fuatilia. dhibiti. furahia maisha

furahia maisha

Boresha Afya yako na Uwapendao kwa Kutumia vifaatiba muhimu kuwa navyo nyumbani

Previous slide
Next slide

Nafahamu kwa kuwa wewe ni mtu makini, kuwa na afya bora inaendelea kuwa kipaumbele chako namba moja.

Kwa kuwa na afya bora unaweza kufanya shughuli zako za kidunia na kiimani. Na sisi AFYATech, kama unavyotufahamu tunaendelea kukusaidia kufikia lengo lako.

Leo tunakufahamisha orodha ya vifaatiba muhimu vitakavyokusaidia kuwa na afya bora kwa kufuatilia afya yako ukiwa nyumbani.

Pia tunakupa offer maalum, utaokoa 165,000/= utakapotaka kuchukua vifaatiba hivi!

Lakini, kwanza, kwanini tumeamua kukuandikia vifaa?

Sababu 3 zilizotusukuma kukuandikia orodha hii ni kama ifuatavyo:

  1. Licha ya kwamba kuwa na vifaa vitakuwezesha kufahamu kwa uhakika na kuchukua hatua stahiki kwa haraka panapotokea dharura ya afya. Si rahisi kwa mtu ambaye hana taaluma ya afya kuweza kuchagua aina ya vifaa anavyohitaji kuwa navyo nyumbani.
  2. Ingawa watu wengi tunakwenda hospitali tunapoona dalili ya ugonjwa, magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo hayana dalili. Hivyo ni muhimu sana kujenga utaratibu wa kufuatilia hali yako ya afya mwenyewe ukiwa popote.
    Mfano, watu wengi wamekuwa wakifariki au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na shinikizo la damu (presha) na kisukari kwasababu magonjwa haya yanaweza kuwepo kwa muda mrefu bila kuonesha dalili. Hivyo  wengi wanashtukizwa na kiharusi, matatizo ya moyo, figo na kutokuona nk.
  3. Licha unafahamu umuhimu wa kuwahi hospitali unapougua, huwenda hukai karibu na hospitali au hali ya afya inaweza kubadilika nyakati za usiku wakati ambao usafiri ni shida. Hivyo kwa kuwa na kipimo nyumbani unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa afya na kumueleza majibu ya kipimo na kuweza kuokoa maisha ambayo tungeyapoteza kwa kutokuwa tu na vipimo.

Ndiyo maana leo tumekuandalia orodha ya vifaa hivi na kukuwezesha kuwanavyo. Pia tunakupatia.

Kupata offer hii
1 – Bonyeza kitufe cha weka oda leo hapo juu kama unavihitaji vifaa vyote nane.

2- Kama unahitaji kimoja kati ya vifaa hivi, bonyeza kitufe cha weka oda leo kilichopo karibu na kifaa husika. 

Kipimo cha presha Automatic-BP Machine.

Kipimo cha Presha

Kipimo cha Shinikizo la damu (BP Machine): Takwimu zinaonesha kwa kati ya watu 10, wanne wana shinikizo la juu la damu. Pia, hatari ya kupata Shinikizo la juu la damu huongezeka zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 30 na zaidi.

Faida ya kuwa na kipimo cha presha ni kama ifuatavyo:

  • Epuka madhara yatokanayo na presha kwa kugundua mapema zaidi – Kuna Njia moja tu ya kuweza kutambua kama unashinikizo la juu la damu (presha) kujipima tu!
  • Fahamu maendeleo yako katika kudhibiti presha yako
  • Epuka msongamano hospitali – jipime ukiwa nyumbani
  • Unaweza kujipima presha ukiwa popote sasa. Kinabebeka na chaji inadumu   

TSh. 119,000/=

Kipimo cha Sukari

Kipimo cha sukari (Glucometer) ni muhimu kwani takwimu zinaonesha kati ya watu 100 basi SABA(7) huwa na kisukari. Na wengi huchelewa kufahamu kama wana kisukari.

Hata kama huna kisukari, ni vizuri kuwa na kipimo hiki

Faida ya kuwa na kipimo hiki cha sukari ni kama ifuatavyo:

  • Ishi kwa raha licha ya kuwa na kisukari huku ukiwa na kipimo kinachoongoza kwa usahihi wa matokeo
  • Utaweza kufahamu maendeleo yako katika kudhibiti sukari
  • Epukana na vidonda kwenye vidole – mashine hii hutumia pini ndogo sana
  • Muundo mzuri wa kuvutia

TSh. 44,900/=

Kipimo cha Sukari-Gluconavii
Weighing Scale -Kipimo-cha-Uzito-Black

Kipimo cha uzito

Epuka magonjwa kwa kufuatilia na kudhibiti uzito wako. Faida ya kuwa na kipimo chiki cha uzito ni kama ifuatavyo:

  • Fahamu uziito wako kwa uhakika
  • Epuka madhara ya uzito mkubwa kwa kuchukua hatua stahiki mapema
  • Tathmini kama njia unazotumia kupunguza uzito zinafanya kazi kama ulivyotegemea
  • Battery hukaa muda mrefu na mnaweza kutumia zaidi ya mtu mmoja
  • Ina muundo wa kuvutia sana. Itapendezesha mandhari ya unapoiweka

TSh. 58,900/=

Unaweza kutuamini!

Tunaaminika

Tangu 2016 tunasaidia watu kufikia malengo yao ya kiafya

Ushauri

Wa Kitaalamu Kuhusu Vifaa Unavyohitaji.

Lipa baada

ya kupokea na KURIDHIKA na vifaa ulivyoagiza

Warranty

Zaidi ya mwaka. Tutakusaidia hata baaada ya warranty kuisha

Kipima joto / Thermometer

Kipima joto (Thermometer) – kama jina linavyosema, kipimo hichi hupima joto la mwili. Badala ya kukadiria joto la mwili kwa mkono, ni muhimu kupata kipimo sahihi cha joto, haswa kwa watoto na wagonjwa wa kisukari

Mtu atakuwa na homa kama joto lake ni zaidi ya 36.9⁰C. Kama hutokumbuka basi kuna thermometer ambayo hubadili rangi kulingana na majibu ya kipimo: kama mtu ana homa huwa nyekundu na huwa kijani kama joto liko sawa.

  • Fahamu kwa uhakika kama una homa ama la
  • Ni rahisi kutumia. Hubadilika rangi na kuwa nyekundu kama mtu ana homa, na huwa ya kijani kama joto lako ni la kawaida
  • Epuka madhara ya homa hasa kwa watoto wadogo
  • Battery hukaa muda mrefu sana! Haivunjiki kwa urahisi na ina muundo mzuri wa kuvutia

TSh. 19,900/=

Kipimo cha Uwiano wa Uzito na Urefu

Kipimo cha Uwiano wa Uzito na Urefu

  • Fahamu uziito wako kwa uhakika
  • Epuka madhara ya uzito mkubwa kwa kuchukua hatua stahiki mapema
  • Tathmini kama njia unazotumia kupunguza uzito zinafanya kazi kama ulivyotegemea
  • Unaweza kutumia muda wowote na haihitaji nishati yeyote
  • Unaweza kwenda nayo popote

TSh. 14,900/=

Kipimo cha kiwango cha Oxygen kwenye damu

Faida ya kuwa na kipimo cha oxygen kwenye damu ni kama ifuatavyo:

  • Epuka madhara yatokanayo na kupungua kwa oxygen mwilini!
  • Fahamu maendeleo yako katika kudhibiti tiba unayotumia
  • Epuka msongamano hospitali – jipime ukiwa nyumbani
  • Unaweza kujipima kiwango cha oxygen ukiwa popote sasa Kinabebeka na chaji inadumu  

TSh. 53,900/=

Kipimo cha Oxygen kwenye damu - pulse oximeter
Nebulizer Mesh Portable Nebulizer-HES-NEB-01

Nebulizer

Kifaa utakachokitumia ili kupata nafuu ya haraka na epuka madhara ya pumu. Nebulizer ni kifaa ambacho kinatumika kupeleka dawa kwenye mapafu.

Faida ya kuwa na nebulizer ni kama ifuatavyo:

  • Hivyo unapokuwa na nebulizer utapata ahueni haraka.
  • Pia, huhitaji kutumia nguvu kuvuta dawa ndani kama ambavyo huwa wakati unapotumia inhaler, hii ni kwasababu kifaa hichi maalum hutoa mvuke na presha ambayo husaidia kuisukuma dawa moja kwa moja kwenye mapafu.
  • Ni rahisi kutumia na
  • Unaweza kuwa nacho wakati wote na popote! Ni kama unatembea na hospitali na watoa huduma wa afya! 

TSh. 148,900/=

Urafiki na mwanao Akiwa tumboni

Kusikia mpigo wa moyo ya mtoto wako kwa mara ya kwanza huleta faraja usiyoweza kusahau.

  • Sikiliza mapigo ya moyo wa mtoto wako popote, wakati wowote ukitumia kifaa cha fetal Doppler.
  • Haijalishi una shughuli nyingi kiasi gani, shikamana na mtoto wako katika kipindi chote cha ujauzito ukitumia Fetal Doppler; kifaa hiki cha kusikilizia mapigo ya moyo ya mtoto wazazi wanaweza kutegemea.

TSh. 249,000/=

Fetal doppler - kipimo cha mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni

HES-P-D-BDW-1_19016

HES-P-D-SET-D8_31212

HES-WB-01_1212

HES-P-D-DM-2_22878

DM-BP-01_12034

HES-P-D-BPA-12_18778

Tafadhali Sambaza Ujumbe huu
Facebook
Twitter
WhatsApp
Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Vifaatiba Muhimu Kuwa Navyo Nyumbani-Home Kits?
Mimi ni Dr. Adinan