Figo kufeli ni nini?
Figo kufeli ni ugonjwa unaowatesa takribani watu 10-17 kati ya 100 Tanzania, na zaidi ya watu milioni mbili wakihitaji huduma ya kusafisha au kubadilisha figo Kusini mwa jangwa la Sahara. Madhara ya figo kufeli hujumuisha ya kiuchumi na kijamii. Gharama ni kubwa za matibatu ukiacha ukweli kwamba hazipo kila sehemu.
Kuna uhusiano wa figo kufeli, presha na kisukari?
Kisukari na shinikizo la damu ni sababu mbili kuu za figo kushindwa kufanya kazi (figo kufeli). Figo zina jukumu muhimu katika kudhibiti shinikizo la damu kwa kutoa homoni iitwayo renin, ambayo husaidia kudhibiti presha ya damu.
Kwa watu wenye kisukari, viwango vya juu vya sukari kwenye damu vinaweza kuharibu mishipa midogo ya damu kwenye figo, na hivyo kupunguza uwezo wao wa kuchuja taka kutoka kwenye damu. Baada ya muda, uharibifu huu unaweza kusababisha hali inayoitwa ugonjwa wa figo wa kisukari (dibetic nephropathy kwa kimombo).
Bila tiba na kudhibiti kisukari, ugonjwa wa figo wa kisukari huweza kuendelea hadi kufikia figo kufeli.
Figo kufeli pia inaweza kusababishwa na shinikizo la damu lisilodhibitiwa. Shinikizo la juu (presha) la mara kwa mara katika mishipa ya damu inaweza kuharibu mishipa ya damu katika figo, hivyo kupunguza uwezo wa figo kuchuja taka kutoka kwenye damu.
Figo kufeli pia husababisha presha. Kupungua uwezo wa figo kuchuja taka husababisha mrundikano wa taka hizi mwilini. Taka hizi husababisha mishipa kusinyaa na hivyo kusababisha presha kupanda tena.
Idadi ya watu wenye tatizo la figo kufeli inaongezeka, kwanini?
Ni muhimu kutambua kwamba shinikizo la damu na ugonjwa wa kisukari mara nyingi hayana dalili, ikimaanisha kwamba watu walio na magonjwa haya wanaweza wasiwe na dalili zozote hadi madhara yatokee.
Nawezaje kuepuka figo kufeli kama ninaugua presha au kisukari?
Ufuatiliaji wa mara kwa mara wa shinikizo la damu na viwango vya sukari vya damu haswa wa nyumbani unaweza kusaidia kugundua na kudhibiti magonjwa haya kabla hayajasababisha madhara makubwa kama vile figo kufeli.
Fahamu hatua nyengine unaweza kuchukua kulinda figo zako ili kuepuka figo kufeli.
Ufanye nini kuanzia leo kuepuka figo kufeli?
Nakushauri mambo mawili muhimu:
- Mosi, kubali kimatendo kwamba kufuatilia afya yako ni jukumu lako, na
- la pili fahamu na ishi ukweli huu, kwamba magonjwa yenye athari kubwa na za muda mrefu kwako na familia yako yanaweza yasioneshe dalili!
Kwahiyo, kwa kifupi, ya kufanya ili kuepuka magonjwa haya ikiwemo figo kufeli ni:
- Fuata mtindo wa maisha mzuri kwa afya yako: kula vizuri, fanya mazoezi, wacha matumizi ya tumbaku nk.
- Fundisha familia yako na wengine namna ya kujali afya zao. Itazidisha ufanisi upande wako
- Hakikisha unafahamu hali yako kwa uhakika – itapendeza ukiwa na vipimo muhimu nyumbani haswa vya presha na kisukari.
Dhibiti presha na Epuka Madhara
Anza leo kufuatilia presha yako. Pata kipimo cha presha kwa bei ya offer!
Pata Offer Yako Leo!