Kuna Umuhimu wa Kuwa na Kipimo Cha Presha Nyumbani?
𝐉𝐞, 𝐮𝐧𝐚𝐣𝐮𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐬𝐡𝐢𝐧𝐢𝐤𝐢𝐳𝐨 𝐥𝐚 𝐣𝐮𝐮 𝐥𝐚 𝐝𝐚𝐦𝐮 (Presha)? Ndiyo, wewe! Unaweza kuwa na presha bila kuonesha dalili!
𝐏𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚 𝐧𝐢 𝐦𝐮𝐮𝐚𝐣𝐢 𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐦𝐲𝐚 𝐤𝐢𝐦𝐲𝐚. Imeitwa hivi kwasababu haina dalili kama vile magonjwa mengine!
𝐖𝐚𝐭𝐮 𝟑𝟎 𝐤𝐚𝐭𝐢 𝐲𝐚 𝟏𝟎𝟎 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐩𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚 𝐋𝐀𝐊𝐈𝐍𝐈 𝐰𝐚𝐭𝐮 𝟐𝟓 𝐡𝐚𝐰𝐚𝐟𝐚𝐡𝐚𝐦𝐮 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚 𝐮𝐠𝐨𝐧𝐣𝐰𝐚 𝐡𝐮𝐮! Ulikuwa unafahamu kwamba watu wengi hivi hawafahamu hali yao ya presha kama inavyooneshwa na tafiti? Unaweza kujiuliza kufahamu kuna umuhimu gani!
𝐖𝐚𝐭𝐮 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐨𝐠𝐮𝐧𝐝𝐮𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐩𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚 𝐡𝐮𝐰𝐚 𝐭𝐚𝐲𝐚𝐫𝐢 𝐰𝐚𝐦𝐞𝐬𝐡𝐚𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐦𝐚𝐝𝐡𝐚𝐫𝐚 𝐲𝐚 𝐮𝐠𝐨𝐧𝐣𝐰𝐚 𝐡𝐮𝐮 𝐡𝐚𝐭𝐚𝐫𝐢 𝐧𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐨𝐳𝐢𝐝𝐢. Kwasababu presha haina dalili watu wengi wamekuwa wakichelewa kutafuta tiba na hivyo kupata athari za ugonjwa huu kama kiharusi, matatizo ya moyo, kufeli figo nk. Vipi unaweza kuepuka changamoto hii?
𝐓𝐚𝐟𝐢𝐭𝐢 𝐳𝐢𝐦𝐞𝐭𝐡𝐢𝐛𝐢𝐭𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐏𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚 𝐧𝐢 𝐮𝐠𝐨𝐧𝐣𝐰𝐚 𝐮𝐧𝐚𝐨𝐭𝐢𝐛𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐮𝐤𝐢𝐭𝐚𝐦𝐛𝐮𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐚𝐩𝐞𝐦𝐚 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐮𝐤𝐮𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐮𝐚 𝐬𝐭𝐚𝐡𝐢𝐤𝐢. Lakini kuna changamoto ambayo HES tumekuja kuitatua.
𝐊𝐣𝐢𝐩𝐢𝐦𝐚 𝐭𝐮 𝐧𝐝𝐢𝐲𝐨 𝐧𝐣𝐢𝐚 𝐩𝐞𝐤𝐞𝐞 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐟𝐚𝐡𝐚𝐦𝐮 𝐡𝐚𝐥𝐢 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐲𝐚 𝐩𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚. Presha haiumi! Njia moja tu ya kuweza kutambua kama una presha: kujipima tu! Hatahivyo changamoto inakuja kwenye kudhibiti presha baada ya kujipima.
𝐓𝐮𝐦𝐞𝐤𝐮𝐣𝐚 𝐧𝐚 𝐮𝐟𝐮𝐦𝐛𝐮𝐳𝐢 𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐤𝐮𝐬𝐚𝐢𝐝𝐢𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐚𝐦𝐛𝐮𝐚 𝐡𝐚𝐥𝐢 𝐲𝐚𝐤𝐨 𝐲𝐚 𝐩𝐫𝐞𝐬𝐡𝐚 𝐦𝐚𝐩𝐞𝐦𝐚 𝐭𝐞𝐧𝐚 𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐧𝐲𝐮𝐦𝐛𝐚𝐧𝐢.
Faida za Kipimo Hiki Cha Presha ni Zipi?
1- Urahisi wa kufahamu presha yaka: Kipimo hiki cha presha kina kiashiria cha Shirika la Afya Duniani kitakachokuonesha kama una presha.
2 – Inarekodi majibu kwa muda mrefu: Sasa unaweza kutambua wakati gani presha yako hukaa sawa na wakati gani hupanda. Hii itakusaidia kubaini ni kitu gani huwenda husababisha presha yako kupanda.
3 – Taa maalumu ya kuashiria kiwango kizuri na kibaya cha presha: Kipimo hiki cha presha hii huwaka taa ya rangi ya nyekundu kama shinikizo lako la damu liko juu-presha, na huwaka taa ya rangi ya kijani kama shinikizo la damu yako liko katika kiwango kizuri.
Pia itakufahamisha kama uko katika hatari ya kupata presha kwa kuwaka taa ya rangi ya chungwa!
4 – Inatumia umeme: mbali na kukusaidia kuepuka gharama za battery hukupa majibu sahihi ya presha.
5 – Inarekodi majibu ya watu wawili tofauti: Inakuwezesha kufahamu majibu halisi ya presha yako na ya mwenza wako bila kuchanganya.