Presha ni nini?
Presha ni shinikizo la damu la juu. Tulifahamu kwamba shinikizo la damu ni msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu. Hii ni sawa na maji yanavyohitaji msukumo ili kupita kwenye mpira.
Kama presha ni ndogo sana, damu haitafika kwa viungo muhimu. Vivyo hivyo, kama presha ni kubwa sana, inaweza kuharibu mishipa ya damu na kusababisha madhara makubwa kwa afya.
Tukusaidie Kudhibiti Presha?
Muulize Dr. Adinan sasa akushauri namna sahihi ya kudhibiti Presha. Utalipia TSh. 4900/= tu!
Presha ya Kawaida ni Ngapi?
Kiwango cha Presha Mwilini
Presha ya kawaida ya damu ni 120/80 mmHg. Namba ya juu (120) inaitwa systolic, ambayo ni presha wakati moyo unasukuma damu.
Namba ya chini (80) inaitwa diastolic, ambayo ni presha wakati moyo unapumzika kati ya mipigo. Ikiwa presha yako ni zaidi ya 130/80 mmHg, ni muhimu kuchukua hatua za kudhibiti.
Madhara ya Presha
Shinikizo la juu la damu linaweza kusababisha matatizo makubwa kama vile:
- Ubongo: Kiharusi
- Moyo: Shambulio la moyo au moyo kushindwa kufanya kazi
- Macho: Kupoteza uwezo wa kuona
- Figo: Kushindwa kufanya kazi vizuri
Aina za Presha
- Shinikizo la Juu la Damu la Sekondari
Shinikizo la juu la damu linalosababishwa na hali maalum ya kiafya kama ugonjwa wa figo au matatizo ya tezi. Hii ni nadra na inajulikana kwa wagonjwa wachache. - Shinikizo la Juu la Damu la Msingi
Aina hii ya shinikizo la damu haina sababu maalum inayoeleweka. Inachangia idadi kubwa ya wagonjwa wa shinikizo la damu, takriban 90%. - Presha ya Hofu
Hii hutokea wakati mtu anapokuwa na wasiwasi au hofu, mara nyingi wakati wa kupima presha hospitalini.
Nini Cha Kufanya Unapogundulika na Presha?
- Pima Mara kwa Mara: Hakikisha unapata vipimo vya kawaida ili kufuatilia mabadiliko ya presha yako.
- Badilisha Mtindo wa Maisha: Punguza matumizi ya chumvi, ongeza mazoezi, na kula vyakula vyenye afya.
- Tumia Dawa Kama Ulivyoelekezwa: Fuata maelekezo ya daktari kuhusu matumizi ya dawa.
Kufahamu maana ya shinikizo la damu na jinsi ya kudhibiti ni hatua muhimu kwa kudumisha afya bora. Hakikisha unapata vipimo vya mara kwa mara na kufuata ushauri wa daktari ili kuepuka matatizo makubwa yanayoweza kusababishwa na shinikizo la juu la damu.
Fahamu Wastani wa Presha Yako
Unahitaji kujipima presha ukiwa nyumbani. Ni muhimu hata kwa wale ambao si wagonjwa wa presha. Lengo ni wewe kuwa na afya bora!
Ili kuidhibiti na kujikinga na madhara ya presha kama vile kiharusi, kufeli figo nk. ni muhimu kujua presha yako kwa uhakika.
Kujipima presha ukiwa nyumbani ni njia ya kuaminika na inayoshauriwa kukuwezesha kufahamu wastani halisi wa presha yako.
Wastani wa Presha Una Umuhimu Gani?
Nafahamu unajiuliza, kuna utofauti gani ya presha yangu nikiwa nyumbani na ile ya hospitali?
Tafiti zinaonesha kwamba sasa watu 3 kati ya 10 wenye umri wa miaka 30 na zaidi wana presha.
Wakati mwengine presha hii hujificha (masked hypertension). Yani wanakuwa na presha ya kawaida wanapopimwa hospitali lakini wakiwa nje ya hospitali presha yao hupanda.
Na wakati mwengine huwa kubwa hospitali na hurudi katika hali ya kawaida unapokuwa nyumbani.
Dhibiti Presha Unapojipima Nyumbani
Tunaamini kwamba mtu huweza kudhibiti anachokijua / kifahamu. Ikiwa nawe unaamini hivi utakubaliana kabisa kwamba kufahamu presha ni moja ya kitu cha muhimu kinachoweza kukusaidia kufanya maamuzi.
Ikiwa unaamini kama sisi kwamba presha ni hatari basi utachukua hatua kudhibiti hatari hii. Naaamini kwamba hauamini kinyume chake kwamba presha si hatari.
Hatahivyo, ningependa kukupa sababu 3 zinazokufanya wewe kufikiri kuhusu kufahamu hali yako ya presha haswa ukiwa nyumbani.
Kuna sababu mbili muhimu kwanini ujipime presha ukiwa nyumbani.
- Hakuna namna ingine ya kufahamu kama una presha. Presha hubadilika badilika.
- Shinikizo la damu la juu / presha haina dalili au dalili za onyo hivyo watu wengi hawajui wanayo.
- Presha inapokuwa juu huendelea kuleta madhara licha ya kwamba unaweza usione dalili
Hivyo, kupima shinikizo la damu ndiyo njia pekee ya kujua ikiwa una shinikizo la damu.
Epuka Madhara ya Presha Unapopima Nyumbani
Kulingana na majibu ya presha yako, unaweza kuchukua hatua stahiki mapema. Mfano kama presha yako itakuwa kubwa utajua kwamba inatakiwa kushushwa.
Vile vile ikiwa uko kwenye matibabu utafahamu ufanisi wa matibabu. Kwa hali hii utaweza kuwasiliana na daktari wako na kurekebisha aina ya matibabu au kuendelea nayo.
Dondoo kwa anayepima shinikizo la damu nyumbani
Fuata dondoo hizi muhimu ili ufaidike na kupima shinikizo la damu nyumbani:
- Wasiliana na tabibu wako kumtaarifu kuwa unapima presha yako nyumbani.
- Rekodi vipimo vya shinikizo la damu kila unapopima
- Jipime shinikizo la damu kwa wakati mmoja kila siku.
- Pima angalau mara mbili, ndani ya dakika tano
- Ikiwa una wasiwasi juu ya nambari zako za shinikizo la damu, wasiliana na mhudumu wa afya anayekuhudumia.
- Hakikisha usahihi wa majibu ya kipimo: tumia mashine sahihi na ujipime kwa njia sahihi.
Haijalishi umri wako, unaweza pia kuchukua hatua kila siku kusaidia kuweka shinikizo la damu yako katika safu nzuri.