Pata Nafuu haraka kutokana na magonjwa yanayokusababishia shida ya kupumua kwa mfano asthma/pumu uwapo na nebulizer. Nebulizer ni kifaa mashine ndogo ambayo itakusababisha uheme kama ulivyokuwa unahema mwanzo kabla ya shambulio la asthma kwa mfano. Kifaa hichi huleta nafuu ya haraka kwasababu hupeleka dawa moja kwa moja kwenye mapafu kwa haraka katika hali ya mvuke. Hivyo hukuepusha na madhara yatokanayo na kukosa hewa safi ikiwamo kifo.
Nebulizer inavyofanya kazi. Nebulizer hubadilisha dawa ya iliyo katika hali ya maji maji kuwa mvuke. Dawa huingia kwenye mapafu yako wakati unavuta pumzi polepole, kwa dakika 10 hadi 15.
Nafuu ya haraka na kwa wepesi ni faida muhimu 2 za nebulizer: Kama wewe ni mgonjwa wa pumu huwenda unatumia au unafahamu inhaler. Uzuri wa inhaler nayo ni kupeleka dawa moja kwa moja kwenye mapafu. Lakini utakubaliana na mimi kwamba unahitaji kutumia nguvu kuvuta hewa ndani unapotumia inhaler. Hii huwa changamoto kama umekamatwa na asthma/pumu kali sana au matatizo/magonjwa ya mapafu makali. Wakati huu utahitaji nebulizer kwakuwa huitaji kutumia nguvu nyingi kupumua.
Nitajuaje kama nahitaji Nebulizer?: Wewe na daktari wako mnaweza kuamua ikiwa nebulizer ndiyo njia bora ya kupata dawa unayohitaji. Chaguo la kifaa linaweza kutegemea ikiwa unapata nebulizer rahisi kutumia na ni aina gani ya dawa unayotumia.
Reviews
There are no reviews yet.