fbpx
Sale!

Kipimo cha Presha-Automatic BP Machine

5/5

Kipimo cha presha kitaboresha maisha yako kwa kukusaidia kudhibiti presha na kuepuka madhara yake. Presha na madhara yake vinaongoza kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu.

Unaweza kuepuka madhara haya kwa kufahamu hali yako ya presha na kudhibiti kama ipo juu. Ubaya ni kwamba presha inaweza kuwa juu sana bila kuonesha dalili hata moja. Kuna namna moja tuu ya kuweza kufahamu presha yako. Kupima tu!

Tafiti zinaonesha wenye kipimo cha presha na wanaoitumia wakiwa nyumbani, wanaepuka presha na madhara yake (kiharushi, ugonjwa wa moyo, figo nk.) ukilinganisha na wasiyokuwa nayo. 

Kwanza tufahamu faida za kuwa na kipimo cha presha:

1. Amani moyoni – sasa unafahamu presha yako kwa uhakika! Hutakuwa tena unahisi! Si ukisikia kichefuchefu au mapigo ya moyo yanakwenda kasi au kichwa kuuma unaanza kuhisi presha imepanda. Hapana, sasa hali yeyote ikitokea unaweza kupima presha yako na kufahamu ikoje. Hivyo kukupa faida ingine, kupata huduma ya tatizo husika.

2. Kipimo cha presha kitakufahamisha kama tiba unayoendelea nayo inafanya kazi. Sasa unaweza kufuatilia matibabu yako na kufahamu kama yanafanya kazi ama la. Unapopima na kukuta presha yako iko kwenye kiwango kinachotakiwa chukua hatua stahiki mapema – hutokuwa na hofu kuhusu presha yako – utaweza kuifuatilia mwenyewe ukiwa nyumbani. Kumbe huwenda muda hupimi presha yako unakosa fursa adhim ya kutambua na kudhibiti madhara ambayo yangegundulika kwa wakati?

3. Kudhibiti presha yako – huwa unapimwa presha ukienda hospitali kuhudhuria kliniki yako. Unafikiri ni kwanini? Hii ni kufuatilia hali ya presha yako. Sasa, swali la kujiuliza, kipimo kimoja kinatosha? Jawabu ni hapana. Kwanini sasa usubiri mpaka mwezi huku ukiwa hujui kama presha yako imepanda? Maana ingine ni kwamba madhara yanayotokea leo kwasababu presha yako iko juu yataendelea kutokea mpaka mwezi upite ndiyo yafahamike na presha kuanza kudhibitiwa.

4. Kudhibiti madhara ya presha. Kufahamu kiwango chako cha presha leo inakusaidiaje? Kufahamu presha yako leo inakusaidia kuchukua hatua stahiki mapema. Hatua hizi zinatofautiana kulingana na majibu ya kipimo. Inaweza kukuhamasisha kurudi hospitali kama presha yako iko juu ingali unaendelea na tiba-hapa utaepuka madhara ya presha kuwa juu. Hatua nyengine ya kuchukuwa, ukikuta presha yako iko chini, inaweza kuwa kumchinjia kuku mhudumu wako wa afya anayekutibu (ingawa si lazima) – hapa utakuwa unampongeza na wewe utabaki na furaha.

5. Unaweza kurekodi vipimo vingi, kuweka kumbukumbu, na kufahamu wastani wa presha yako ya damu. Kumbuka shinikizo la damu hubadilika badilika. Yani ukipima kiwango cha presha saa 06:10 kitakuwa tofauti na ukipima tena presha yako saa 06:12. Sasa unahitaji wastani wa presha yako ya damu. Huna haja ya kufanya mahesabu tena bali sasa kipimo hiki kinakupa wastani wa presha yako ya damu.

Tatizo tunalo kusaidia kutatua: Tafiti zinaonesha kwamba presha ya damu huanza kupanda kwa wenye miaka 30 na zaidi. Hivyo, ni muhimu kuwa na kipimo cha kupima shinikizo la damu kuweza kuchukua hatua stahiki kwa wakati kujikinga na madhara ya presha.

Matumizi: Hii ni mashine ambayo utaitumia kupima presha ukiwa nyumbani. Ukinunua kutoka kwetu tutakupa maelekezo ya namna bora utaweza kuitumia hii mashine kuweza kupata matokeo ya kiafya unayoyatarajia

Original price was: Sh 149,000.0.Current price is: Sh 119,000.0.

Availability: In stock

SKU HES-P-D-BPA-12 Categories , , Tag

Fahamu Faida Kipimo Hiki Cha Presha

1- Urahisi wa kufahamu presha yaka: Kipimo hiki cha presha kina kiashiria cha Shirika la Afya Duniani kitakachokuonesha kama una presha. 

2 – Inarekodi majibu kwa muda mrefu: Sasa unaweza kutambua wakati gani presha yako hukaa sawa na wakati gani hupanda. Hii itakusaidia kubaini ni kitu gani huwenda husababisha presha yako kupanda.

3 – Taa maalumu ya kuashiria kiwango kizuri na kibaya cha presha: Kipimo hiki cha presha hii huwaka taa ya rangi ya nyekundu kama shinikizo lako la damu liko juu-presha,  na huwaka taa ya rangi ya kijani kama shinikizo la damu yako liko katika kiwango kizuri.

Pia itakufahamisha kama uko katika hatari ya kupata presha kwa kuwaka taa ya rangi ya chungwa! 

4 – Inatumia umeme: mbali na kukusaidia kuepuka gharama za battery hukupa majibu sahihi ya presha.

5 – Inarekodi majibu ya watu wawili tofauti: Inakuwezesha kufahamu majibu halisi ya presha yako na ya mwenza wako bila kuchanganya

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kipimo cha Presha-Automatic BP Machine”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Okoa -20% leo!. Ungependa kuuliza kuhusu bidhaa hii?