Hongera, siwezi kuiacha! Umechukua hatua kubwa kwa kuchagua kusomea kozi za afya, uamuzi ambao utaleta mabadiliko makubwa katika maisha yako. Kozi za afya zina thamani kubwa, zinakupa ujuzi wa kufanya mambo mengi katika maisha, na zina heshima kubwa katika jamii yetu.
Baada ya kutoa hongera, nina habari njema kwako! Habari hii itakusaidia katika safari yako ya masomo kwa kutoa msaada muhimu wa vifaatiba. Lengo letu ni kutimiza mambo matatu kwa wakati mmoja. Tunaamini umeshazoea kufanya mambo mawili.
Lengo la kwanza ni kukusaidia kuwa mtaalamu bora wa afya, lengo la pili ni kuhakikisha usipoteze pesa kununua vifaa visivyofaa, na lengo la tatu ni kukusaidia kuchagua vifaa vyako vya kujifunzia hata kama una kikwazo cha bajeti.
Ufanisi katika kozi yoyote unategemea moja kwa moja kwenye utendaji, mazoezi, na kujifunza kwa vitendo. Fani za afya zinahitaji ujuzi wa vitendo, hivyo ni muhimu kuwa tayari kufanya mazoezi ya vitendo. Zoezi!
Kwa mfano, kujifunza jinsi ya kumchunguza mgonjwa kunahitaji mazoezi mengi na kujituma, haswa nje ya masaa ya darasani. Kwa hivyo, ni muhimu kuwa na vifaa vyako vya mafunzo.
Lakini ni vifaa gani vya mafunzo unavyohitaji? Kabla ya kukuambia ni vifaa gani, nataka kusisitiza umuhimu wa ubora. Kumbuka kuwa majibu unayopata kutoka kwenye vifaa ndivyo unavyojifunza. Kwa mfano, unapopima sauti za mapafu na moyo, stethoscope yako inapaswa kurekodi sauti hizo kwa usahihi. Hivyo, ubora ni muhimu.
Jambo lingine muhimu ni aina ya vifaa unavyohitaji. Kwa mfano, ikiwa unafuata kozi ya upasuaji, unahitaji vifaa tofauti na mtu anayesomea upasuaji. Vifaa hivi vimeorodheshwa kulingana na mifumo ya mwili ambayo utaifunza.
PATA USHAURI, NOTES & VITABU
Pata ushauri muhimu kutoka Kwa Dr. Adinan. Utajumuika pia na wanafunzi wenzako ambao mtajadiliana na kubadilishan ujuzi na namna ya kuwa bora.
Aina za Vifaa Vya Mafunzo Na Matumizi Yake
Vifaa unavyohitaji ni muhimu kwa kutoa huduma kwa mteja (Mgonjwa), ambayo ni pamoja na kufanya vipimo kadhaa kwenye mifumo mbalimbali ya mwili wa binadamu.
- Kipima Presha (BP Machine), Stethoscope & Torniquet: Hizi ni vifaa muhimu kwa kumpima mgonjwa kwa kuchukua presha ya damu (BP Machine) na kusikiliza mwenendo wa moyo (Stethoscope). Torniquet hutumiwa wakati wa kuchukua sampuli za damu kwa uchunguzi.
- Kipima Mapafu na Oxygen Level (Stethoscope & Pulse Oximeter): Kupitia Stethoscope, unaweza kuchunguza hewa inayoingia mapafu ya mgonjwa, na Pulse Oximeter hutumiwa kupima kiwango cha oksijeni mwilini.
- Kipima Uimara wa Mfumo wa Fahamu (Reflex/Patella Hammer, Monofilament, Tuning Fork, Pen Torch): Vifaa hivi hutumika kufanya vipimo vya utimilifu wa mfumo wa fahamu kwa kuchunguza ikiwa mgonjwa anaweza kuhisi (Monofilament), kuona (Snellen chart), kusikia (Tuning fork), na kuitikia vichocheo (Patella hammer). Pia, Pen Torch hutumiwa kuangalia jinsi jicho linavyoitikia mwanga.
- Kipima Ujauzito na Maendeleo ya Kijusi (Gestation Wheel, Tape Measure, Fetoscope): Vifaa hivi hutumiwa kujua umri wa ujauzito na kukadiria tarehe ya kujifungua (Gestation Wheel & Tape Measure). Kwa wanafunzi wa afya, Fetoscope hutumiwa kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto.
- Kipima masikio (Otoscope): Otoscope hutumiwa kuchunguza sikio la mgonjwa na kugundua masuala ya masikio.
- Miwani ya Upasuaji (Theatre Goggles): Kwa wakati wa kufanya kazi kama mtoa huduma wa afya, barakoa za upasuaji zinahitajika kuzuia hatari ya maambukizi kutokana na majimaji au damu kurukia na kuingia machoni.
- Vifaa vya Kujikinga (Medical Coat au Apron): Kulingana na kozi yako, unaweza kuhitaji vifaa vya kujikinga kama vile medical coat (kwa mfano katika kozi za tiba) au apron (kwa mfano katika kozi za uuguzi).
- Vipima Urefu, Upana na Mzunguko (Tape Measure na MUAC Tape): Vifaa hivi hutumiwa kuchukua vipimo vya urefu, upana, na mzunguko wa sehemu mbalimbali za mwili, kwa mfano, kuangalia maendeleo ya mtoto au hali ya lishe.
- Macho (Ophthalmoscope, Tonometer): Hivi ni vifaa muhimu kwa kuchunguza macho ya mgonjwa.
- Angle za joints (Goniometer): Vifaa hivi vinaweza kutumiwa katika kuchunguza viungo vya mwili na kuchukua vipimo sahihi.
Vifaa hivi ni muhimu katika kozi za afya kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kufanya vipimo sahihi katika mifumo tofauti ya mwili wa binadamu. Kila kifaa kina jukumu lake muhimu katika kutoa huduma ya afya na kusaidia katika utambuzi sahihi.
Kila mwaka, mamia ya wanafunzi wanaojiunga na Chuo cha Afya hujikuta katika changamoto zinazohusiana na vifaa vyao vya kazi.
Wengi wao, kama wewe, hawana ufahamu wa vifaa wanavyotakiwa kuwa navyo, na hii inaweza kuwa changamoto kubwa sana.
Kama mwalimu na daktari mwenye uzoefu wa miaka 10 katika fani ya afya, nimekuwa nikishuhudia hili mara kwa mara.
Karibu 80% ya wanafunzi wanaingia chuoni hawana uelewa mzuri wa vifaa wanavyohitaji, na hii imesababisha matatizo mengi, kama vile kununua vifaa vichache kwa gharama kubwa, kuwa na vifaa visivyo na umuhimu, na vifaa visivyokuwa na ubora.
Ninakupa ushauri huu leo kama mwalimu na daktari ili kukusaidia kuepuka changamoto hizi. Ushauri wangu unategemea uzoefu wangu wa miaka mingi katika fani hii.
Ninataka kuanza kwa kukushirikisha stori fupi ya kibinafsi. Mwaka 2006 nilikuwa kama wewe.
Nimechaguliwa kujiunga kusoma kozi ya udaktari. Nilipokuwa mwanafunzi, nilitapeliwa na kuuziwa vifaa visivyokuwa na ubora na vya gharama kubwa.
Niliingia chuoni nikiwa na list ya vifaa ambavyo sikuwahi kuviona kabla. Sikujua namna ya kuhakiki ubora, kipi ni cha muhimu, na wapi napaswa kununua vifaa hivyo.
Nilikubaliana na changamoto hii kwa sababu nilihitaji vifaa hivyo kwa mafunzo yangu.
Hii inaweza kutokea kwa yeyote kati yetu. Kama nilivyokuwa wakati huo, huwenda nawe leo umepatwa na butwaa kuhusu vifaa na unahangaika kuvipata.
Lakini, sio tu kuhusu kuwa na vifaa, bali ni kuhusu kuwa na vifaa bora na vyenye thamani.
Nilipokuwa nafundisha wanafunzi wangu , walikuwa wanatapeliwa. Hawakujua namna ya kujilinda dhidi ya matapeli wanaowalenga.
Wewe pia hujasalimika na ulanguzi unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu katika biashara ya vifaa vya afya.
Kinachosikitisha ni kwamba wanafunzi hawa, kama ilivyokuwa kwangu wakati ule, wanaweza kushindwa kuwasiliana na wauzaji wa vifaa au hata kubadilisha vifaa vyao visivyokuwa na ubora.
Na mara nyingi, familia zao hazipo tayari kununua vifaa vipya kila mara vinapoharibika.
Kwa kutambua changamoto hii, mwaka 2015, nilijadiliana na wanafunzi ambao walihitaji niwe nawatafutia vifaa.
Nilisaidia kwa kadri nilivyoweza, lakini nilipoona uhitaji unaongezeka, nililazimika kuongeza huduma zangu.
Hivyo, mwaka 2016, nilisajili biashara iitwayo Health Equipment Solutions (HES).
Tangu wakati huo, nimekuwa nikisaidia wanafunzi katika fani za afya kupata vifaa bora kwa bei nafuu na vyenye warranty.
Nia yangu ni kuhakikisha kuwa unapata vifaa vyenye ubora ili ufanikiwe katika masomo yako na baadaye katika kazi yako ya kutoa huduma za afya.
Kumbuka warranty ni mpaka umalize chuo!
Lakini pia, nimejitolea kuelimisha wanafunzi kuhusu jinsi ya kuchagua vifaa kwa ujasiri na kujikinga dhidi ya utapeli popote pale watakaponunua.
Leo, nitakufahamisha kuhusu vifaa unavyohitaji kwa mafunzo yako na kukupa siri ya mambo muhimu ya kuzingatia ili upate vifaa bora.
Kwa sababu tunaamini kwamba vifaatiba bora vitakuwezesha kuwa mhudumu bora wa afya, na lengo letu ni kusaidia kuweka ufanisi na ubora katika mafunzo yako.
Kwa hiyo, nakukaribisha kutembelea duka letu la vifaa tiba bora. HES iko hapa kuhakikisha kuwa unaanza safari yako ya kiafya kwa kuwa na vifaatiba bora na vyenye thamani.
Tunakutakia mafanikio makubwa katika kazi yako ya kutoa huduma za afya, na tuko hapa kusaidia kufanikisha malengo yako. Asanteni sana.
Vifaa Kwa Mwanafunzi wa Udaktari (MD)
Utafanya kazi kama daktari ispokuwa tu ni mwanafunzi.
Si tu utashiriki kwenye majadiliano ya kitabibu ispokuwa utahudhuria na kusaidia upasuaji na kuzalisha.
Utahitaji vifaa ambavyo vitakuzuia na hatari ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na majimaji / damu kukurukia na kuingia machoni (theatre goggles).
Vifaa hivi ni: 1-BP Machine; 2-Stethoscope; 3-Thermometer; 4-Tape measure; 5-Patella/reflex hammer; 7-Pregnancy wheel/Gestation wheel; 8-Tuning fork; 9-Theatre goggles; 10-MUAC Tape; 11-Pulse Oximeter; 12-Fetoscope; 13-Monofilament; 14-Torniquet; na 15-Snellen chart
Vifaa Kwa Mwanafunzi Kozi ya CLINICAL Medicine (CO)
Kazi yako kama daktari mwanafunzi itakuwa ni kumpa huduma mteja (Mgonjwa) ikiwamo kumfanyia vipimo.
Vipimo hivi ni kama cha presha ya damu, utimilifu wa mishipa ya fahamu, joto, ukuaji wa mimba, kufahamu tarehe ya ujauzito, na hata kuzalisha wajawazito.
Hivyo, kwa mtiririko huohuo, utahitaji kipimo cha presha na kipimo cha kusikiliza mapigo ya moyo, kipimo cha kugonga kupima utimamu wa mishipa ya fahamu.
Pia unahitaji kipima joto, gestation wheel kukadiria uja uzito na ukuaji wa mimba, na vifaa vitakavyoweza kukusaidia kujikinga wakati unazalisha wajawazito.
Kwa kuongezea, unahitaji tochi na kifaa kinachosaidia katika kuchukua vipimo vya damu.
Kitaalamu vifaa hivi ni: 1-BP Machine; 2-Stethoscope; 3-Thermometer; 4-Tape measure; 5-Patella/reflex hammer; 7-Gestation wheel; 8-Tuning fork; na 9-Theatre goggles.
Vifaa Kwa Mwanafunzi Kozi ya Uuguzi (NURSING)
Kazi yako kama muuguzi itakuwa ni kumpa huduma mteja (Mgonjwa). Huduma hii hujumuisha kumfanyia vipimo mbalimbali kubaini hali ya afya ya mgonjwa.
Wateja wako watakuwa wa makundi mbalimbali kwa mfano wajawazito na watoto.
Kwa ujumla, wateja huhitaji kupima presha ya damu, joto. Kwa wajawazito, utahitaji kupima ukuaji wa mimba, kumtaarifu tarehe ya kujifungua, na kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto. Kumbuka kuzalisha pia ni huduma MUHIMU kwa wajawazito.
Hivyo, kwa mtiririko huohuo, utahitaji kipimo cha presha na kipimo cha kusikiliza mapigo ya moyo, kipima joto.
Unahitaji pia kifaa cha kukadiria uja uzito na ukuaji wa mimba, kitakachokuwezaesha kusikia mapigo ya moyo ya mtoto na vifaa vitakavyoweza kukusaidia kujikinga wakati unazalisha.
Pia utahitaji tochi na kifaa kinachosaidia katika kuchukua vipimo vya damu.
Kitaalamu vifaa hivi ni: 1-BP Machine; 2-Stethoscope; 3-Thermometer; 4-Tape measure; 5-Torniquet; 6-Gestation wheel; 7-Pinnard fetoscope; 8-MUAC na 9-Theatre goggles.
Vifaa Kwa Mwanafunzi Kozi ya Physiotherapia (Physiotherapy)
Kazi yako kama physiotherapist mwanafunzi itakuwa ni kumpa huduma mteja (Mgonjwa) ikiwamo kumfanyia vipimo kama cha presha ya damu, utimilifu wa mishipa ya fahamu, na angle za viungo.
Pia utatakiwa, wakati mwengine, kufahamu kiwango cha oxygen.
Kitaalamu vifaa hivi ni: 1-BP Machine; 2-Stethoscope; 3-Thermometer; 4-Tape measure; 5-Patella/reflex hammer; 6-Pulse oximeter na 7-Goniometer
Goniometer kifaa cha mafunzo kwa kozi ya physiotherapy. Hutumika kupima nyuzi (Angle) za viungo
Siwezi Kununua Vifaa Vyote Kwa Wakati Mmoja: Je, Nianze na Vifaa Vipi?
Hili swali ni MUHIMU kujiuliza kwa kuwa wakati mwenignie tunapata changamoto za kifedha hivyo kutokuweza kununua vifaa vyote kwa pamoja.
Majibu ya hili swali yako ya aina mbili, lakini kama swali ni je vifaa gani naweza kuanza navyo na nikafanya mafunzo kwa ufaninisi
Nitakujibu kama ifuatavyo. Kwanza inahitaji ufahamu wa ratiba ya chuo chako au kundi lako kama mmegawanywa kwenye makundi.
Kwasababu vifaa vingine huitajika zaidi katika idara fulani.
Licha kuwa navyo vyote ni muhimu zaidi, lakini ikibidi, kwa uzoefu wangu, nimekuandikia kukushauri kwa kila kozi unaweza kuanza na vifaa vipi bila kuathiri mafunzo yako.
Ukiwa na vifaa saba (7) unaweza kufanya vizuri. Vifaa hivi ni 1-BP Machine; 2-Stethoscope; 3-Thermometer; 4-Tape measure; 5-Theatre goggles; 6-Patella hammer na 7-Pen torch
Mambo 7 Ya Kuzingatia Unaponunua Vifaa Vya Mafunzo
1. Fahamu na vielewe vifaa vinavyohitajika: Ni muhumu kuhakikisha unafahamu vifaa MUHIMU vinavyohitajika kabla hujanunua.
Fahamu vinafanya nini pia, na fahamu vipi unaweza kuhakiki ubora.
Njia rahisi ni kumtafuta mtaalamu wa fani unayokwenda kusomea- kwa mfano, nenda hospitali ya jirani muulize daktari au muuguzi wa pale.
2. Uzoefu wa wauzaji…Vifaa huitaji utaalam, hasa vifaatiba.
Muuzaji kama ana ujuzi na vifaa anavyouza mteja hufaidika kwa kupata ushauri wa kitaalamu.
Kwa mfano, utaelekezwa namna ya kutumia na namna ya kurekebisha kikitokea dosari.
Pia, kama una pesa kidogo unaweza kushauriwa vifaa gani ni muhimu zaidi ili uanze navyo.
Wauzaji wana UZOEFU wa kutosha, Wanajua wanachokiuza na namna kinavyotumika? Haya ni maswali muhimu.
3. Je, Wauzaji wanaaminika? Kama ni kampuni inaaminika? Kuaminika hapa kuna namna mbili:
1-imani kwenye ubora wa bidhaa;
2-imani kwa mteja, je, kifaa kinabadilishwa pindi kikibainika kina hitilafu baada ya kununua?
4. Namudu bei? Ikumbukwe pia, fani za Afya zinahitaji vifaa vingi (zaidi ya vitano) kwa wakati mmoja.
Bila shaka vifaa hivi vitakuwa ghali. Lakini ukilinganisha wauzaji, bila kuathiri ubora, Je bei ipi unaimudu?
5. Je, wanaweza kunisafirishia kifaa nikakipata nilipo? Kwa wanafunzi, kulinda muda ni muhimu sana.
Ni muhimu kujiuliza kama unaponunua vifaa wana uwezo wa kukusafirishia mpaka ulipo?
Kumbuka, kama kitaharibika ukiwa chuoni inabidi ufanyike mpango ili uletewe kifaa hapo.
6. Uwezo wa kampuni kukuhudumia? Jiulize, kwamfano wamekuahidi wataweza kukubadilishi kifaa kikiwa kina hitilafu,
Je, wana stock kubwa ya bidhaa? Au ikitokea tatizo unasubirishwa kwa muda mrefu?
7. Nunua vifaa kwa seti: Punguza gharama kwa kununua vifaa vikiwa kwenye seti kuliko kimojakimoja.
Mara nyingi wafanya biashara huuza kwa bei rahisi kama utanunua vifaa kama seti.
Unahitaji Vifaa Vya Mafunzo Leo? - Soma Hii Kwanza
Sasa umeshakuwa mtaalamu. Nakuhakikishia unaweza kununua kifaa kutoka kwa yeyote bila wasiwasi wowote ule.
Ikiwa unahitaji vifaatiba kwa mafunzo yako, tuwasiliane tutakupatia vifaa bora vyenye warranty mpaka umalize chuo!
HES tumekuwa tukiwasaidia wanafunzi kama wewe kupata vifaatiba bora kwa ajili ya mafunzo yao kwa takribani miaka sita (6) sasa!
HES tumetofautiana na wafanyabiashara wengine kwa mambo matatu (3) muhimu sana!
1. Tunakuondolea wasiwasi wa kupoteza pesa zako – kama uko mbali na ofisi zetu, utalipia baada ya kupokea bidhaa.
2. Tunakuhakikishia ubora – HES inakubadilishia kifaa kwa haraka sana kama kina changamoto zozote! Warranty mpaka umalize chuo. Lakini la mwisho muhimu sana ni
3. USHAURI! Wanafunzi wote walionunua kwetu wanatushukuru kwa ushauri tuliowapa kabla na baada ya kununua vifaa!