Lehemu (Cholesterole): Ni nini na nawezaje Kuipunguza?
Bila shaka umeisikia kuhusu lehemu. Lehemumu ni nini?
Lehemu, (kwa kimombo cholesterole), ni aina ya mafuta yanayoujenga mwili wa mwanadamu.
Ingawa ni maarufu kwa ubaya tuu, ukweli ni kwamba lehemu inahitajika mwilini. Ni vizuri ifahamike pia kwamba kuna lehemu nzuri na mbaya.
Lehemu huitajika mwilini kwa kiwango maalum. Kiwango kikizidi lehemu ni hatari kiafya.
Lehemu hutokea wapi?
Kuna vyanzo viwili vya lehemu:
- Chanzo cha kwanza ni vyakula.
- Chanzo cha pili ni kutengenezwa kutoka kwenye ini – Kiwango kikubwa.
Lehemu huwa na mzunguko. Kutoka kwenye ini kuingia kwenye mishipa ya damu –> kupelekwa sehemu inapohitajika kwenye mwilini –> kurudishwa kwenye ini tena na kuhifadhiwa mpaka mahitaji yatokee.
Lehemu ikizidi hubaki kwenye damu kwani si lehemu yote inaweza kuondolewa kutoka kwenye damu.
Lehemu haitakiwi kuzagaa bila kazi. Ikizagaa bila kazi huanza kuganda haswa kwenye mishipa ya damu.
Shinikizo la juu la damu (presha) ni moja ya madhara makubwa yanayosababishwa na lehemu kuganda kwenye mishipa ya damu.
Lehemu inasababishaje kiharusi?
Lehemu inapoganda husababisha mishipa kukakamaa au kuziba au vyote kwa pamoja.
Inapokakamaa shinikizo la damu huongezeka, hivyo kusababisha presha.
Lehemu inapoziba husababisha damu kutokufika sehemu husika hivyo kuleta madhara kulingana na sehemu mshipa ulioathirika upo.
Kwa mfano mshipa wa kwenye ubongo ukiziba mtu hupata kiharusi. Kama mshipa unaohudumia misuli ya moyo ukiziba, mtu hupata shambulio la moyo.
Nawezaje kudhibiti kiwango cha lehemu?
Unaweza kudhibiti kiwango cha lehemu kwa kutumia njia tatu:
1- Kupunguza chakula chenye lehemu au vyanzo vya lehemu;
2- Kupunguza kiwango cha lehemu kinachofyonzwa kutoka kwenye utumbo na kuingia kwenye mfumo wa damu ikiwa umeshazila;
3-kuziondoa kwenye mfumo wa damu kama zimepenya.
Nimefafanua njia hizi kwa upana zaidi hapa chini. Tafadhali endelea kusoma
1. Vyakula vya kupunguza Lehemu – cholesterol
Vyakula vyenye kambakamba zinazoyeyuka zinapunguza uwezekano wa lehemu kunyonywa kutoka kwenye utumbo na kuingia kwenye mfumo wa damu ikiwa umeshazila.
Vyakula hivi ni
- Ndizi,
- Maharage,
- Tufaa (apple),
- Karanga
- bamia na
- Biringanya
- Zabibu
- Machungwa machachu.
- Samaki haswa wenye mafuta mengi,
- Mafuta ya mimea kama vile ya alizeti huondoa lehemu kwenye mfumo wa damu kama zimepenya kutoka tumboni.
2. Fanya mazoezi
Kutembea kwa haraka angalau kwa dakika 25 kwa siku tatu ndani ya wiki hupunguza lehemu mbaya.
3. Punguza Pombe
Kwasasa majadiliano ni makubwa juu ya kiwango kipi cha pombe ni salama kwa afya.
Ingawa ushauri kwa sasa ni kwamba angalau mwanaume anywe bia 2 kwa siku na mwanamke bia 1 kwa siku.
4. Usitumie tumbaku
Tumbaku hupunguza kiwango cha HDL (lehemu nzuri) na hivyo kuongeza kiwango cha LDL (lehemu mbaya)
Hivyo kuacha kuvuta sigara kunaboresha kiwango chako cha cholesterol cha HDL
Faida hutokea haraka:
Faida ya kuacha sigara
- Ndani ya dakika 20 baada ya kuacha, shinikizo la damu na mapigo ya moyo hurejea kwenye kiwango punde kabla ya kuvuta sigara.
- Ndani ya miezi mitatu baada ya kuacha, mzunguko wako wa damu na utendaji wa mapafu huanza kuboreka
- Ndani ya mwaka mmoja baada ya kuacha, hatari yako ya kupata ugonjwa wa moyo hupungua kwa wastani wa 50%.
6. Kuwa na uwiano mzuri wa Uzito na Urefu
Unene wa kupitiliza husababisha kiwango cha lehemu. Hakikisha una uwiano mzuri kiafya
7. Dawa zinazopunguza kiwango cha lehemu
kulingana na kiwango cha lehemu kilichopo mwilini daktari wako atakushauri aina ya dawa na dozi ya kutumia ili kuweza kuipunguza
SAIDIA WENGINE
- Tutafurahi kusikia maswali au maoni yako kuhusu makala haya. Tafadhali tuandikie hapo chini.
- Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.