Ni hatari na inasikitisha! Ugonjwa wa presha unasababisha vifo na ulemavu wa kudumu duniani kote. Kwa Tanzania, inakadiriwa kwamba watu 3 kati ya watu 10 wenye umri wa miaka 30 na zaidi wana presha. 

Presha (Shinikizo la damu la juu) isiyoshushwa na kudhbitiwa ndiyo husababisha madhara. Unajua ni asilimia ngapi ya wagonjwa wa presha wameweza kushusha presha zao na kudhibiti?

Kama hufahamu takwimu hizi, tafiti zinaonesha ni angalau wagonjwa 30 kati ya 100 wanaotibiwa wameweza kushusha presha zao. 

Narudia, ni angalau wagonjwa 30 kati ya 100 wanaotibiwa ugonjwa wa presha wameweza kushusha presha zao za damu. 

Ungependa kufahamu jambo moja muhimu kulifanya ili uweze kudhibiti presha na kuepuka madhara yake? Karibu sana! Kama umefika hapa wewe ni mtu makini.

Kufahamu jambo hili ni muhimu kwani jambo hili ndio msingi ambalo ukilikamilisha njia zingine zote zinafuata na usipolifanya huwezi kupiga hatua moja ya kudhibiti kisukari na madhara yake.

Kabla ya kuliongelea, ni muhimu kuweka msingi juu ya mambo manne (4) muhimu. Mambo haya yote yamethibitishwa na tafiti nyingi zilizofanywa nje na ndani ya nchi.

1-Ugonjwa wa Shinikizo la Damu ni Hatari!

 

Ugonjwa wa shinikizo la damu ni moja ya sababu kubwa za vifo duniani.

Kwa bahati mbaya, watu wengi hawana dalili zozote za ugonjwa huu mpaka pale wanapopatwa na madhara makubwa kama kiharusi au mshtuko wa moyo.

Kwa hiyo, ni muhimu sana kupima shinikizo la damu mara kwa mara ili kugundua ugonjwa huu mapema na kupata matibabu.

Ugonjwa wa presha una athiri viungo muhimu vya mwili; ubongo na kuleta kiharusi;

2-Kinga ni Bora Kuliko Tiba ya Madhara!

 

Kwa bahati mbaya, watu wengi hawapimi shinikizo la damu mara kwa mara na wanapogundulika na ugonjwa huu, huwa tayari na madhara ya ugonjwa huu.

Kuchelewa kunafanya matibabu kuwa magumu zaidi na gharama kubwa.

Hata hivyo, kwa kuwa na kipimo cha presha nyumbani, unaweza kupima shinikizo la damu mara kwa mara na kugundua ugonjwa huu mapema.

Hivyo, kwa kupima unaweza kupata matibabu ya mapema na kuepuka madhara makubwa na gharama kubwa.

3-Kushusha presha inawezekana!

 

Watu wengi hupata ugonjwa wa presha kutokana na mwenendo wa maisha mbaya kwa afya. Hatari ingine ya kupata presha ni kuwa na umri zaidi ya miaka 30.

Kwa hiyo, kubadilisha mtindo wa maisha na kufuata mlo sahihi na mazoezi ya mara kwa mara, kunaweza kusaidia kudhibiti shinikizo la damu.

Hatahivyo ili kuweza kujua mabadiliko ya tabia hubadilishaje presha yako inabidi uweze kuifuatilia. Cha kufuatilia hapa ni tabia na shinikizo la damu.  

 Sasa, ushaanza kuhisi siri hii ni ipi. Kama bado, endelea sasa hivi unafahamu.

4. Ugonjwa wa presha hauna dalili!

Unapoona dalili za ugonjwa presha , maana yake presha ilipanda bila kudhibitiwa kwa muda mrefu.

Ndiyo maana wagonjwa wengine wanaogundulika na presha kwa mara ya kwanza huwa tayari na madhara ya ugonjwa huu.

Ndiyo maana presha huitwa muuaji wa kimya kimyaa

Yani presha, licha ya madhara yake makubwa huweza kuwepo kwa muda mrefu bila kuonesha dalili hata moja!

Bila Shaka sasa utakuwa ushafahamu hili Jambo Moja Muhimu.

Kama bado, ngoja nikufahamishe. 

Fahamu Presha Yako, Linda Afya Yako!

Kupima tu kutakuwezesha kufahamu presha yako, kuchukua hatua stahiki mapema ili kuidhibiti kama iko juu. Narudia tena, kupima tuu!

Kumbuka kuwa afya na uhai wako ni muhimu zaidi ya chochote. Uhai wako ni muhimu kwa familia yako, ndugu, jamaa na marafiki. 

Wagonjwa wengi, hata wahudumu wa afya, hutafuta huduma za afya wanapoona dalili mfano maumivu, au wasipoweza kufanya shughuli zao za kila siku. 

Ingawa si tabia nzuri kwa magonjwa mengine unaweza kunusurika ila kwa presha ni hatari!

Sasa unafahamu ULAZIMA wa kufuatilia presha yako kama una miaka 30 au zaidi.

Kama unakubaliana na mimi kwamba  kipimo cha presha ni MUHIMU SANA kama si LAZIMA kuwa nacho nyumbani ili kudhibiti presha na kuepuka madhara yake, AFYATech tutakuwezesha leo kuwa mstari wa mbele kuboresha presha afya yako.

Tunakupatia kipimo cha presha ambacho ukiwa nacho unafahamu presha yako ukiwa nyumbani, huna hofu kuhusu presha, na unaweza kutathmini kila ambacho unakifanya ili kushusha presha mfano tiba, mazoezi au vyakula.!

Kumbuka kwamba kuzuia ni bora kuliko kutibu, na kupima shinikizo la damu mara kwa mara ni NJIA BORA ya kufahamu, kudhibiti na kuepuka madhara yake.

Fahamu Presha Yako!

Fahamu kiwango cha presha yako ya damu na chukua hatua stahiki mapema unapotumia kipimo cha chenye teknolojia ya hali ya juu.

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Kushusha Presha Inawezekana: Fahamu Siri 1?
Mimi ni Dr. Adinan