fbpx

Nafikiri hakuna haja ya kufafanua maziwa ni nini kwani kwa muda mrefu binadamu amekuwa akitumia maziwa ya ng’ombe, mbuzi, na kondoo, kama chakula au kinywaji.

Lakini je, maziwa ni salama kwa mgonjwa wa presha? Kabla ya kujibu swali hili kwanza tufahamu faida za maziwa kwa binadamu.

Faida ya Maziwa kwa Binadamu

Maziwa yana faida nyingi kwa afya ya binadamu. Maziwa yana protini inayohitajika kujenga mwili.

Pia, maziwa yana madini ya kalsiamu na fosforasi ambazo husaidia mifupa na meno kuwa imara, , na zinki inayohitajika kwa ukuaji na ukarabati wa mwili.

Pia, maziwa yana vitamini B12 huboresha mishipa ya fahamu na mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.

Maziwa yanaweza kusindikwa na hivyo kuongeza faida kulingana na bidhaa inayotokana na usindikaji.

Nitaeleza kwa kifupi baadhi ya bidhaa hizi na faida zake.

Bidhaa zitokanazo na maziwa ni pamoja na jibini, siagi, mtindi, maziwa ya unga, na juisi ya maziwa.

  • Jibini: Jibini hutengenezwa kwa kugandisha maziwa na kuondoa maji yake. Kuna aina nyingi za jibini, kama vile jibini laini, jibini ngumu, na jibini isiyokuwa na mafuta mengi.
  • Mtindi / Yoghurt: Yoghurt ni bidhaa ya maziwa inayotengenezwa kwa kuchachusha maziwa na kuongeza bakteria wanaofaa kwa afya. Yoghurt ina faida ya kuimarisha mfumo wa kinga na kuboresha utendaji wa mfumo wa utumbo.
  • Siagi ya Maziwa: Siagi ya maziwa hutengenezwa kwa mafuta ya juu (tunapenda kuita cream) kutoka kwenye maziwa yaliyosindikwa. Inaweza kutumiwa kwenye mikate na kama kiungo katika kupikia.

Bidhaa hizi zina ladha nzuri na zinaweza kuwa sehemu muhimu ya lishe yenye afya.

Hatahivyo, bidhaa za maziwa zinaweza kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta mabaya kwa afya, ambayo yanaweza kuathiri afya ya moyo na kusababisha ongezeko la cholesterol.


Athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kwa kutumia maziwa

Mbali na faida zote hizi, maziwa yanaweza kuwa na athari kwa binadamu haswa katika mfumo wa damu – moyo na mishipa ya damu ikiwa aina na kiwango cha maziwa hakitazingatiwa na mtumiaji.

Hivyo, ni muhimu kuzingatia matumizi ya bidhaa hizi kwa kiasi, hasa kwa watu wenye presha ya juu au matatizo mengine ya kiafya.

Nitumie Kiwango Kipi cha Maziwa na Bidhaa Zake kwa Siku

Kiwango kwa siku kinachopendekezwa ni kati ya mililita 250 hadi 500 (sawa na glasi 1-2) ya maziwa ya kawaida, au sawa na mililita 200 hadi 250 ya mtindi.

  • Maziwa fresh: Kati ya mililita 500 hadi 1000 (sawa na glasi 2 hadi 4).
  • Jibini: Gramu 30 hadi 60 (sawa na kipande 1 hadi 2 cha jibini).
  • Mtindi / Yoghurt: Gramu 200 hadi 400 (sawa na chombo 1 hadi 2 cha yoghurt).

Hata hivyo, watu wenye presha ya juu wanaweza kuhitaji kupunguza matumizi ya maziwa yenye mafuta mengi na badala yake kuchagua maziwa yenye mafuta kidogo au yasiyokuwa na mafuta.

Fahamu Presha Yako!

Fahamu kiwango cha presha yako ya damu na chukua hatua stahiki mapema unapotumia kipimo cha chenye teknolojia ya hali ya juu.

Namna ya kutambua maziwa yenye mafuta mengi

Kutambua maziwa yasiyo na mafuta mengi (low-fat milk) au maziwa yaliyoondolewa mafuta yote (skimmed milk) kutoka kwenye maziwa yenye mafuta mengi (full-fat milk) kunaweza kufanyika kwa njia kadhaa. Hizi hapa ni baadhi ya njia za kutambua tofauti hizo:

1. Lebo ya Bidhaa: Njia rahisi na ya moja kwa moja ni kusoma lebo ya bidhaa. Watengenezaji wa maziwa huandika aina ya maziwa kwenye pakiti, kama vile “maziwa yasiyo na mafuta” (skimmed milk), “maziwa yenye mafuta kidogo” (low-fat milk), au “maziwa yenye mafuta mengi” (full-fat milk). Mara nyingi, asilimia ya mafuta katika maziwa itaandikwa wazi.

2. Muonekano: Maziwa yenye mafuta mengi yana muonekano mzito na rangi iliyo zaidi kuelekea manjano ikilinganishwa na maziwa yasiyo na mafuta au yenye mafuta kidogo, ambayo yana muonekano mwepesi na rangi nyeupe zaidi.

3. Ladha: Maziwa yenye mafuta mengi yana ladha nzuri, ya mafuta na ya kuvutia zaidi ikilinganishwa na maziwa yasiyo na mafuta, ambayo mara nyingi yana ladha kama maji.

4. Utando wa juu: Maziwa yenye mafuta mengi yana tabia ya kuunda tabaka la mgando au cream juu yake baada ya kukaa kwa muda. Maziwa yasiyo na mafuta au yenye mafuta kidogo hayatoi utando.

Ni muhimu kuchagua aina ya maziwa inayokufaa kulingana na mahitaji yako ya kiafya na mapendeleo yako ya ladha.

Kwa mfano, watu wenye kuchunga uzito wao au wenye matatizo ya kiafya yanayohusiana na mafuta wanaweza kuchagua maziwa yasiyo na mafuta au yenye mafuta kidogo.

 

 

SAIDIA WENGINE

  • Tutafurahi kusikia maswali au maoni yako kuhusu makala haya. Tafadhali tuandikie hapo chini.
  • Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.
 
Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Muulize Dr. Adinan