Uchanganuzi wa dakika kumi huwezesha kutambua na kuponya sababu ya kawaida ya shinikizo la damu.
Madaktari katika Chuo Kikuu cha Queen Mary cha London na Hospitali ya Barts, na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Cambridge, wameongoza utafiti kwa kutumia aina mpya ya CT scan kubaini na kuondoa viuvimbe vidogo kwenye tezi ya adrenal na kuponya shinikizo la damu-presha.
Viuvimbe hivi hugunduliwa kwa mtu mmoja kati ya ishirini walio na shinikizo la damu la juu-presha.
Watu 128 walishiriki katika utafiti wa uchunguzi mpya baada ya madaktari kugundua kwamba shinikizo la damu la juu-presha lilisababishwa na homoni ya aldosterone ambayo hutolewa na viuvimbe kwenye tezi ya adrenali, ambayo inaweza kuondolewa bila madhara.
Uchanganuzi hutumia kipimo kifupi sana cha metomidate, rangi ya mionzi ambayo hushikamana tu na viuvimbe vinavyotoa aldosterone.
Viuvimbe vilivyokuwa vikitoa aldosterone nyingi zaidi vilikuwa vikitoa mwanga na hivyo kugundulika.
Profesa Morris Brown, mwandishi mwenza wa utafiti huo na Profesa wa Shinikizo la damu la Endocrine katika Chuo Kikuu cha Queen Mary cha London, alisema:
“Vinundu hivi vinavyotoa aldosterone ni vidogo sana na havionekani au hupuuzwa wakati wa CT scan ya kawaida. Hadi sasa, inakadiriwa kuwa 99% ya wagonjwa wenye viuvimbe hivi hawajatambuliwa bado kutokana na kutokuwepo kwa vipimo. Tunatumahi kuwa hii inakaribia kubadilika.”
Tezi la adrenal linafanya kazi gani?
Tezi za adrenali hutoa homoni iitwayo aldosterone. Aldosterone husababisha chumvi kubaki katika mwili, na kuongeza shinikizo la damu.
Utafiti huu unamaanisha nini kwenye mafanikio ya tiba ya shinikizo la juu la damu?
95% ya wagonjwa wa shinikizo la juu la damu-damu, chanzo hakijulikani, na hali hiyo inahitaji matibabu ya maisha kwa kutumia madawa.
Presha ya wagonjwa wanye kiwango kikubwa cha aldosterone ni ngumu kutibika kwa dawa zitumiwazo sana, na hatari ya kuongezeka kwa mshtuko wa moyo na kiharusi.
Utafiti huu unatoa fursa ya kupunguza yale tuliyokuwa hatuyajui kuhusu presha. Huwenda sasa wagonjwa asilimia 5% zaidi wataweza kupata tiba ya presha.
Nini chimbuko la utafiti huu?
Utafiti wa awali wa kikundi katika Chuo Kikuu cha Queen Mary uligundua kwamba katika 5-10% ya wagonjwa wa shinikizo la damu sababu ni mabadiliko ya vinasaba katika tezi za adrenal, ambayo husababisha kiasi kikubwa cha homoni ya aldosterone, kuzalishwa.
Ungependa kufahamu zaidi?
Bonyeza HAPA kusoma utafiti huu uliochapishwa na jarida la nature.