Nini Maana Ya Mawimbi

Utakumbuka wakati ule ametangazwa mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 Tanzania, watu wengi walianza kuchukua tahadhari. Lakini kirusi alishaingia Tanzania. Watu baadhi wakaumwa. Kwakuwa tahadhari ilikuwa juu, idadi ya waliokuwa wanaumwa ikaanza kupungua. Virusi hawakuwa wameisha! Walikuwa wachache. Na walizunguka kwa watu wachache.

Virusi wakaendelea kusambaa kwa watu kidogo kidogo. Mwisho walioambukizwa wakawa wengi! Nao wengi walioambukizwa virusi wakaweza kuwaambukiza wengi….. Idadi ikawa kubwa tena! Ikawa kama wimbi la maji: lilipanda, likashuka, likapanda tena. 

Wimbi linamaanisha kuongezeka kwa idadi ya watu wagonjwa, na kisha kupungua. Neno “wimbi” linamaanisha muundo wa asili wa vilele na mabonde. Maana yake ni kwamba wakati wa mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza, hata kama maambukizi yamepungua, milipuko ya baadaye ya magonjwa inawezekana.

“Mawimbi” yanamaanisha upunguaji au ukosefu wa mzunguko wa virusi kwa kiwango cha kusababisha mlipuko. Kupungua kwa mzunguko wa virusi hutokana na kukata mnyororo wa uambukizaji kutoka kwa mtu au vitu vilivyo na vimelea vya magonjwa. Haimaanishi kwamba virusi waenezao ugonjwa huo wamekwisha

Ukiwa umedhidibiti magonjwa ya mlipuko, Ukilegea tu, unapata wimbi. Kwa maana ingine, unatakiwa ujipange kuzuia wimbi. 

Kinachosababisha ugonjwa kupungua

  • Kuchukua hatua madhubuti za kupunguza maambukizi. Mfano Kuvaa barakoa, kukaa umbali ulioshauriwa (1 mita), kusafisha mikono.
  •  Kujikinga kwa kutumia chanjo
  • Kutibu ugonjwa wenyewe
 

Kinachosababisha Wimbi (Ongezeko la Ugonjwa)

Visababishi vya wimbi huwa ni kinyume cha vinavyo sababisha ugonjwa upungue. Kwa maana ya kwamba, usipochukua hatua madhubuti za kupunguza maambukizi, usipopata chanjo na kama wagonjwa hawatibiwi basi virusi vitaendelea kuwepo na kuwaathiri wengine. Wengine wengi. Wimbi.
Sababu ingine muhimu ni, kubadilika kwa virusi vyenyewe na kuwa sugu kwa dawa zianazotumika kutibu au chanjo zinazotoa ulinzi dhidi ya virusi hivyo. Tumeshasikia kwamba virusi vilivyogundulika Africa ya Kusini vilikuwa sugu kwa chanjo mojawapo za Corona.

Wimbi la 3 la COVID-19: Tutegemee nini?

Bila shaka, kila mtu, taasisi na mataifa yangependa kuona yanapata ushindi dhidi ya Corona. Kutafakari swali hili MUHIMU yafaa tuzingatie mambo matatu (3) MUHIMU. Moja, sababu ya kuingia kwa wimbi la sasa. Pili, kirusi anayesababisha wimbi la sasa. Na tatu, tumejipangaje kukabiliana na wimbi hili na kuzuia yajayo?

Tanzania tuna nafasi nzuri ya kuishinda Corona kwa kuwa tuna uzoefu tofauti wa mawimbi mawili tofauti: wimbi la kwanza tulilishinda vizuri. Wimbi la pili lilipita na bila shaka tulijifunza kulingana na hali ilivyokuwa. 

Aina ya kirusi anayesababisha wimbi husika: Kama kirusi anayesababisha wimbi hili ni ambaye kajibadilisha tutegemee yafuatayo: Kasi ya maambukizi inaweza kuwa kubwa kuliko ilivyokuwa kwenye mawimbi yaliyotangulia na kubadilika kwa dalili za Corona. Kwa wakati huu, ni muhimu sana kuhakikisha unapata habari za uhakika kuhusu Corona kutoka katika mamlaka zenye uhakika!

Utayari wa kukabiliana na wimbi hili pamoja na kuzuia mawimbi mengine ni MUHIMU. Ni jukumu la KILA MMOJA. Na huitaji ushirikiano wa sekta zote. Na nchi zote. Yafuatayo ni Muhimu kuzingatia:

  1. Kwakuwa ueneaji wa COVID-19 bado umebaki kuwa ule ule licha ya kubadilika kwa aina ya virusi, ni muhimu kuhakikisha tunazingatia maelekezo yote kutoka mamlaka husika za Afya.
  2. Kwakuwa kufahamu  aina ya virusi ni muhimu kukabiliana na mawimbi haya, mamlaka husika hutengeneza uwezo kwa wataalamu wa Afya kugundua aina, kutengeneza chanjo na hata dawa.
  3. Kutambua wagonjwa na kuanza tiba mapema, tutegemee kuimarishwa kwa nyenzo pamoja na utambuzi wa watu ambao wana dalili za mapema kama vile joto kupanda

Hitimisho

  • Wimbi ni muongezeko wa idadi kubwa ya watu walioambukizwa ugonjwa.
  • Wimbi huweza kutokea kipindi chochote cha makabiliano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kuambukiza.
  • Jitihada za kujiepusha na hatari ya kuambukizwa ziboreshwe katika ngazi zote, mtu mmoja mmoja, jamii na taasisi. Kupata wimbi ni chaguo kama ilivyo kuepuka wimbi

******Desclaimer: makala haya hayajakaguliwa na wana-epidemiolojia. Maoni yaliyotolewa katika ufafanuzi huu yanawakilisha maoni ya waandishi na sio lazima ya taasisi ya mwenyeji, the

 

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu FAHAMU Wimbi la Magonjwa Ya Kuambukiza?
Mimi ni Dr. Adinan