Ukubwa wa tatizo la Magonjwa ya Moyo
Ni moja ya magonjwa machache ambayo yanendelea kuwa na hatua mbaya kadiri siku zinavyokwenda.
Kisukari kinakuweka kwenye hatari ya uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kuliko. Kadiri muda wa kuwa na kisukari unavyozidi, ndivyo uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo unavyoongezeka.
Ugonjwa wa kisukari husababisha vifo vya ghafla kwa kusababisha magonjwa ya moyo. Jifunze jinsi ya kulinda moyo wako kwa mabadiliko rahisi ya mtindo wa maisha ambayo pia hukusaidia kudhibiti ugonjwa wa kisukari.
Habari njema ni kwamba unaweza kupunguza hatari uliyonayo ya kupata ugonjwa wa moyo na kuboresha afya ya moyo wako kwa kubadilisha tabia fulani za maisha. Mabadiliko hayo yatakusaidia kudhibiti kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza pia.
Magonjwa ya Moyo Ni Nini?
Kana majina mawili yatumikayo kuzungumzia magonjwa ya moyo: ugonjwa wa moyo na magonjwa ya moyo na misipa ya damu. Ugonjwa wa moyo ni aina mbalimbali za shida zinazoathiri moyo wako.
Ugonjwa wa moyo na mishipa inajumuisha aina zote za ugonjwa wa moyo, kiharusi, na ugonjwa wa mishipa ya damu.
Aina maarufu ni ugonjwa wa mishipa ya damu ya moyo, ambayo huathiri mtiririko wa damu kwenye moyo.
Namna Kisukari Kinavyoathiri Moyo Wako
Kadiri muda unavyokwenda kisukari kinaweza kuharibu mishipa yako ya damu na mishipa ya fahamu kwenye moyo.
Kisukari husababisha mkusanyiko wa “utando wa lehemu”wa lehemu ndani ya mishipa ya damu ya kwenye moyo ambayo huusika na usambazaji wa damu na hewa safi ya oksijeni kwenye moyo.
Utando wa lehemu husababisha mishipa kuwa myembamba na kupunguza mtiririko wa damu na ugumu wa mishipa – hali inayoitwa atherosclerosis.
Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye moyo kunaweza kusababisha mshtuko wa moyo.
Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye ubongo kunaweza kusababisha kiharusi.
Ugumu wa mishipa (atherosclerosis) unaweza kutokea katika sehemu zingine za mwili pia. Katika miguu na nyayo.
Ugumu wa mishipa ya damu kwenye miguu na nyayo mara nyingi ni ishara ya kwanza kwamba mtu mwenye kisukari ana ugonjwa wa moyo na mishipa.
Madhara yote haya yanaweza kugundulika na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo kama utagundua kwa wakati sahihi na kuchukua hatua stahiki.
Hatahivyo, cha kuzingatia ni kwamba madhara yote haya yanayotokea kwenye moyo yanaweza yasiwe na dalili yeyote mpaka pale ambapo madhara yamekuwa makubwa na kuelekea kwenye moyo kufeli.
Magonjwa mengine ambayo huongeza hatari ya mgonjwa wa kisukari kupata ugonjwa wa moyo ni:
- Shinikizo la juu la damu huweza kuathiri mishipa ya damu. Kuwa na shinikizo la damu na kisukari kunaweza kuongeza hatari yako ya ugonjwa wa moyo. Inakadiriwa angalau 10-23% ya wenye kisukari wana shinikizo la juu la damu pia.
- Kiwango kikubwa cha lehemu (LDL Cholesterol) “nyepesi” (“mbaya”) katika mfumo wako wa damu inaweza kutengeneza utando wa kuta za mishipa iliyoharibika na hivyo kuongeza hatari ya ugonjwa wa moyo. Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu lehemu niandikie msg nikutumie link uisome.
- Kiwango kidogo cha lehemu nzito (HDL cholesterol) inadhaniwa kuchangia ugumu wa mishipa.
- Kiwango kikubwa cha Triglycerides (aina ya mafuta katika damu yako) inadhaniwa kuchangia ugumu wa mishipa.
Hakuna hali yoyote kati ya hizi ina dalili. Daktari wako anaweza kupima shinikizo la damu yako na kufanya uchunguzi wa damu kubaini kama viwango vyako vya LDL, HDL, na triglyceride viko juu.
Sababu hizi pia zinaweza kuongeza hatari yako ya ugonjwa wa moyo
- Kuvuta sigara
- Kuwa na uzito kupita kiasi au kuwa na unene kupita kiasi
- Kutokufanya shughuli za mwili kwa kiwango cha kutosha.
- Kula chakula chenye mafuta mengi haswa ya wanyama, lehemu, na chumvi nyingi
- Kunywa pombe kupita kiasi. Unafahamu kiwango cha pombe salama kwa afya yako?
Ugonjwa wa moyo kufeli
Wagonjwa wa kisukari pia wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa moyo kushidwa kufanya kazi- moyo ku-feli. Moyo kushidwa kufanya kazi haimaanishi moyo umeacha kupiga; ina maana moyo wako hauwezi kusukuma damu kutimiza mahitaji ya mwili kulingana na uhitaji.
Hii inaweza kusababisha uvimbe kwenye miguu yako na maji kuongezeka kwenye mapafu yako, na kufanya iwe vigumu kupumua.
Moyo huendelea kushidwa kufanya kazi kadiri siku zinavyokwenda na kuwa mbaya zaidi, lakini utambuzi wa mapema na matibabu hsaidia kupunguza madhara na kuzuia au kuchelewesha hali kuwa mbaya zaidi.
Uchunguzi wa Ugonjwa wa Moyo
Vipimo vya shinikizo la damu yako, viwango vya lehemu, na uzito vitakufahamisha daktari wako na wewe pia kuhusu hatari yako ya kupata ugonjwa wa moyo. Daktari wako anaweza pia kupendekeza vipimo vingine ili kuangalia afya ya moyo wako, ambavyo vinaweza kujumuisha:
- Electrocardiogram (ECG au EKG) kupima shughuli za umeme za moyo wako.
- Echocardiogram (echo) kuchunguza mabadilko katika misuli ya moyo wako, valvu najinsi moyo wako unavyosukuma vizuri.
- Kipimo kuchunguza moyo unavyohimili mazoezi mazito ya mwili
Namna ya Kujikinga na Ugonjwa wa Moyo
Dhibiti Msongo wa mawazo unaweza kuongeza shinikizo la damu na pia unaweza kusababisha tabia zisizofaa, kama vile kunywa pombe kupita kiasi au kula kupita kiasi.
Badala yake, tembelea mshauri wa afya ya akili, jaribu kutafakari, fanya mazoezi ya mwili, au pata usaidizi kutoka kwa marafiki na familia.
Daktari wako pia anaweza kuagiza dawa ambazo zinaweza kusaidia kuweka sukari yako ya damu, shinikizo la damu, lehemu, na triglycerides karibu na viwango unavyolenga.
- Dhibiti sukari kwenye damu yako kadri uwezavyo. Unafahamu namna ya kutathmini tiba yako.
- Fanya kipimo cha HBA1C angalau mara mbili kwa mwaka, mara nyingi zaidi ikiwa dawa yako itabadilika au ikiwa una hali zingine za kiafya. Shauriana na daktari wako kuhusu mara ngapi ni sawa kwako. (Fahamu vipimo muhimu kwa mgonjwa wa kisukari)
- Hakikisha unafahamu kiwango chako cha presha ya damu. Angalau shinikizo la damu yako liwe chini ya 140/90 mm/Hg (au lengo ambalo daktari wako anaweka).
- Weka uwiano wako wa uzito na kimo katika wastani unaoshauriwa kiafya. Kupunguza uzito – kwa watu wanene na wanene kupitiliza- angalau kwa asilimia 5 ya uzito wao hupunguza hatari ya madhara ya kisukari kwenye moyo
- Fahamu na dhibiti kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu. Fahamu zaidi kuhusu lehemu-bonyeza HAPA
- Epuka kiwango kikubwa cha chumvi- hasa ile ya kuongeza mezani.
- Kula matunda na mboga zaidi.
- Fanya shughuli zinazotumia nguvu ya mwili kama vile mazoezi. Tafiti zinaonesha angalau ufanye mazoezi kwa dakika 150 kwa wiki. Ikiwa kila siku ni bora zaidi – angalau dakika 25 kila siku.
- Fuata maelekezo ya matumizi ya dawa zako.
Kwa uzoefu wangu, mtu anapogundulika na kisukari hupata huzuni ghafla na kuanza kufikiria athari ambazo amekwisha kuziona zikiwatokea watu anao wafahamu.
Kumbe badala ya kuhuzunika, alitakiwa afurahi. Afurahi kwamba amegundua kuwa ana kisukari mapema. Na sasa anaanza kuchukua hatua stahiki mapema.
Kufahamu hali yako ya kisukari mapema ndiyo siri. Ukishafahamu utaweza kuchukua hatua stahiki kwa wakati kudhibiti kisukari na kuepuka madhara yake.
AFYATech tunakusaidiaje? AFYATech tumekuwa tukitoa elimu kuhusu kudhibiti kisukari na presha kwa zaidi ya miaka 4 sasa kupitia maandiko na grupu za WhatsApp.
Leo tutakusaidi kuweza kufahamu hali yako kwa uhakika na kukusaidia kudhibiti kisukari na kulinda moyo wako.
Nimeandaa video kuhusu umuhimu wa kuwa na vifaatiba hivi. Kuwa navyo nyumbani. Nimeelezea faida ya kuwa na vifaa hivi nyumbani.
Ingawa sasa umeshakuwa mtaalamu wa kisukari na namna ya kulinda moyo wako, ni muhimu kuangalia video hii itakayokufahamisha kwa kina kuhusu kuishi kwa furaha na amani huku ukiwa na kisukari.
Pia itakufahamisha umuhimu wa kuwa na vifaa na faida lukuki za kuwa na vifaa muhimu kudhibiti kisukari na presha.
Ukifanikiwa, nitakupatia vifaa hivi kwa bei ya offer. Tafadhali bonyeza kitufe hapo chini kilichoandikwa FAHAMU SASA
LINDA MOYO WAKO: DHIBITI KISUKARI
Tafadhali Bonyeza batani FAHAMU SASA kutazama video na kupata offer yako