Kipimo cha presha kitaboresha maisha yako kwa kukusaidia kudhibiti presha na kuepuka madhara yake. Presha na madhara yake vinaongoza kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu.
Unaweza kuepuka madhara haya kwa kufahamu hali yako ya presha na kudhibiti kama ipo juu. Ubaya ni kwamba presha inaweza kuwa juu sana bila kuonesha dalili hata moja. Kuna namna moja tuu ya kuweza kufahamu presha yako. Kupima tu!
Tafiti zinaonesha wenye kipimo cha presha na wanaoitumia wakiwa nyumbani, wanaepuka presha na madhara yake (kiharushi, ugonjwa wa moyo, figo nk.) ukilinganisha na wasiyokuwa nayo.
Kwanza tufahamu faida za kuwa na kipimo cha presha:
1. Amani moyoni – sasa unafahamu presha yako kwa uhakika! Hutakuwa tena unahisi! Si ukisikia kichefuchefu au mapigo ya moyo yanakwenda kasi au kichwa kuuma unaanza kuhisi presha imepanda. Hapana, sasa hali yeyote ikitokea unaweza kupima presha yako na kufahamu ikoje. Hivyo kukupa faida ingine, kupata huduma ya tatizo husika.
2. Kipimo cha presha kitakufahamisha kama tiba unayoendelea nayo inafanya kazi. Sasa unaweza kufuatilia matibabu yako na kufahamu kama yanafanya kazi ama la. Unapopima na kukuta presha yako iko kwenye kiwango kinachotakiwa chukua hatua stahiki mapema – hutokuwa na hofu kuhusu presha yako – utaweza kuifuatilia mwenyewe ukiwa nyumbani. Kumbe huwenda muda hupimi presha yako unakosa fursa adhim ya kutambua na kudhibiti madhara ambayo yangegundulika kwa wakati?
3. Kudhibiti presha yako – huwa unapimwa presha ukienda hospitali kuhudhuria kliniki yako. Unafikiri ni kwanini? Hii ni kufuatilia hali ya presha yako. Sasa, swali la kujiuliza, kipimo kimoja kinatosha? Jawabu ni hapana. Kwanini sasa usubiri mpaka mwezi huku ukiwa hujui kama presha yako imepanda? Maana ingine ni kwamba madhara yanayotokea leo kwasababu presha yako iko juu yataendelea kutokea mpaka mwezi upite ndiyo yafahamike na presha kuanza kudhibitiwa.
4. Kudhibiti madhara ya presha. Kufahamu kiwango chako cha presha leo inakusaidiaje? Kufahamu presha yako leo inakusaidia kuchukua hatua stahiki mapema. Hatua hizi zinatofautiana kulingana na majibu ya kipimo. Inaweza kukuhamasisha kurudi hospitali kama presha yako iko juu ingali unaendelea na tiba-hapa utaepuka madhara ya presha kuwa juu. Hatua nyengine ya kuchukuwa, ukikuta presha yako iko chini, inaweza kuwa kumchinjia kuku mhudumu wako wa afya anayekutibu (ingawa si lazima) – hapa utakuwa unampongeza na wewe utabaki na furaha.
5. Unaweza kurekodi vipimo vingi, kuweka kumbukumbu, na kufahamu wastani wa presha yako ya damu. Kumbuka shinikizo la damu hubadilika badilika. Yani ukipima kiwango cha presha saa 06:10 kitakuwa tofauti na ukipima tena presha yako saa 06:12. Sasa unahitaji wastani wa presha yako ya damu. Huna haja ya kufanya mahesabu tena bali sasa kipimo hiki kinakupa wastani wa presha yako ya damu.
Tatizo tunalo kusaidia kutatua: Tafiti zinaonesha kwamba presha ya damu huanza kupanda kwa wenye miaka 30 na zaidi. Hivyo, ni muhimu kuwa na kipimo cha kupima shinikizo la damu kuweza kuchukua hatua stahiki kwa wakati kujikinga na madhara ya presha.
Matumizi: Hii ni mashine ambayo utaitumia kupima presha ukiwa nyumbani. Ukinunua kutoka kwetu tutakupa maelekezo ya namna bora utaweza kuitumia hii mashine kuweza kupata matokeo ya kiafya unayoyatarajia
Reviews
There are no reviews yet.