Kufahamu virutubisho vilivyomo kwenye chakula ni vizuri na unapata manufaa mengi. Lakini, ni rahisi kuelewa na kupanga mlo wako kwa kutumia uhalisia kwa sababu kuu tatu.
- Tunaona kwanza chakula: Ukweli usiopingika kwamba tunapokwenda sokoni tunalenga kununua mchicha na si Vitamin A na pia tunanunua nyama tunapo kwenda buchani badala ya kusema nakwenda kununua protini.
- Kiwango cha virutubisho hutofautiana baina ya vyakula, lakini ya tatu na ya muhimu zaidi ni kwamba
- Vyakula karibia vyote huwa na aina tofauti ya virutubisho. Namaanisha kwa mfano maharage yana protini, wanga na mafuta na vitamini mbalimbali vilevile muhindi una wanga, mafuta na protini na vitamini mbalimbali.
Kwenye kitabu hiki tumezingatia maisha yetu ya kila siku hivyo kukusaidia msomaji kufahamu kwa uhakika na kuweza kupanga bila hofu aina ya mlo unaoutaka ili kuweza kuboresha afya yako bila kuathiri kiwango chako cha sukari.
Kitabu hiki kina sura zifuatazo
- Uhusiano wa Vyakula na Kisukari: Sura hii inachunguza jinsi vyakula vinavyoathiri kiwango cha sukari mwilini na jinsi ya kuchagua vyakula bora kudhibiti kisukari.
- Je, Mgonjwa wa Kisukari anaweza Kula Vyakula vya Wanga?: Sura hii inajibu swali muhimu kuhusu uwezekano wa wagonjwa wa kisukari kula vyakula vya wanga na mbinu za kufanya hivyo kwa usahihi.
- Protini na Kisukari: Mwongozo wa Lishe Bora kwa Mgonjwa wa Kisukari: Inaelezea umuhimu wa protini katika lishe ya mgonjwa wa kisukari na jinsi ya kuijumuisha kwa usahihi katika mlo.
- Mafuta: Mgonjwa wa Kisukari Ale Mafuta ya Aina Gani?: Hutoa mwongozo wa kuchagua aina sahihi za mafuta kwa wagonjwa wa kisukari na jinsi ya kudhibiti ulaji wa mafuta.
- Matunda kwa Mgonjwa wa Kisukari: Inajadili jinsi ya kuchagua na kudhibiti ulaji wa matunda kwa wagonjwa wa kisukari ili kudumisha viwango vya sukari mwilini.
- Vinywaji Bora kwa Mgonjwa wa Kisukari: Inatoa mwanga kuhusu vinywaji ambavyo ni salama na vinavyofaa kwa wagonjwa wa kisukari kudumisha afya bora.
- Mlo Bora kwa Mgonjwa wa Kisukari: Inajumuisha mwongozo wa kuanzisha mlo bora kwa wagonjwa wa kisukari, pamoja na mapishi na mbinu za kupanga milo.
- Sahani Yako: Mambo ya Kuzingatia Kuhusu Mlo Unaofaa kwa Mgonjwa wa Kisukari: Inatoa mwongozo wa kuzingatia vipengele muhimu vya sahani katika kudumisha mlo bora kwa wagonjwa wa kisukari.
- Hatua 5 za Kufuata Uweze Kubadilisha Mlo Wako na Kudhibiti Kisukari: Hutoa hatua rahisi na za vitendo za kubadilisha mlo ili kudhibiti kisukari na kudumisha afya bora.
- Dhibiti na Epuka Madhara ya Kisukari: Inashughulikia mbinu za kudhibiti na kuepuka madhara ya kisukari kwa kuzingatia lishe na mbinu za maisha.
Jipatie kitabu kinachokuwezesha kudhibiti kisukari huku ukila vyakula uvipendavyo.
ABEID FUNDI (verified owner) –
0757915531