fbpx

Kiharusi ni nini?

Kiharusi ni ugonjwa unaotokea kwenye ubongo kwasababu ya kukosa damu kwa muda. Kiharusi ni moja ya madhara ya presha na kisukari.

Kuna aina tatu za kiharusi:

  • Kiharusi cha ghafla cha muda mfupi. Aina hii ya kiharusi hutokea kwasababu ya ukosefu wa damu wa muda mfupi kwenye ubongo. Hali hii huisha baada ya muda na hali hurejea kama kawaida
  • Kiharusi kinachotokea kwasababu mishipa ya damu kuziba cha (hufahamica kama Ischemic stroke) ni aina ya kawaida ya kiharusi, ambapo kuganda kwa damu huzuia mtiririko wa damu kwenye ubongo,
  • Kiharusi husababishwa na mshipa wa damu kupasuka na damu kuingia kwenye ubongo (hemorrhagic stroke).

Kiharusi husababishwa na nini?

Kiharusi husababishwa na kutokufika kwa damu sehemu ya ubongo.

Ikiwa mshipa wa damu unaopeleka damu kwenye sehemu ya ubongo ukaziba au kupasuka mtu yuko hatarini kupata kiharusi kama hajapata tiba haraka.

1.Kiharusi kinachotokea kwasababu mishipa ya damu kuziba husababishwa na mshipa wa damu kukamaa au kitu chochote kinachoweza kuziba mshipa.

Vitu vinavyoweza kuziba mshipa wa damu wa kwenye ubongo ni kama vile damu iliyoganda kwenye ubongo au sehemu ingine ya mwili na kusafiri mpaka kwenye ubongo.

Kiharusi kinachotokea kwasababu ya mshipa wa damu kuziba ndiyo aina ya kiharusi kinachotokea mara nyingi zaidi.

2. Kiharusi kinachotokea kwasababu sehemu ya mshipa wa damu kupasuka au damu kuvuja

Aina hii ya kiharusi husababishwa na vitu mbalimbali kama nilivyoviainisha hapa chini:

  • Kuwa na shinikizo la juu la damu: Shinikizo la damu linaweza kusababisha mishipa ya damu kwenye ubongo kusinyaa au kupasuka.
  • Mishipa ya damu inapopasuka au kukakamaa huongeza hatari ya sehemu za ubongo kukosa damu na kusababisha kiharusi.
  • Majeraha: Kuumia kwenye ajali moja kwa moja kwenye mshipa wa damu husababisha damu kuvuja na hivyo kutokufika kwenye sehemu ya ubonngo. 
  • Dawa: Matumizi ya dawa zinzozuia damu kuganda yanahusishwa na kiharusi.
  • Magonjwa ya mishipa: Baadhi ya magonjwa ya mishipa mishipa kutanuka kunaweza kufanya mshipa wa damu kuvuja au kupasuka.

Dalili za kiharusi ni zipi?

Ubongo ni kiungo kinachoratibu shughuli zote za mwili na unawajibika kwa mawazo yetu yote, mienendo, na hisia.

Ubongo umegawanyika katika sehemu tofauti mbalimbali, kila sehemu ikiwajibika kwa kazi maalum.

Kwa mfano, sehemu yenye kudhibiti mienendo ya hiari kama kuongea, na sehemu zenye kushughulikia hisia kutoka kwenye sehemu mbalimbali za mwili.

Njia moja ya kuelewa kazi tofauti za ubongo ni kupitia picha ya ubongo ikionesha sehemu za ubongo zinazohudumia sehemu mbalimbali za mwili (Homonculus)Picha ya ubongo ikionesha sehemu za ubongo zinazohudumia sehemu mbalimbali za mwili (Homonculus). Picha hii inaonyesha uwakilishi wa mwili wa mwanadamu katika ubongo, ambapo ufanyaji kazi wa kila kiungo cha mwili huakisi kiwango cha nafasi inayochukua kwenye ubongo.

Kwa mfano, mikono na mdomo vinawakilishwa kwa sehemu kubwa kuliko miguu na mgongo, kuonyesha ukubwa wa kazi ya mdomo katika kuhisi na wa mikono kufanya kazi.

Hivyo, shinikizo la damu linapoharibu mishipa ya damu katika ubongo, inaweza kusababisha dalili mbalimbali za mishipa ya fahamu, kulingana na eneo na ukubwa wa uharibifu. 

Kwahiyo mgonjwa ataona dalili ambazo ni madhara ya kiharusi.

Madhara ya kiharusi

Madhara ya kiharusi kwenye sehemu ya ubongo husababisha mapungufu ambayo ndizo dalili za kiharusi. Madhara haya yanaweza kutofautiana lakini mara nyingi hujumuisha 

  • Udhaifu wa ghafla au kufa ganzi upande mmoja wa mwili, 
  • Ugumu wa kuzungumza au kuelewa mazungumzo, 
  • Matatizo ya kuona, na 
  • Kuhisi kizunguzungu au kutokuweza kusimama
  • Uso kwenda upande 
  • Udhaifu kwenye mikono au miguu
  • Kichwa kuuma sana

Uangalizi wa kimatibabu wa haraka ni muhimu mtu anapopata kiharusi, kwani matibabu ya haraka yanaweza kusaidia kupunguza uharibifu wa ubongo na kuboresha matokeo ya tiba.

Ni muhimu kukumbuka kwamba wakati mwengine mgonjwa anaweza asioneshe dalili zozote au wakati mwengine akafariki mojakwamoja baada ya kupata kiharusi. 

Mtu anapimwaje kutambua aina ya kiharusi? 

Utambuzi wa kiharusi mara nyingi huhusisha vipimo vifuatavyo:

  1. Kipimo cha picha ya ubongo kufahamu sehemu na madhara yalipotokea. Vipimo hivi ni CT Scan au uchunguzi wa MRI.
  2. Kipimo cha moyo cha picha kipimo hiki huchunguza kama kuna damu iliyoganda kwenye vyumba vya moyo
  3. Kipimo cha lehemu kwenye damu yako kubaini aina na viwango vya lehemu vilivyopo
  4. Kipimo cha chembechembe za damu hufanywa kuchunguza ugandaji wa damu yako
  5.  Kipimo cha sukari kwenye damu yako. Kumbuka kisukari ni moja ya vihatarishi kwa mtu kupata kiharusi
  6. Kipimo cha shinikizo la damu kubaini kiwango chake  

Je, kuna tiba ya kiharusi?

Matibabu ya kiharusi yamegawanyika katika sehemu kuu mbili: 

  1. matibabu ya mwanzo-kuzuia uharibifu usiendelee na
  2. matibabu ya baada – kurejesha uwezo wa viungo kufanya kazi.

Matibabu ya kiharusi ya mwanzo

Chaguo la matibabu ya mwanzo hutegemea aina ya kiharusi. 

Kiharusi cha ghafla cha muda mfupi na kiharusi kinachotokea kwasababu ya mshipa kuziba

Aina hizi mbili za kiharusi hutokea kwasababu damu imeganda. Na lengo la matibabu ni kuondoa damu iliyoganda. 

  • Dawa zinazotumika ni za kuyeyusha mabonge ya damu kushusha presha, kupunguza lehemu
  • Wakati mwengine inaweza kuhitaji operesheni, ya kuzibua mishipa kwa kuvuta bonge la damu nje ya mwili
  • Kama mshipa umekakamaa na kupungua njia, tabibu anaweza kuweka kifaa kinachotanua na kuongeza mduara wa mshipa

Matibabu ya Kiharusi Kilichosababishwa na Damu Kuvuja

Kiharusi kilichotokea kwasababu ya damu kuvuja kwenye ubongo hutibiwa kwa kuziba sehemu inapovuja. Kuna namna nyingi ambazo matabibu hufanya ili kuziba mishipa hii. 

Wakati mwengine matabibu hutumia dawa kinzani za zile zinazosababisha damu kuyeyuka hutumika ili kuruhusu damu kuganda. 

Matibabu ya Kiharusi ya baada 

Lengo la matibabu ya baada ya kiharusi ni kurejesha uwezo wa viungo kufanya kazi ikiwa ulipotea.

  • Mgonjwa huweza kuhitaji mafunzo ya namna ya kuongea vizuri, kutembea na hata utambuzi.
  • Wakati mwengine matibabu hujumuisha kujifunza tena jinsi ya kufanya kazi za kila siku kwa kutumia viungo ambavyo havijaathirika. Hii inaweza kuhusisha tiba kwa njia ya mazoezi ya kimwili, tiba kwa njia ya ya kazi, na tiba ya kutumia umeme kwa vituo vya afya vyenye vifaa vya kisasahotuba.
  • Huduma za uuguzaji wa nyumbani kwa mgonjwa wa kiharusi pia ni muhimu. Ni muhimu kwa anayemuuguza mgonjwa wa kiharusi kufahamu dondoo muhimu ili kutoa huduma bora na kuboresha afya ya mpendwa wake. 

Mtu anaweza kurejea hali yake ya zamani baada ya kupata kiharusi?

Uponaji wa kiharusi hutegemea sana uharibifu uliotokea kwenye ubongo. Ikiwa uharibifu ulikuwa mkubwa, mtu hatoweza kurudi katika hali yake alivyokuwa kabla ya kupata kiharusi.

Hapa inabidi, baada ya kiharusi, mtu aendelee na huduma za kitabibu huku mwili ukiendelea kujikarabati na uwezo uliopotea kurejea.

Nawezaje kujikinga na kiharusi?

Ni muhimu kuzingatia kwamba, wakati mgonjwa wa kiharusi anauguzwa anatakiwa kuendelea kuchukua hatua ikijumuisha hatua za kuzuia kupata kiharusi kwa mara nyengine.

Ni muhimu kufuatilia na kudhibiti siku zijazo kama vile shinikizo la damu na kisukari, udhibiti wa kolesteroli, kuzingatia lishe bora na mazoezi, na kufuata matumizi sahihi ya dawa na kuacha vihatarishi vinavyowezakusababisha presha au sukari kuwa juu. .

Kuepuka kiharusi kunahusisha kudhibiti shinikizo la damu na kuepuka vihatarishi vingine kama vile kuvuta sigara, kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu /cholesterol kwenye damu, na kisukari.

Ufuatiliaji wa mara kwa mara wa shinikizo la damu na marekebisho ya mtindo wa maisha inaweza kusaidia kuzuia shinikizo la damu na kupunguza hatari ya kiharusi.

 

SAIDIA WENGINE

  • Tutafurahi kusikia maswali au maoni yako kuhusu makala haya. Tafadhali tuandikie hapo chini.
  • Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.
 
Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Kiharusi ni ugonjwa gani? Fahamu uweza kuepuka?
Mimi ni Dr. Adinan