Kwanini Ufahamu Vipimo Muhimu kwa Mgonjwa wa Presha ?
Unaweza kudhibiti na kuepuka madhara ya presha. Hatahivyo, unaweza tu kufanikiwa kama utaweza kuchukua hatua stahiki mapema. Huwezi kuchukua hatua stahiki mapema mpaka ujue hali halisi.
Kitaaluma ya udaktari, unaweza kujua hali halisi ya afya ya mtu kwa kufanya vipimo husika. Lakini elimu hii haipo kwa wagonjwa wa presha. Kitu ambacho kimeendelea kusababisha madhara ya presha kama vile kiharusi nk.
Ili kuweza kuchukua hatua stahiki mgonjwa wa presha ni LAZIMA (Samahani kwa kutumia neno hili ila ndo UKWELI, na msema kweli…) ajue namna ya kubaini hali yake ya kiafya. Ajue vipimo muhimu vya kufanya.
Vipimo muhimu kwa mgonjwa wa presha
Ili kukurahisishia, nimegawanya vipimo muhimu mgonjwa wa presha anatakiwa kufanya kwenye makundi mawili.
Kundi la kwanza ni vipimo vya muda maalum ambavyo hufanyika hospitali, na kundi la pili ni vipimo ambavyo hutakiwa kufanyika mara kwa mara na ambavyo nakushauri kuwa navyo nyumbani.
Pima Presha Kwa Usahihi
Fahamu kiwango cha presha yako ya damu na chukua hatua stahiki mapema unapotumia kipimo cha chenye teknolojia ya hali ya juu.
Vipimo Muhimu Mgonjwa Wa Presha Anatakiwa Kufanya Hospitali
1.Kupima Presha: Kiwango chako cha presha ya damu ndiyo kiashiria kikubwa kwamba umeidhibiti ama la! Ni kwa kupima tu ndipo mtu atagundua kama presha iko juu. Tafiti zinaonesha wanaojipima mara kwa mara hudhibiti vizuri presha zao.
2. Pima kiwango cha sukari kwenye damu: Ili kuweza kufahamu kiwango cha sukari kwenye damu na kuweza kuidhibiti pamoja na kuepuka madhara yake inabidi uwe na mashine yako kuweza kupima sukari kila wakati unapotaka kufanya hivyo. Wagonjwa wa kisukari wako katika hatari ya kupata presha. Hivyo ni muhimu kufahamu kiwango chako cha sukari
3. Uwiano wa Uzito na Urefu: Uzito mkubwa huongeza hatari ya kupata au kutokuweza kudhibiti presha. Hivyo ni muhimu kufuatilia kwa ukaribu uzito wako na kufahamu uwiano wa urefu na uzito (BMI).
4. Vipimo muhimu kuchunguza afya ya Moyo
4. Chest X-Ray Moja ya vipimo muhimu kwa mgonjwa wa presha. NI muhimu kwa mgonjwa wa presha kufanya vipimo muhimu ili kuepuka shinikizo la juu la damu (presha) na madhara yakeFanya X-Ray ya Kifua: Kubaini kama kuna athari zozote katika moyo. Hichi ni kipimo cha mwanzo kwani X-Ray pekee haiwezi kutambua hitilafu zote zinazotokea kutokana na presha.
5. Kipimo cha umeme wa Moyo (ECG) Hichi ni kipimo ambacho hujulikana kwa kirefu kama electorkardiogram. ECG ni kipimo mahususi cha umeme wa moyo.
6. Echocardiogram (ECHO): Hichi ni kipimo ambacho huchunguza moyo unavyopokea na kusukuma damu. Huchunguza pia misuli ya moyo inavyosinyaa na kutanuka kusukuma damu.
Pia huchunguza na kupima ukubwa wa vyumba vya moyo pamoja na milango (valves) kama iko imara na kufanya kazi kama inavyotarajiwa.
7. Pima hali ya Figo: Presha huathiri figo na kuleta athari kubwa zingine kama kisukari. Kwasababu hiyo ni muhimu sana kufahamu hali ya figo. Daktari wako atakupima mkojo kama kipimo cha mwanzo kubaini hitilafu zilizopo
8. Mafuta yaliyopo kwenye damu. Cholesterole-pima kiwango cha mafuta kwenye damu kama una presha. Kiwango cha mafuta kwenye damu: Baadhi ya mafuta yamenasibishwa na kusababisha presha.
Mafuta haya, lehemu ndogo- huaribu mishipa na kufanya ikakamae. Kwasababu kuna dawa za kupunguza mafuta hayo, ni muhimu kufahamu kupima ili kupata dawa itakayokufaa.
9. Pima macho: Kama tulivyoona macho pia ni sehemu ya viungo vinavyoathiriwa na presha. Hivyo ni muhimu kufahamu hali ya afya ya macho yako pindi unapogundulika una presha na wakati
Vipimo Muhimu Mgonjwa Wa Presha kuwanavyo Nyumbani
Vipimo vitatu vya mwanzo ndiyo vipimo muhimu ninavyokushauri kuvitumia nyumbani mara kwa mara kuweza kubaini hali ya afya na kuchukua hatua stahiki mapema. Vipimo hivi ni
1. Kipimo cha Presha: Kiwango chako cha presha ya damu ndiyo kiashiria kikubwa kwamba umeidhibiti ama la! Ni kwa kupima tu ndipo mtu atagundua kama presha iko juu. Tafiti zinaonesha wanaojipima mara kwa mara hudhibiti vizuri presha zao.
2. Kipimo cha kisukari kwenye damu: Ili kuweza kufahamu hali yKipimo cha Sukari-Gluconaviiako ya kisukari na kuweza kuidhibiti pamoja na kudhibiti madhara yake inabidi uwe na mashine yako kuweza kupima sukari kila wakati unapotaka kufanya hivyo. Wagonjwa wa kisukari wako katika hatari ya kupata presha. Hivyo ni muhimu kufahamu kama presha yako imeshababishwa na kisukari
3. Kipimo Uwiano wa Uzito na Urefu: Uzito mkubwa huongeza hatari ya kupata au kutokuweza kudhibiti presha. Hivyo ni muhimu kufuatilia kwa ukaribu uzito wako na kufahamu uwiano wa urefu na uzito (BMI).
Ngoja nikuridhishe ni kwanini ni kwanini UNAHITAJI kufahamu hali yako tena ukiwa nyumbani
Kuwa na Vipimo Nyumbani Kunasaidiaje Kudhibiti na Kuepuka Madhara ya Presha?
1. Usiri wa presha: Huwenda ulishawahi kusikia kwamba presha ya kupanda au shinikizo la juu la damu ni muuaji wa kimyakimya! Kama ulishawahi kusikia au kama bado ngoja nikufafanulie vitu viwili muhimu sana.
Vitu ambavyo ukivifahamu unaweza kuepuka madhara ya presha kama vile figo kufeli na kiharusi. Kitu cha kwanza cha muhimu ni kwamba Presha haina dalili – presha inaweza kuwa juu kiasi cha kuweza kupasua mishipa ya damu kwenye ubongo bila wewe kuonesha dalili hata moja.
Kwa kutokuonesha dalili watu wengine wamekuwa na presha kwa muda mrefu bila kufahamu. Presha inapokuwa juu kwa muda mrefu bila matibabu yeyote inaathiri viungo muhimu sana kwa afya, furaha, uchumi na uhai wako.
Unaweza kuepuka madhara haya kwakuwa unakuwa umetatua sehemu kubwa sana ya fumbo la ugonjwa wa presha ya kupanda, kufahamu.
2. Presha ni ugonjwa wa muda mrefu – muda mwingi utakuwa nje au mbali na kituo cha afya. Yani ugonjwa utakuwa nao hata kama hauko hospitali. Ni muhimu wewe kuwa mstari wa mbele kuukabili na kuepuka madhara yake.
3. Kutathmini tiba kama inafanya kazi. Fikiria umetoka hospitali ambako ulikuwa umeongezewa dawa ya presha kwa kuwa ulipopimwa shinikizo la damu, presha yako ilikuwa juu. Umefika nyumbani, kama kawaida, wewe unafuata maelekezo ya daktari, unatumia dawa.
Ni bora dawa iwe inafanya kazi kama ilivyotegemewa – kushusha presha. Je, kama haishushi kama ile ingine uliyokuwa unatumia awali?
Ninachotaka kukueleza ni kwamba, kwa kupima tuu ndiyo utafahamu kama dawa iliyoongezwa inafanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Offer ya Muda Mfupi!
Pata Punguzo la TSh. 90,000/=
Kipimo cha Presha, Kisukari & Uzito
- Fuatilia sukari yako ukiwa nyumbani
- Fahamu kama tiba inafanya kazi
- Fahamu nini husababisha sukari kupanda
- Kuwa na amani
Ufanye Nini?
Nitafurahi ukinihakikishia hata kwa ishara kwamba kuanzia leo utataka kufuatilia presha yako. Ungependa kufahamu jambo la pili?
- Fahamu: Sasa ushafahamu kitu cha kwanza muhimu sana – kutaka kujua hali ya presha yako inakubidi upime tu! Jambo la pili la muhimu ni kuhakikisha unafahamu hali ya afya ya viungo hivi muhimu. Baada ya kugundua kwamba una shinikizo la juu la damu. Anza sasa kufuatilia afya yako ukiwa nyumbani na vifaa vyetu vyenye ubora na warranty.
- Fanya: Ukifahamu hali ya viungo hivi unaweza kudhibiti au kuzuia madhara kwa kuwa kuchukua hatua stahiki -mapema- kuepuka au kupunguza kasi ya uharibifu.
- Furahia maisha: Kila mtu anatamani kufurahia maisha. Unapokuwa na amani kuhusu afya yako, basi nasi tunafarijika kwani tumetimiza lengo letu la kukusaidia kushiriki mstari wa mbele kuboresha afya yako.
Lengo letu ni kukusaidia kushiriki mstari wa mbele kuboresha afya yako kwa kukupatia elimu sahihi na vifaatiba bora kwa ajili ya kufuatilia afya yako ukiwa nyumbani.
Tutafurahi ukituachia maoni yako kuhusu ujumbe huu na ukisambaza kwa unaowajali.
HES-P-D-BDW-1_19016
HES-P-D-SET-D8_31212
HES-WB-01_1212
HES-P-D-DM-2_22878
DM-BP-01_12034
HES-P-D-BPA-12_18778