fbpx

Shinikizo La Damu La Juu – Presha

Facebook
Twitter
WhatsApp

Imeandikwa na Dr. Adinan J. MD. MSc. FDHS. F.Forgatty, mtafiti wa magonjwa na  mkufunzi wa vyuo vya Afya kwa zaidi ya miaka 10. 

Shinikizo la damu ni nini?

Shinikizo la damu si baya, shinikizo la damu la juu ndiyo baya na hatari kwa afya yako.

Je, ulikuwa unafahamu unaweza kuwa na presha (shinikizo la juu la damu) bila kuonesha dalili yeyote?

Kwanza tufahamu maaana ya shinikzo la damu kabla hatujazungumzia shinikizo la juu au kama inavyofahamika zaidi Presha!

Maji huitaji msukumo ili kuweza kupita kwenye mpira. Msukumo huu ndiyo huitwa shinikizo au presha…

kama maji yanavyohitaji presha kupita kwenye bomba au mpira ndiyo hivyo hivyo  damu huihitaji pressure kupita kwenye mishipa ya damu.

Kwa kutumia mfano wa maji, kama pressure itapungua sana, maji hayatafika sehemu muhimu yanapotakiwa kwenda. 

Vivo hivyo kama presha ikiwa kubwa sana, mabomba ya maji yatapasuka, na hivyo tnea maji hayatofika sehemu husika.

Vivyo hivyo damu. Presha ikiwa kubwa sana, huaribu mishipa ya damu na kusababisha damu kumwagika sehemu isiyotakiwa na kuleta madhara, na pia kutokufika sehemu inayotakiwa.

Viungo vikubwa na muhimu huathiriwa na shinikizo la juu la damu. Mifano ya viungo hivyo na madhara ni

  • Ubongo (kupata kiharusi),
  • Moyo (kupta shambulio la Moyo au Moyo kushindwa kufanya kazi),
  • Macho kutokuona,
  • Figo kufeli,

 

Presha ya Kawaida ya damu ni 120mmHg wakati moyo unasukuma damu na 80mmHg wakati moyo unapokea damu. Kama ambavyo huandikwa 120/80mmHg. 

 

Kuna ina ngapi za shinikizo la juu la damu?

Kuna aina mbili za shinikizo la juu la damu kulingana na kinachosababisha.

1. Shinikizo la juu la damu ambalo sababu ya presha kupanda inafahamika – hii hutokea kwa wagonjwa kati ya 5%-10% ya wagonjwa wa presha. Maranyingi hutokea kwa watu wenye umri chini ya miaka 40.

2. Shinikizo la juu la damu ambalo sababu ya presha kupanda haifahamiki. Aina hii ya shinikizo la damu ndiyo huongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa, 90%.

3. Presha ya hofu – aina hii ya presha hutokea kwa mtu ambaye kiuhalisia hana shinikizo la juu la damu bali presha yake huwa juu kutokana na hofu pale ambapo atapimwa presha yake hospitali. 

Kupanda kwa presha anapokuwa hospitali hunasibishwa na hofu kwakuwa hajazoea mazingira ya hospitali.

Pia unaweza kugawa aina za shinikizo la juu la damu kulingana na athari zinazojiitokeza wakati presha inapokuwa juu sana au namna presha inavyobadilika kwa matibabu.

4. Shinikizo la damu la juu kali – presha huwa zadi ya 180 / 120 mmHg na uharibifu wa viungo mbalimbali. Hali hii ni dharura ya kitabibu na inatakiwa kutibiwa hospitali. 

Aghalabu hali hii hujitokeza. Inakadiriwa ni kati ya mtu 1 kati ya wagonjwa 50.000 huwa na shinikizo la damu la juu sugu.

5. Shinikizo la damu la juu sugu – presha huwa ngumu kushuka hata unapotumia aina tofauti tatu za dawa kwa wakati mmoja. Inakadiriwa angalau 10% ya wagonjwa huwa na shinikizo la damu la juu sugu.

6. Shinikizo la damu peke. Si wakati wote utakuta presha ya juu (wakati moyo unadunda) na ya chini (wakati moyo umetulia) zimepanda. Wakati mwingine unakuta presha ya juu ndiyo imepanda na ya chini iko kawaida au ya chini imepanda na ya juu iko kawaida.

Shinikizo la juu la damu husababishwa na nini?

Kama tulivyoona, ni 5%-10%  tu ya gonjwa wa presha ambao madaktari wanaweza kubaini kilichosababisha shinikizo la damu kuwa juu. 

Lakini pia kuna vitu ambavyo hukuweka wewe katika hatari ya kuwa na presha kuliko yule ambaye hana vitu hivyo. Vitu hivi huitwa vihatarishi. 

Naomba nikufahamishe kwamba kisababishi na kihatarishi si sawa. Tukikiita kitu kisababishi cha ugonjwa X maana yake ni kwamba yeyote aliyeko na hicho kitu atapata ugonjwa X.

Ukiwa na kihatarishi cha ugonjwa X maana yake ni kwamba uko katika hatari ya kupata ugonjwa X, hatahivyo si lazima uupate. 

Nitoe mfano kwenye ugonjwa wa kipindupindu. Bacteria aina ya vibrio cholerae husababisha kipindupindu na  kutokuzingatia usafi ni kihatarishi. 

Wakati kila mgonjwa wa kipindupindu utamkuta na Vibrio cholerae, lakini si kila asiyezingatia usafi atapata kipindupindu. 

Sasa nishakufahamisha tofauti ya kisababishi na kihatarishi, turudi kwenye vihatarishi vya ugonjwa wa presha. 

Vihatarishi vya kupata presha vimegawanyika katika makundi mawili:

  • Vile ambazo huwezi kuvidhibiti (ziko nje ya uwezo wako) na
  • vile ambazo unaweza kuvidhibiti.

Vihatarishi vya presha ambavyo unaweza kuvidhibiti ni mfumo wa maisha kama vile

  • Mlo, kula chumvi nyingi, vyakula vyenye mafuta mengi ya wanyama, na kutokula matunda na mboga mboga;
  • Kutokufanya mazoezi au kutokufanya shughuli zinazotumia nguvu; utumiaji wa tumbaku kama kuvuta sigara;
  • Unywaji pombe kupita kiasi; na
  • Uwiano mkubwa wa uzito na kimo kama vile unene na unene wa kupitiliza.

Vihatarishi vya presha ambavyo huwezi kuvidhibiti ni

  • Umri, shinikizo linaanza kupanda kuanzia miaka 30,
  • Jinsia, na
  • Vinasaba kuwa na ndugu au mzazi aliyekuwa na presha;
  • Kuwa na magonjwa mengine kama kisukari na figo

Dalili za shinikizo la juu la damu-presha

Presha inajulikana kama muuaji wa kimya kimya. Presha inaweza kuwepo bila kuonesha dalili yeyote. Hivyo, wengi wenye presha hawatambui kama wana tatizo hili.

Kwahiyo, ni muhimu kupima presha mara kwa mara angalau mara mbili kwa mwaka. Hatahivyo, wagonjwa wa presha wemekuwa wakionesha dalili kama

  1. vile kuumwa kichwa asubuhi,
  2. kutoka damu puani,
  3. kizungu zungu,
  4. kuhisi mapigo ya moyo (kwa kawaida huwa hatuhisi moyo ukipiga-ukianza kuhisi unapiga kuna tatizo).

Kama presha ni kubwa sana utakuwa na

  1. uchovu,
  2. kichefuchefu,
  3. kutapika,
  4. kuchanganyikiwa,
  5. kuwa na wasiwasi,
  6. kuumwa na kifua na
  7. kutetemeka.

Nitafahamuje kama nina presha?

Utajuaje kama una presha? hili ni swali la muhimu kwasababu tumeona kwamba presha inaweza kuwa juu bila kuonesha dalili yeyote.

Kwakuwa wengi tunapelekwa hospitali na dalili tunayoiona au inayotuathiri, presha inatuonya kwamba tusisubiri dalili, tupime kila wakati!

Ukitaka kufahamu kama una shinikizo la juu la damu, inabidi upime shinikizo la damu kwa kutumia kipimo cha presha. Hapa chini nakufundisha namna ya kutafsiri majibu ya kipimo hichi.

Majibu huandikwa kwa mfumo wa namba mbili, ya juu na ya chini (X/Y).

Namba ya juu (X) ni shinikizo la damu wakati moyo umedunda (wakati unasukuma damu) na namba ya chini (Y) ni presha wakati moyo umetulia (wakati moyo unapokea damu).

Mtu anakuwa na shinikizo la juu la damu kama anakuwa na shinikizo linalosoma zaidi ya 139 kwenye namba ya juu na zaidi  89 kwenye namba ya chini.

Nifanye ninapogundulika nin shinikizo la damu la juu?

 

Unapogundulika na shinikizo la damu la juu daktari wako atafanya mambo mawili muhimu:

Jambo la kwanza litakuwa kukufanyia vipimo muhimu kwa mgonjwa wa presha.  Jambo la pili itakuwa kuanzishia mpango wa matibabu wa presha. 

Daktari atakufanyia vipimo hivi muhimu kutathmini hali ya ufanyaji kazi wa macho, figo, moyo:

  1. Fanya X-Ray ya Kifua: Kubaini kama kuna athari zozote katika moyo. Hichi ni kipimo cha mwanzo kwani X-Ray pekee haiwezi kutambua hitilafu zote zinazotokea kutokana na presha.
  2. Pima Sukari: Kuna uhusiano mkubwa kati ya presha na kisukari kama tafiti mbalimbali zinavyoonaesha. Kuwa na magonjwa yote kwa wakati mmoja huleta madhara zaidi kwa viungo muhimu.
  3. Pima hali ya Figo: Si tu presha huathiri figo bali wakati mwengine presha husababishwa na matatizo ya figo. Kwasababu hiyo ni muhimu sana kufahamu hali ya figo. Ukifanya hivi
  4. Pima macho: Kama tulivyoona macho pia ni sehemu ya viungo vinavyoathiriwa na presha. Hivyo ni muhimu kufahamu hali ya afya ya macho yako pindi unapogundulika una presha na wakati
  5. Kiwango cha mafuta kwenye damu: Baadhi ya mafuta yamenasibishwa na kusababisha presha. Kwasababu kuna dawa za kupunguza mafuta hayo, ni muhimu kufahamu kupima ili kupata dawa itakayokufaa.

Jiunge na Group Letu La WhatsApp Tujadiliane Kwa Pamoja Namna Ya Kudhibiti Presha na Kisukari


Nawezaje Kujikinga na presha na madhara yake?

Njia zinazopendekezwa kujikinga na presha na madhara yake ni

  1. Kufahamu presha yako: Jambo la kwanza na la umuhimu ni kufahamu presha yako “namba zako”. Tafiti zinaonesha wanaopima presha yao mara kwa mara na kufahamu presha zao wanaweza kuepuka na kudhibiti presha zao kuliko wasiofahamu. 
  2. Mfumo wa maisha: mlo,Tumia chumvi kidogo na usiongeze chumvi mezani (jiepushe na kula chumvi ambayo haijapikwa); kufanya mazoezi, punguza matumizi ya tumbaku na pombe
  3. Kula matunda na mbogamboga,  na vyakula vyenye mafuta mengi. punguza msongo wa mawazo,

Kama tayari unaugua presha fanya yafuatayo: 

  1. Fahamu namba zako – pima kila siku shinikizo lako la damu
  2. Fuatilia matibabu kwa ukamilifu-tumia dawa na hudhuria kliniki kama ulivyoshauriwa
  3. Badili mfumo wako wa maisha – badili/rekebisha aina na kiwango cha milo yako.
  4. Tibu magonjwa mengine kama unayo, haswa kisukari ili kupunguza hatari ya kupata madhara kwenye moyo na mishipa ya damu.

 

SAIDIA WENGINE

Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.

 

Ukiwa Tayari! Namna 3 tunasaidia kuboresha afya yako

  1. AFYAPlans inakuwezesha Kudhibiti na kuepuka madhara ya presha: Ungana na Daktari wako kwa msaada na mwongozo binafsi Kuhusu dawa, VIPIMO, maarifa na ujuzi. Bonyeza HAPA kujiunga grupu letu.
  2. Vitabu vya Elimu vinavyokuwezesha kufanya Maamuzi sahihi kuboresha afya yako. Mfano kudhibiti kisukari huku ukila Vyakula unavyovipenda. Bonyeza HAPA kufahamu zaidi
  3. Vifaa vya Matibabu ya Nyumbani vinavyokupa amani na uhakika wa afya yako muda wote. Bonyeza HAPA kuvifahamu.

Uko tayari kuboresha AFYA Yako? Tuwasiliane

HES-P-D-BDW-1_19016

HES-P-D-SET-D8_31212

HES-WB-01_12127

HES-P-D-DM-2_22878

DM-BP-01_12034

HES-P-D-BPA-12_18778

HES-CC-D-Nebul-1_11922

HES-CC-D-PO2-1_7479

HES-P-D-SET-6_4194

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Shinikizo La Damu La Juu – Presha?
Mimi ni Dr. Adinan