Kuna wakati hutokea unatakiwa kuamua kuhusu jambo fulani. Nafahamu mpaka sasa ushaamua vitu vingi.

Inawezekana unataka kuamua kuhusu jambo fulani kuhusu maisha yako. Inawezekana kuwa matibabu, aina ya biashara ya kufanya au …

Swali linakuja kwamba, huwa unafuata njia gani ili uweze kuamua? Kumbuka kuamua ni mchakato, si lengo. Yani kama umeamua kutumia tiba hiii lengo lako ni kupona au kupunguza maumivu. Kama ni kuamua kuhusu biashara, lengo lako ni kutengeneza uchumi wako imara. Si kuamua ili mradi.

Leo, naomba nikupe dondoo moja muhimu. Ingawa unahiari ya kuamua mambo yako, ukweli ni kwamba huna uwezo wa kuamua kila kitu ili KUFIKIA LENGO lako, KUBORESHA!

Huwenda unashindwa kuamua kwasababu ya maarifa ulonayo, au uzoefu kuhusu suala husika.

Ingawa una changamoto tajwa hapo juu, maamuzi ni lazima yafanyike. Ikitokea wakati wowote unataka kufanya maamuzi lakini umejifanyia tathmini ukaridhika kwamba huwezi kufanya maamuzi sahihi yenye tija…fanya hivi:

Uliza wanaojua ikiwa hujui.

Kwahiyo ni muhimu, haswa linapokuja mambo muhimu kama afya yako kuhakikisha una uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa/ tiba/ kifaa fulani kabla ya kufanya maamuzi yeyote.

Nikutakie wakati mwema

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Namna ya Kufanya Maamuzi Sahihi Kuhusu Afya Yako?
Mimi ni Dr. Adinan