fbpx

Kisukari / Diabetes Mellitus

Kisukari, ni ugonjwa unaosababisha kuwa na sukari zaidi ya kiwango kinachotakiwa kwenye damu. Madhara mabaya ya kisukari ni ukaukaji wa maji kwenye seli za mwili, koma na kifo kama hujatibiwa kwa haraka.

Ugonjwa huu ni mkubwa kiasi gani? Inakadiriwa kuwa kati ya watu 100, nane wana ugonjwa wa kisukari. Hatahivyo, kwakuwa sukari inaweza kuwepo kwa muda mrefu bila kuonesha dalili, karibia asilimia 30% ya wanye kisukari hawajijui. Hii husababisha wengi kuwa tayari na madhara ya kisukari wakati wanapogundulika kuwa na ugonjwa huu.

Kisukari husababishwa na kuharibiwa kwa seli kwenye Kongosho au kutokufanya kazi kwa insulin au vyote kwa pamoja. Kongosho ina seli zijulikanazo kama Beta. Seli hizi ndizo hutoa Insulini. Utafiti unaonesha kwamba mwili hushindwa kuzalisha seli hizi kama zitaharibika kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 30.

Soma zaidi

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Kisukari?
Mimi ni Dr. Adinan