Pulse oximeters (PO2) inapima kiwango cha hewa ya oxygen (O2) kilicho kwenye damu. PO2 inapima kiwango cha hemoglobin kilichobeba O2.
Upumuaji
Bila shaka unafahamu kwamba viumbe hai, ikiwemo binaadamu, huitaji hewa ya Oxygen (O2) ili kuishi. Na pia hutoa hewa Carbon Dioxide (CO2) kama uchafu. Hewa hizi hubebwa katika damu. Binadamu huvuta hewa ya O2 kwa kutumia pua. Hewa hii huingia katika mapafu. O2 hutoka kwenye mapafu na huingia katika damu na kupelekwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo ubongo. Katika damu, Oxygen na CO2 hubebwa na hemoglobini. Unaweza fikiria kwamba O2/CO2 ni abiria, hemoglobini ni gari na mishipa ya damu ni barabara. CO2 hutoka katika damu na kuingia kwenye mapafu na kupumuliwa nje ya mwili.
Ugonjwa wowote unaoathiri mfumo wa upumuaji hupunguza kiwango cha O2 na hivyo kuhatarisha uhai wa mtu. Magonjwa kama pumu, moyo, vichomi (pneumonia), TB na hivi sasa Corona, kwa uchache huathiri mfumo wa upumuaji.
Namna P02 inavyofanya kazi
P02 hutumia miale ya mwanga kupima kiwango cha oxygen kilichobebwa na hemoglobin. Mianga iko ya aina mbili, ile ya kupima kiwango cha oxygen kwenye hemoglobin na mingine hupima kiwango cha CO2 kwenye hemoglobini
Je, nahitaji P02 nyumbani?
Kama wewe ni mgonjwa wa Moyo, ulishapata shinikizo la moyo; pumu; TB ama tatizo linaloathiri upumuaji ni MUHIMU kwako kuwa na P02 nyumbani.