwa sukari mwilini.
Pia wagonjwa wa kisukari wanaomeza dawa wanaweza wakapungukiwa na sukari mwilini ikiwa ni moja ya madhara ya dawa.
Sukari ya kushuka (hypoglycemia) ni shida inayowakumba wagonjwa wengi wa kisukari wanaotumia dawa aina ya sulfonylurea au insulini.
Hivyo ni muhimu kwa kila mgonjwa wa kisukari kufanya vipimo hivi ili uweze kuchukua hatua za haraka kujikinga.
Nimevigawa vipimo hivi katika makundi mawili kulingana na wapi kipimo kitafanyika, hospitali au nyumbani.
Vipimo vya nyumbani ni vile ambavyo unashauriwa kuwa navyo ili kuweza kukusaidia kutathmini tiba na hali yako ya kiafya na hivyo kuepuka madhara ya kisukari kabla hayajakomaa na kuwa hatarishi.
Vipimo vya hospitali, kwasasa huduma hii hutolewa hospitali na tafsiri ya vipimo hivi hutolewa na muhudumu wa afya.
Kama tulivyoona hapo juu, ubaya wa ugonjwa wa kisukari ni kwamba sukari inaweza kuwa juu na kuendelea kuleta madhara bila kuonesha dalili!
Kama hutokuwa unapima, yani hutokua unafahamu kiwango chako cha presha au sukari, unajiweka kwenye hatari ya kupata kiharusi, figo kufeli, kupata vidonda nk.
Hivi vyote huaribu furaha ya maisha, vitakugharimu pesa nyingi za matibabu na utashindwa kufanya shughuli zako za kungeza kipato chako kwakuwa muda mwingi utakuwa unautumia hospitali.
HbA1C (Kipimo cha Miezi 3): Ukipima sasa hivi sukari ukakuta iko sawa, hongera. Lakiini, inawezekana kwamba imeshuka kwasababu mbalimbali ikiwamo njaa au kama ulifanya mazoezi muda mfupi.
Ndiyo maana kuna kipimo cha kupima udhibiti wa kisukari kwa muda wa miezi 3. Daktari wako atakuelekeza kutoa damu kwa ajili ya kupima kipimo cha HbA1C kuweza kutathmini maendeleo yako.
Pima hali ya Figo: Kisukari huathiri figo na kuleta athari kubwa zingine kama presha. Kwasababu hiyo ni muhimu sana kufahamu hali ya figo.
Pima macho: Kama tulivyoona macho pia ni sehemu ya viungo vinavyoathiriwa na kisukari. Hivyo ni muhimu kufahamu hali ya afya ya macho yako pindi unapogundulika una presha na wakati
Kiwango cha mafuta kwenye damu: Baadhi ya mafuta yamenasibishwa na kusababisha kisukari. Kwasababu kuna dawa za kupunguza mafuta hayo, ni muhimu kufahamu kupima ili kupata dawa itakayokufaa.
Pima kiwango cha sukari kwenye damu: Ili kuweza kufahamu hali yako ya kisukari na kuweza kuidhibiti pamoja na kudhibiti madhara yake inabidi uwe na mashine yako kuweza kupima sukari kila wakati unapotaka kufanya hivyo
Kupima Presha: Kiwango chako cha presha ya damu ndiyo kiashiria kikubwa kwamba umeidhibiti ama la! Ni kwa kupima tu ndipo mtu atagundua kama presha iko juu. Tafiti zinaonesha wanaojipima mara kwa mara hudhibiti vizuri presha zao.
Kupima hisia miguuni haswa sehemu zile zilizokwenye hatari ya kupata vidonda. Ni muhimukufanya kipimo hiki ili kuhakiki utimamu wa mishipa yako ya faahmu. Hii itakuwezesha kuepuka vidonda ambavyo vinaweza kukusababisha ukatwe mguu.
Kifaa hichi chenye kinyuzi ni mahususi kwa kupima hisia na hivyo kuweza kuelewa hatari uliyonayo- uwezekano wa kuumia bila kuhisi maumivu.
Uwiano wa Uzito na Urefu: Uwiano wa uzito na Urefu unaathiri hali yako ya kisukari kwa kuwa uwiano mkubwa huongeza hatari ya kutokudhibiti kisukari. Hivyo ni muhimu uwe na kipimo cha uzito na urefu ili uweza kufuatilia kwa ukaribu.
Ingawa ni LAZIMA kupima ili kuweza kudhibiti kisukari na kuepuka madhara yake, si lazima kuwa na vifaa hivi nyumbani.
Hatahivyo kuna faida nyingi za muhimu za kuwa na vifaa hivi nyumbani. Mimi na kushauri kuwa na vifaa hivi nyumbani. Fahamu sababu.
Sababu moja ya msingi inayozaa faida nyinginezo ni kwamba kuwa na vifaa hivi nyumbani hukuwezesaha kufahamu hali yako ya sukari kwa uhakika wakati wowote ule.
Kama tulivyoona hapo juu, ubaya wa ugonjwa wa kisukari ni kwamba sukari inaweza kuwa juu na kuendelea kuleta madhara bila kuonesha dalili!
Kufahamu hali yako ya sukari kwa uhakika wakati wowote ule huja na faida zifuatazo.
Rudisha amani yako: Kwa uzoefu wangu, mtu anapogundulika na kisukari hupata huzuni ghafla na kuanza kufikiria athari ambazo amekwisha kuziona zikiwatokea watu anao wafahamu. Mtu huanza kufikiri vipi nikipat vidonda miguuni, vipi nikipata shamulio la moyo au kiharusi kama fulani. Je, na mini sintoweza kufurahia tendo la ndoa? Madhara yote haya sasa unaweza kuyaepuka kwasababu sasa unaweza kuchukua hatua stahiki mapema kulingana na kiwango chako cha sukari kwa kuwa unafahamu.
La sivyo raha usingeipata kama ungepata madhara haya ya kisukari.
Faida nyenginezo ni kwamba sasa utatumia muda wako kupumzika na kukaa na familia yako badala ya kutumia muda huo kwenda hospitali na kukaa kwenye foleni. Au kwenda mbali kwingine kwasababu tuu unataka kupima presha au kisukari.
Faida ingine muhimu ni kuokoa gharama za matibabu ya madhara ya kisukari. Madhara yote, mfano kiharusi, figo kufeli, kupata vidonda na kupungua nguvu za kiume, huaribu furaha ya maisha.
Magonjwa haya yanagharimu pesa nyingi za matibabu na unashindwa kufanya shughuli zako za kungeza kipato chako kwani muda mwingi unakuwa kwenye matibabu.
Vifaa 3 vitakusaidia kudhibiti na kuepuka madhara ya kisukari. Ukiwanavyo unaweza kufahamu kama uko kwenye hatari ya kupata vidonda na madhara mengine.
SAIDIA WENGINE
Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu. Usisahau kutupa maoni au kutuuliza swali lolote
HES-P-D-BDW-1_19016
HES-P-D-SET-D8_31212
HES-WB-01_12127
HES-P-D-DM-2_22878
DM-BP-01_12034
HES-P-D-BPA-12_18778
HES-CC-D-Nebul-1_11922
HES-CC-D-PO2-1_7479
HES-P-D-SET-6_4194