Madhara ya kisukari: Kinywa na Meno

Facebook
Twitter
WhatsApp

Imeandikwa na Dr. Adinan J. MD. MSc. FDHS. F.Forgatty, mtafiti wa magonjwa na  mkufunzi wa vyuo vya Afya kwa zaidi ya miaka 10. 

Madhara ya Kisukari: Kinywa na Meno

Ugonjwa wa Kisukari husababisha kiwango cha sukari kuwepo kwa wingi katika damu na hivyo katika mate yako. Bakteria walioko mdomoni hutumia sukari hii kama chakula. Kwa hiyo bakteria hukuwa na kustawi zaidi katika mazingira yenye sukari.  Bakteria hawa husababisha meno kuoza na kutoboka. Na kama hujapata tiba haraka unaweza kupoteza jino kwa kung’oa. 

Kumbuka tulisema kisukari hupunguza kinga ya mwili kwa kuharibu seli nyeupe. Seli nyeupe hukusaidia kupambana na magonjwa kwa kuwakamata na kuwaharibu bakteria wanapoingia kwenye mwili.

Unaweza kupata changamoto zifuatazo mdomoni kama una kisukari

  • Kukauka kwa mate
  • Vidonda visivyopona haraka mdomoni
  • Fizi kuoza na kutoka damu kirahisi\
  • Meno kuoza na kutoboka

Namna ya kuwa na afya bora ya kinywa na meno

Kudhibiti sukari ni silaha yako muhimu. Unapodhibiti sukari pia hukuwezesha kudhibiti magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.  

Hakikisha unapata huduma kutoka kwa mhudumu wa afya pindi utakapokuwa na dalili zifuatazo

  • Fizi kuwa nyekundu kuliko kawaida ulivyozoea
  • Fizi kutoka damu kwa urahisi

Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku na kutumia fluoride. 

Ukiwa Tayari! Namna 3 tunasaidia kuboresha afya yako

  1. AFYAPlans inakuwezesha Kudhibiti na kuepuka madhara kisukari: Ungana na Daktari wako kwa msaada na mwongozo binafsi Kuhusu dawa, VIPIMO, maarifa na ujuzi. Bonyeza HAPA kujiunga grupu letu. 

  2. Vitabu vya Elimu vinavyokuwezesha kufanya Maamuzi sahihi kuboresha afya yako. Mfano kudhibiti kisukari huku ukila Vyakula unavyovipenda. Bonyeza HAPA kufahamu zaidi

  3. Vifaa vya Matibabu ya Nyumbani vinavyokupa amani na uhakika wa afya yako muda wote. Bonyeza HAPA kuvifahamu.

Uko tayari kuboresha AFYA Yako? Tuwasiliane

Leave a Replay

Zilizosomwa zaidi

Follow Us on Facebook

Follow Us on Twitter

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Madhara ya kisukari: Kinywa na Meno?
Mimi ni Dr. Adinan