Kufahamu virutubisho vilivyomo kwenye chakula ni vizuri na unapata manufaa mengi. Lakini, ni rahisi kuelewa na kupanga mlo wako kwa kutumia uhalisia kwa sababu kuu tatu.
- Tunaona kwanza chakula: Ukweli usiopingika kwamba tunapokwenda sokoni tunalenga kununua mchicha na si Vitamin A na pia tunanunua nyama tunapo kwenda buchani badala ya kusema nakwenda kununua protini.
- Kiwango cha virutubisho hutofautiana baina ya vyakula, lakini ya tatu na ya muhimu zaidi ni kwamba
- Vyakula karibia vyote huwa na aina tofauti ya virutubisho. Namaanisha kwa mfano maharage yana protini, wanga na mafuta na vitamini mbalimbali vilevile muhindi una wanga, mafuta na protini na vitamini mbalimbali.
Kwenye kitabu hiki tumezingatia maisha yetu ya kila siku hivyo kukusaidia msomaji kufahamu kwa uhakika na kuweza kupanga bila hofu aina ya mlo unaoutaka ili kuweza kuboresha afya yako bila kuathiri kiwango chako cha sukari.
Jipatie kitabu kinachokuwezesha kudhibiti kisukari huku ukila vyakula uvipendavyo.
Reviews
There are no reviews yet.