Kipimo Cha Uzito
Kipimo cha uzito ni kipimo muhimu kinachopuuzwa!
Kadiri uwiano wako wa uzito na urefu (BMI) unavyoongezeka, ndivyo hatari yako ya kupata magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari cha aina ya 2, ugonjwa wa ini, shida ya kupumua na saratani huongezeka.
Fahamu BMI yako na chukua hatua muhimu kudhibiti afya yako. Jipatie vifaa vitakavyokufahamisha BMI yako.
Ni vizuri kama umeanza kuchukua hatua kupunguza uzito. Tunakuwezesha kufuatilia uzito wako na kutathmini kama hatua unazochukua zinaleta tija.
Matumizi: Hii ni mizani ambayo utaitumia nyumbani ili kufahamu si tu uzito wako, bali tutakuwezesha kufahamu pia uwiano wako wa uzito na urefu.
Uwiano kati ya uzito na urefu ni kizio muhimu kinachotumika kupima hali ya Afya ya mwanadamu. Uzito mkubwa umekuwa ni changamoto kubwa ya Afya dunia nzima.
Faida ya kuwa na mashine ya kupima uzito:
- Sasa unaweza kufuatilia uzito wako ukiwa nyumbani na hivyo kuweza kuepuka magonjwa ya moyo, presha na kisukari.
- Mashine hizi zinatumia umeme na battery ambazo hukaa muda mrefu zaidi ukilinganisha na mizani zingine.
Vipi nitafahamu BMI Yangu? Kufahamu BMI yako unatakiwa ufahamu urefu wako katika mita, na uzito wako katika kilogram. Zidisha urefu wako kwa urefu. Kisha, gawanya uzito wako kwa urefu*2.
👉 Kwamfano, kama una kilo 75Kg na urefu wa 1.5m, BMI yako ni = 75/(1.5*1.5)=75/2.25=33.3. Au kama una kilo 70kb na urefu wa 2m: BMI= 70/(2*2)=70/4=17.5.
👍 Hatahivyo kuna vifaa ambavyo unaweza kutumia kujipima BMI yako bila kukokotoa. Zawadi ninayokupa leo ni kukupa calculator itakayokuwezesha kutambua BMI yako
Fahamu sifa ya mizani hii hapo chini
Sh 79,000.0 Original price was: Sh 79,000.0.Sh 54,900.0Current price is: Sh 54,900.0.
Availability: In stock
Ikombe –
Kipimo cha uzito na urefu
Dr. Adinan J. MD. MSc. FDHS. FFogarty (verified owner) –
Asante sana kwa Support Mr. Ikombe. Vipi unaonaje kipimo chetu cha uzito?