fuatilia. dhibiti. furahia maisha
furahia maisha
Anza safari ya kuelekea Afya bora kwa kuwa na
- Elimu sahihi
- Usaidizi wa moja kwa moja, na
- Vifaa tiba muhimu kufuatilia afya yako nyumbani.
Jiunge PreshaPlan Sasa!
Fahamu
- Ushauri wa Wiki kwa simu au ujumbe wa WhatsApp
- Kuunganishwa kwenye Jukwaa la mtandaoni.
- Kusoma makala zote kuhusu kisukari na presha na magonjwa mengine kwenye tovuti ya AFYATech
- *Vipimo muhimu kufuatilia na kudhibiti kisukari ukiwa nyumbani kwa bei ya punguzo
Fanya
- Huduma zote kwenye mpango wa Fahamu, na
- Uchambuzi wa vyakula unavyopendelea kula na ushauri
- Ratiba / Mpango wa chakula kulingana na vyakula unavyovipenda kwa wiki
- Ushauri mahususi wa namna ya kuepuka madhara ya kisukari ikiwemo kufanyiwa tathimini ya tiba
Furahia
- Huduma zote kwenye mpango wa Fanya, na
- Kitabu kitakachokufundisha nini cha kula na namna ya kuchanganya vyakula bila kupandisha sukari
- Kuletewa vipimo ulivyoagiza ulipo
- Punguzo la bei ya glucose strips popote utakapokuwepo
Kwanini Wanafanikiwa?
Elimu sahihi
Kufahamu vyakula, tabia za mtindo wa maisha, tiba na athari na namna ya kuziepuka
Ushauri mahususi
Kulingana na mahitaji yako na hali yako ya afya. Kwamfano tunatumia vyakula unavyopenda
Msaada wa mojaa kwa moja
Kutoka kwa wataalamu wetu watakaohakikisha umeelewa na kutenda
Amani
Kulingana na unavyoshiriki. Huna hofu. Una mtaalamu wako wakati wowote!
Una Maswali haya?
Hii ni programu ya muda gani?
AFYA-Plan ni programu ya miezi sita (6), hatahivyo unaweza kuzidisha kadiri unavyopenda na kuona ina manufaa.
Kuna faida gani kuweka oda yangu online?
Unaweza kutoka muda wowote iwapo utaona umefuzu. Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwezesha kudhibiti afya yako mwenyewe ukiwa nyumbani. Tunashauri angalau utoke baada ya miezi mitatu, ila kama unaona umefuzu unaweza kutoka muda wowote!
Nyie ni hospitali?
AFYATech si hospitali na bado haina hospitali kwasasa. Kazi yetu ni kuendelea pale ambapo hospitali zimeishia. Tunakuhakikishia afya bora nyumbani. Tutakushauri kila wakati. Unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana moja kwa moja na wahudumu wetu!
Nifanye nini kama sijakipenda kifaa mlichonipatia?
Lengo letu ni kukuwezesha kukupa elimu sahihi, kukuwezesha kuchukua hatua stahiki na kukukwezesah kudhbiti magonjwa haya. Ikiwa programu hii haina tija baada ya kujifanyia tathmini unaweza kujitoa na tutakurudishia pesa yako ndani ya mwezi mmoja.
Nalipiaje bidhaa ili nizipate?
Unaweza kulipa kabla au mara tu baada ya kupokea bidhaa yako. Hii ni kwasababu ya kutunza uaminifu na kukupa uhuru wa kuagiza bila stress
Mtanifundisha Kutumia VIfaa hivi?
Bila shaka. Lengo letu ni kukusaidia kuboresha afya yako na ya watu unaowathamini. Tumetengeneza video za maelekezo. Pia tutakuelekeza moja kwa moja kama video haitoshi.
Mnapatikana wapi?
Moshi-HQ,
Dar – Agent,
Mwanza – Agent,
Dodoma – Agent,
Arusha – Agent
Singida – Agent,
Morogoro – Agent,
Ifakara – Agent,
Mbeya – Agent, na
Zanzibar – Agent.
👉Kwingine kote tunasafirisha ndani ya saa 24.
Vifaa vimetengenezwa wapi?
Tuna vifaa kutoka India, China, Uturuki, South Korea nk. Hatahivyo, sisi tumejikita kwenye ubora zaidi kuliko sehemu bidhaa imetoka. Na tumekuwa tukitumia majibu ya tafiti kuamua bidhaa ya kuagiza kwa ajili ya matumizi yako na kwa watu unaowathamini.
Rejesha Furaha ya Kula!
Jiunge na Fahamu tukupatie uchambuzi kama mlo wako wa sasa unaweza kukusaidia kushusha presha. Tutakupatia uchambuzi huu BUURE KABISA!
Kutoka kukufahamisha uhusiano wa vyakula na kisukari hadi ushauri wa kiasi na mwishowe mpango mkakati wa vyakula, tunakupa njia ya kufurahia vyakula vyako pendwa bila kuongeza viwango vya sukari yako.