Madhara ya Presha: Kwa Hakika, Ni Ukweli Usiopingika
Kwa hakika, ni ukweli usiopingika kwamba matibabu ya shinikizo la damu mara nyingi yanaweza kuepusha madhara makubwa kama vile moyo kufeli au figo kufeli.
Lakini je, umewahi kujiuliza kwa nini baadhi ya watu wanapopata matibabu bado wanakumbwa na madhara haya hatari?
Tukusaidie Kudhibiti Presha?
Muulize Dr. Adinan sasa akushauri namna sahihi ya kudhibiti Presha. Utalipia TSh. 4900/= tu!
Siri Iliyofichika ya Madhara ya Presha
Ninapofikiria kuhusu hili, napata kumbukumbu ya watu ambao wamepambana na presha kwa muda mrefu, lakini wanaishia kupata madhara ya presha kama vile kiharusi, moyo au figo kufeli.
Namaanisha, si ajabu kusikia hiki, mgonjwa alikuwa anapatiwa matibabu ya presha tangu mwaka fulani, lakini mwezi uliopita figo zilifeli na mauti yakamfika.
Swali la kujiuliza hapa ni: Je, mbona wamepata madhara ya presha wakati walikuwa kwenye matibabu ambayo kimsingi yalitakiwa kudhibiti presha na kuwakinga na madhara ya presha?
Je, Kwa Nini Madhara Haya Yanatokea?
Swali lingine unaloweza kujiuliza ni mbona wataalamu wa afya wanasema madhara ya presha yanaweza kuepukwa, sasa mbona wengi bado wanayapata ingawa wanatibiwa?
Kama umejiuliza swali hili basi wewe ni mtu makini sana, na kama hujawahi kujiuliza suala hili lakini unasoma makala haya maana yake unajali sana afya yako!
Nami niko hapa kukujibu.
Hadithi Fupi ya Mgonjwa Aliyepuuza Kipimo
Baada ya kumaliza mafunzo yangu ya udaktari, nilishiriki katika utafiti uliolenga kuboresha ugunduzi wa wagonjwa wa presha kwa kuwawezesha kupima presha zao katika maduka ya dawa.
Ni wakati huo nilipogundua kwa masikitiko, kwamba wagonjwa wengi hupata madhara ya presha bila kufahamu.
Kumbukumbu moja inanijia kichwani, kuhusu mshiriki mmoja wa utafiti ambaye aligunduliwa kuwa na presha kubwa wakati wa vipimo.
Nilipojaribu kumpa rufaa kwenda hospitalini, alinijibu kwa kusema kwamba kwa wakati ule atasubiri kwanza atakwenda hospitali wakati mwengine kwa sababu wakati ule presha haijamsumbua.
Nilipogundua siku iliyofuata kuwa alikuwa amepata kiharusi na kulazwa hospitalini, niliguswa sana na ukweli huo.
Tumejifunza Nini na Tunaweza Kufanya Nini?
Kabisa, ni muhimu kujiuliza: Je, tumejifunza nini kutoka kwa hadithi hizi na ni hatua gani tunaweza kuchukua ili kuzuia madhara ya presha kwa kadri tunavyoweza?
Baada ya kumaliza masomo yangu na kubobea kwenye utafiti, nimegundua pia ni asilimia ndogo tu ya wagonjwa walio kwenye matibabu hufaidika kikamilifu na matibabu.
Bado pia wengi walioko kwenye matibabu hupata madhara ya presha. Ziko sababu tatu – nimezigawa hivi ili kuweza kukufahamisha kwa urahisi.
1. Kutokuwa na uelewa sahihi kuhusu presha
Wengi hawana uelewa sahihi wa ugonjwa wa presha, mfano kutokufahamu ugumu wa kutambua kama una presha.
Pia wengi hawafahamu mtu aliyeko kwenye hatari ya kutokuweza kudhibiti presha, vitu unavyoweza kufanya kudhibiti presha.
Lakini pia, huwenda hata wewe hufahamu namna sahihi ya kutumia dawa za presha: ziwe za hospitali au za asili. Na mbaya zaidi huwafahamu namna ya kutathmini tiba.
Nitakupa mfano kwanini ni muhimu kuwa na ufahamu wa ugonjwa wa presha. Je, ulishawahi kujua kwamba hakuna dalili maalum ya ugonjwa wa presha?
Nikimaanisha, unafahamu presha inaweza kuwa juu bila ya wewe kuwa na dalili hata moja?
Sasa nikwambie hii ni siri kubwa sana ambayo wengi hawajui.
Na ndiyo inasababisha mamia kwa maelfu kuendelea kupata madhara ya presha ingawa wako kwenye matibabu.
Unajua namna kutegemea dalili kunavyochangia kupata madhara ya presha? Endelea kusomanitafafanua wakati nakufahamisha kuhusu sababu ya tatu.
2. Hawafahamu presha zao
Wagonjwa wengi hawafahamu umuhimu wa kufahamu presha zao, kufahamu kwa uhakika kama wanamadhara yeyote ikiwa walikuwa na presha ipo juu kitu ambacho husababisha wengi kuchelewa.
Kwa mfano huo hapo juu, wengi hufuatilia presha zao kwa hisia wakisubiri dalili, hawapimi presha zao.
Ngoja nikuulize kitu, kama ulishawahi kwenda hospitali hata kama unakwenda kwa ugonjwa ambao hauusiani na presha, lazima upimwe presha ushafahamu ni kwanini?
Nitakujibu hivi punde.
Fahamu ya kwamba, iwe uko kwenye matibabu au bado haujagundulika kama una presha, ili kuepuka madhara ya presha ni LAZIMA uwe unafahamu presha yako.
Yani ni LAZIMA UPIME. La sivyo utadumbukia kwenye sababu ya tatu inayohatarisha kupata madhara ya presha.
3. Kutokuchukua hatua stahiki mapema
Unafahamu wagonjwa wengi huwa tayari na madhara ya presha wakati wakiwa wamegundulika kwamba presha zao ziko juu? Kwanini?
Wagonjwa wengi huchelewa. Lakini swali la msingi ni kwanin wagonjwa huchelewa kuja hospitali? Madhara ya shinikizo la juu la damu hutokeaje?
Unakumbuka nilikwambia nitakujibu hili swali? Unajua namna kutegemea dalili kunavyochangia kupata madhara ya presha?
Shinikizo la juu la damu, pia hujulikana kama muuaji wa kimya kimya, ni ugonjwa wa kudumu ambao unaweza huathiri mishipa midogo ya damu katika viungo muhimu vya mwanadamu.
Madhara ya presha hutokea taratibu na kwa muda mrefu. Watu huchelewa kubaini wakati uharibifu huu unatokea.
Sababu ni moja tuu. Presha haiumi!
Hakuna dalili maalum ya presha. Kutokujua imekuwa sababu maalum kwanini bado presha inaendelea kuleta madhara na kusababisha vifo.
Epuka madhara ya presha
Kumbuka kauli mbiu ya AFYATech (F3) kuishi kwa amani na furaha haswa katika mazingira yetu yenye magonjwa mengi, Fahamu, Fuatilia. na Fanya kinachostahili mapema. Furahia maisha.
Kwahiyo kabla hujataka kudhibiti inabidi ufahamu presha yako kwanza! Fuatilia afya yako na uwe na uhakika nayo kwa kufanya vipimo muhimu hospitali na kuwa na vipimo vya kufuatilia afya yako ukiwa nyumbani.
Bonyeza HAPA kuvifahamu vipimo muhimu kukusaidia kudhbiiti presha na ukivihitaji tutakupatia kwa bei ya offer.
Kisha chukua hatua stahiki mapema kufuata matibabu ambayo yanajumuisha dawa, au mabadiliko ya mfumo wa maisha au lishe au vyote kwa pamoja. Kuchukua hatua stahiki ni pamoja na kuwa na mtaalamu wa afya pamoja na watu watakaokuwa wanaku-support kwa kukupa ushauri haswa unapokuwa nyumbani, nje ya hospitali.
Huwa ni ngumu kupata supoti inayojua mambo ya afya ndiyo maana AFYATech tukaanizisha AFYAPlan kuwa mshirika wako kudhibiti presha. Kupitia AFYAPlan utajifunza
Nifanye nini ninapopata madhara ya presha?
Ikiwa umepata au utapata madhara ya shinikizo la damu, ni muhimu kutafuta matibabu mara moja.
Usikate tamaa kwakuwa umepata madhara ya presha. Unapowahi kutibu hupunguza uwezekano wa madhara haya kuwa makubwa zaidi.
Kulingana na madhara uliyopata, matibabu yanaweza kuhusisha dawa, mabadiliko ya mtindo wa maisha, au upasuaji.
Baadhi ya madhara ya presha hupona ikiwa yatashughulikiwa kwa haraka. Lakini pia, madhara mengine ya presha hayaponi na kurejea katika hali ya mwanzo.
Ni muhimu kushirikiana kwa ukaribu kabisa na tabibu wako kuhakikisha unadhibiti shinikizo la damu na kuzuia madhara presha.
Kumbuka fahamu. dhibiti . furahia maisha.