Kama unafanya jitihada kuboresha afya yako kwa kupunguza uzito, ningependaa nikupe ushauri maalum ili ufanikiwe.
Kama unajipima mara kwa mara uzito, unafanya vizuri. Lakini, kuzingatia uzito peke yake haitoshi.
Ndiyo, haitoshi!. Unahitaji kuzingatia uwiano wako wa uzito na urefu (BMI kwa kimombo).
Uwaiano wa uzito na urefu (BMI) ni nini? BMI ni makadirio ya mafuta ya mwili na kipimo kizuri cha hatari uliyonayo kupata magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa kuwa na mafuta zaidi mwilini.
Kadiri BMI yako inavyoongezeka, ndivyo hatari yako ya kupata magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari cha aina ya 2, ugonjwa wa ini, shida ya kupumua na saratani huongezeka.
Madhara Ya Uwiano Mkubwa wa Uzito na Urefu?
Watu walio na unene kupita kiasi wako katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ikilinganishwa na wale walio na uwaino wa kawaida.
Matatizo unayoweza kuyapata ukiwa na uwiano mkubwa ni kama ifuatavyo:
- Vifo katika umri mdogo
- Shinikizo la juu la damu (Presha)
- Cholesterol kwenye damu
- Kisukari aina ya 2
- Ugonjwa wa moyo
- Kiharusi
- Ugonjwa wa mfuko wa nyongo
- Ugonjwa wa mifupa (Osteoarthritis)
- Kuhema kwa tabu ukiwa usingizini
- Matatizo ya akili
- Maumivu ya mwili.
Upi ni uwiano mzuri wa uzito na kimo?
Nawezaje kufahamu Uwiano wa Uzito na Urefu Wangu?
Kufahamu BMI yako unatakiwa ufahamu vitu viwili: urefu wako katika mita, na uzito wako katika kilogram.
Kisha, zidisha urefu wako mara urefu. Kisha, gawanya uzito wako kwa urefu*urefu.
Kwa mfano, kama una kilo 75Kg na urefu wa 1.5m, BMI yako ni = 75/(1.5*1.5)=75/2.25=33.3. Au kama una kilo 70kg na urefu wa 2m: BMI= 70/(2*2)=70/4=17.5.
Hatahivyo kukurahisishia kazi, tunakupatia kifaa ambacho kitakufahamisha BMI yako kwa haraka.
Nini ufanye kuboresha uwiano wa uzito na urefu?
Kwa watu ambao wanachukuliwa kuwa wanene (BMI kubwa kuliko au sawa na 30) au wale walio na uzito kupita kiasi (BMI ya 25 hadi 29.9) na wana sababu mbili au zaidi za hatari, inashauriwa kupunguza uzito.
Watu ambao ni wazito kupita kiasi, hawana kipimo kikubwa cha kiuno, na wana chini ya sababu mbili za hatari wanaweza kuhitaji kuzuia kuongezeka kwa uzito badala ya kupunguza uzito.
Offer ya Muda Mfupi!
Pata Punguzo la TSh. 58,000/=
Kipimo cha Uzito na BMI




- Fuatilia uzito wako kwa kutumia simu
- Fahamu ufanisi wa njia unazotumia kupunguza uzito
- Pata makadirio ya kiwango cha mafuta
- Kipmo kilichoboreshwa usahihi
Saizi ya kiuno chako kinaathiri vipi afya yako?
Hatari yako ya kupata baadhi ya matatizo ya kiafya huathiriwa si tu na uzito wako na uwiano wa uzito na urefu (BMI) lakini pia na eneo ambapo mafuta ya mwili yako mengi kuzidi kiasi.
Ukubwa wa saizi ya kiuno chako inamaanisha kuwa una mkusanyiko mkubwa wa mafuta katika viungo vyako vya tumbo. Mafuta haya yanakuweka katika hatari ya magonjwa sugu kama vile:
- Kisukari aina ya pili
- Magonjwa ya Moyo
- Kiharusi
- Saratani
Hatahivyo, kiwango hiki kinaweza kutofautiana kulingana na rangi au kabila(1). Watu wa jamii tofauti wana kiwango tofauti cha mafuta kwenye ogani za tumboni.
Kwa mfano tafiti zilizofanywa zimeonesha kwamba watu jamii ya Asia wana mafuta mengi kwenye ogani za tumboni ukilinganisha na wenzao wa Ulaya. Watu wa Africa wameonekana kuwa na mafuta machache katika ogani za tumboni.
Kwa afya bora, kiuno chako kinapaswa kuwa chini ya inchi 40 (101 cm) kwa wanaume, na chini ya inchi 35 (90 cm). kwa wanawake. Haya ni makadirio kulingana na tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa watu wenye chimbuko la Africa.
Je, nawezaje kupima saizi ya kiuno changu kwa usahihi?

Napimaje Saizi ya Kiuno Changu Kwa Usahihi?
Ingawa kupima kiuno chako ni rahisi, hapa nakushauri hatua ambazo zitahakikisha kuwa unapata kipimo sahihi zaidi kila wakati:
- Ondoa nguo ambazo zinazuia kiuno chako.
- Simama wima.
- Tafuta sehemu ya chini ya mbavu ya mwisho na sehemu ya juu ya nyonga yako.
- Chagua sehemu nyembamba zaidi kati ya pointi hizi
- Zungusha tepu Sehemu nyembamba zaidi ni laini
- Hakikisha tepu imenyooka na haujasokota (angalia hasa nyuma). Usiikaze sana.
- Hakikisha kuwa tepi iko kwenye kiwango sawa kwa usawa nyuma na mbele.
- Pumua kawaida ukiwa umesimama wima na pima mzunguko wa kiuno chako mara tu baada ya kutoa pumzi.
- Rudia kipimo mara tatu, na ikiwa mbili au tatu kati yao ni tofauti, chukua wastani wa tatu kwa usahihi.
Upi ni Muda Mzuri Wa Kupima Saizi Ya Kiuno?
Ukubwa wa kiuno chako hubadilika mara kadhaa wakati wa mchana. Hivyo, wakati mzuri wa kupima kiuno chako ni asubuhi kabla ya kula au kunywa chochote.
Itakuwa bora ikiwa utajipima wakati na katika hali ile ile kila wakati ili kupata majibu sahihi.
Nifanye nini kama nina saizi kubwa ya kiuno?
Ikiwa mzunguko wako ni mkubwa, unaweza kupata ushauri kutoka kwa daktari wako kuhusu hatua za kufuata, ikiwa ni pamoja na kupunguza uzito.
SAIDIA WENGINE
Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.
HES-P-D-BDW-1_19016
HES-P-D-SET-D8_31212
HES-WB-01_1212
HES-P-D-DM-2_22878
DM-BP-01_12034
HES-P-D-BPA-12_18778