Pata Elimu Sahihi Kuhusu Presha na Kisukari

Muulize Dr. Adinan

Maswali Kuhusu Presha

Hellow karibu sana. Asante sana kwa swali zuri. Kutokuona / kutokuhisi dalili ndiyo hatari ya presha. Presha inaweza kuwa juu kiasi cha kuanza kuathiri viungo muhimu kama moyo na ubongo bila kuonesha dalili. Ndiyo maana ikaitwa Muuaji wa Kimya kimya.

Hivyo, namna moja tu ya kufahamu presha yako ni kupima. Unahitaji kupima presha yako ili kuwa na uhakika wa kiwango. Kufahamu kiwango kunakusaidia kuweza kuidhibiti na kuepuka madhara ya presha

Hapana! Huwezi kuacha dawa hata kama unaona presha yako imekaa sawa! Ukifikiria kuacha dawa inabidi kwanza uwasiliane na daktari anayekuhudumia. Kwanini?

Presha ni ugonjwa wa muda mrefu! Na kwasasa hauna tiba iliyokwishafahamika kwa uhakika kama ina uwezo wa kutibu punde utakapotumia dawa. Kwasasa dawa zilizopo hupunguza presha. Kwahiyo, presha yako imeidhibiti kwasababu umetumia dawa.  

Presha aina ya pili ndiyo inaweza kutibika. Fahamu Aina za presha kwa kubonyeza HAPA

Swali zuri sana. Kimsingi ni wakati tuu umegundulika una presha inabidi ufanye vipimo hivi. Kwanini? Jibu ni rahisi ila ni hatari. Presha haina dalili. Inaweza kuwa juu kwa muda mrefu na kuleta madhara. Kisha mtu hupata madhara ghafla. Mfano kiharusi, mshtuko wa moyo nk. Hivyo kwakuwa mtu hakuwa anajua muda gani amekuwa na presha ni vizuri kupima ili aweze kutibu, kudhibiti na kuepuka madhara kwa uhakika

Kuna Njia moja tu ya kuweza kutambua kama unashinikizo la juu la damu: kujipima tu! Mtembelee mhudumu wa afya ambaye ataweza kukupima. 

Presha haina dalili na sababu hiyo hufanya kuchelewa kugundulika. Na kwasababu huuwa watu wengi bila wenyewe kufahamu kama wana presha, huitwa silent killer, muuaji wa kimyakimya.

Hivyo inashauriwa mtu apime mara kwa mara kama ana sababu hatarishi za kupata presha.

Moja ya visababishi vya presha ni umri kuongezeka: Ukiwa na Umri wa miaka 30 au zaidi uko kwenye hatari na inakubidi uanze kupima presha yako mara kwa mara. Kwa kuanzia unaweza kupima angalau mara moja kwa mwezi. 

Nikweli kabisa unavyosema. Watu wengi wamekuwa wakihofia kujua presha zao. Lakini tafiti zinaonesha kwamba wanaojua hali zao wana uwezo mkubwa wa kudhibiti prehsa na madhara yake kuliko yule ambaye hajui.

Kuepuka na Kudhibiti Presha inawezekana. Ila ili ufanikiwe inabidi kufahamu jambo moja muhimu. Hakuna njia moja tuu ya kudhibiti presha, inabidi kufanya jitihada mbalimbali mchanganyiko.

Bahati nzuri ni kwamba ukitumia njia hizi utaweza pia kudhibiti magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari na saratani.

Sasa umefahamu utangulizi huu, unaweza kuendelea kufanya yafuatayo ili kudhibiti au kuepuka presha.

Soma zaidi. Bonyeza hapa

Shinikizo la juu la damu la juu (presha) ni kuwa na presah iliozidi 139/89mmHg.

Zaidi ya 95% ya wagonjwa wa presha hatujui nini kimesababisha. Asilimia tano waliobaki huwa kuna magonjwa husababisha presha kuwa juu mfano goita, ugonjwa wa figo au kuwa na mimba. 

Hatahivyo, kuna vitu humuweka mtu kwenye hatari ya kuwa na presha. Vihatarishi hivyo ni

  1. Umri mkubwa (kuanzia umri wa miaka 30 au zaidi),
  2. kurithi katika familia,
  3. vyakula,
  4. kutokufanya mazoei,
  5. utumiaji wa tumbaku, na
  6. unyaji pobme uliokithiri.

Tofauti na magonjwa mengi, shinikizo la juu la damu halina dalili. Presha inaweza kuwa kubwa kuweza kupasua mishipa ya kwenye ubongo au kuharibu moyo na figo bila kuwa na dalili hata moja!

Presha imeitwa muuaji wa kimyakimya kwasababu hii. ya kutokuwa na dalili huku ikisababisha vifo kwa watu wengi na kuwaahca wengi na ulemavu wa kudumu 

Ni muhimu kujipima presha ukiwa nyumbani ili uweze kufahamu hali yako halisi ya presha. Nafahamu unajiuliza, kwani vipimo vya hospitali havitoshi? Kuna utofauti gani wa presha yangu nikiwa nyumbani na ile ya hospitali? Tafadhali soma kufahamu sababu.

Tafiti zinaonesha kwamba sasa watu wengi wameanza kuwa na presha iliyojificha (masked hypertension). Yani wanakuwa na presha ya kawaida wanapopimwa hospitali lakini wakiwa nje ya hospitali presha yao hupanda. Na haswa wakati wa usiku.

Tofauti na magonjwa mengi, shinikizo la juu la damu halina dalili. Presha inaweza kuwa kubwa kuweza kupasua mishipa ya kwenye ubongo au kuharibu moyo na figo bila kuwa na dalili hata moja!

Presha imeitwa muuaji wa kimyakimya kwasababu hii. ya kutokuwa na dalili huku ikisababisha vifo kwa watu wengi na kuwaahca wengi na ulemavu wa kudumu.

Mambo manne (4) tunayojifunza hapa ni kwamba:

  1. Presha hubadilika
  2. Kipimo kimoja hakitoshi
  3. Mabadiliko ya presha hata ikipanda inaweza isiwe na dalili hata moja!
  4. Namna ya pekee kufahamu presha yako ni kupima tu!

Hivyo ni muhimu kuwa na kipimo cha presha nyumbani ili uweze kujipima katika mida mbalimbali kufahamu hali yako halisi ya presha.

Presha ya damu hubadilika mara kwa mara. Haiwi ile ile wakati wote. Maana yake ni kwamba unaweza kupima hospitali ukakuta presha ndogo, kumbe muda mwingi presha yako huwa kubwa. Hii tunaita presha iliyojificha, kimombo, masked hypertension.

Lakini kinyume chake ni ukweli, unaweza kupima hospitalini ukakuta presha yako ni kubwa lakini kumbe si kweli, ni kwasababu ya hofu ya mazingira ya hospitali. Hii tunaiita presha iliyotokana na hofu, kimombo, whitecoat hypertension

Changamoto ingine ambayo imechangia pakubwa katika vifo na ulemavu kwa watu wengi ni kwamba hata presha inaweza kuwa juu sana sana bila dalili yeyote. Ndiyo maana wengi hupata kiharusi (stroke) au figo kufeli.

Huonekana ni ghafla ila ukweli ni kwamba wengi waliugua presha bila kuonesha dalili. Nafahamu unajiuliza sasa ufanye nini ili kufahamu presha yako na kujikinga? Ujipime marangapi ili upate wastani wa presha yako kwa siku?

Kujipima mara nyingi kwa siku nzima ndiyo namna sahihi ya kuweza kufahamu kwa uhakika wastani wa presha yako. Ndiyo, Najua ulianza kufikiri hivi.

Suluhisho: Hatahivyo, kuna kifaa ambacho kinaitwa Ambulatory Blood Pressure Measurement (ABPM) hichi kitakupima kwa masaa 24. Kulingana na uhitaji utajipima kwa uwiano wa muda uutakao: kila baada ya lisaa au nusu saa au masaa mawili. 

Tunajifunza nini?: Licha ya sasa tunakitumia kifaa hiki kwa utafiti zaidi, kama mtaalamu, naona hii ndiyo njia tutakayokuja kuitumia siku za usoni ili kuweza kufahamu kwa uhakika kama presha yako ni ya kawaida, iko juu (presha), au iko chini. Hivyo kutuwezesha kuchukua hatua stahiki kwa wakati.

Maswali Kuhusu Kisukari

Ndiyo. Homa inapandisha sukari.

Ugonjwa wowote huleta stress kwenye mwili. Haswa magonjwa ya kuambukiza ambayo mara nyingi huleta Homa, husababisha sukari kupanda.

Ndiyo maana ni muhimu saana kucheki Homa unapojihisi Hali sinshwari.

Kama umekula ndani ya masaa mawili: Iwe angalau 7-10
Kama hujala, kama vile ndo umeamka iwe 3.5 – 7

Sukari ikishuka unahitaji kuiongeza ili usipate madhara ya kupungua kwa sukari.

Kufahamu huduma ya kwanza kwa upungufu wa sukari bonyeza HAPA

Swali lipi Unalo Kuhusu Presha? Tuulize Sasa 

Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Presha na Kisukari: Uliza Ujibiwe?
Mimi ni Dr. Adinan