fbpx

Tafiti nyingi zinaonesha kuwa mazoezi ya kawaida ya mwili yanadhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza na pia ni kinga. 

Kwa mfano, mazoezi hukusaidia kudhibiti shinikizo la juu la damu (Presha) na kudumisha uwiano mzuri wa uzito na urefu (BMI)

Hivyo, mazoezi, hukusaidia kudhibiti na kujikinga na presha na magonjwa yasiyoambukiza na madhara yake mfano ugonjwa wa moyo, figo, kiharusi nk.

Mazoezi Humnufaisha Mgonjwa wa Presha kwa Mambo 6 Muhimu 

1- Moyo huongeza kasi ya mdundo na hivyo kuongeza uimara

2 – Hupunguza Cholesterol/lehemu mbaya hivyo kukukinga na magonjwa ya mishipa ya damu na moyo ikiwamo presha na kiharusi

3 – Hutoa chemikali inayoitwa Adenosine, inayokufanya uwe na nguvu na kujisikia fit muda wote

4 – Hutoa kemikali inayokufanya uwe na raha na kuondoa stress

5 – Unapochakata misuli unasababisha iweze kuitikia vema kazi/maelekezo ya insulin. Hivyo kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu.

6 – Kuishughulisha misuli na mifupa husababisha kuimarika zaidi.

Kwasababu ya faida hizi, mazoezi ni kipengele muhimu katika matibabu ya presha. Hivyo mgonjwa wa presha hata kama anatumia dawa, atapunguza hatari ya kupata madhara ya presha kama akichanganya na mazoezi.

Usisubiri, anza sasa kufanya mazoezi ili kudhibiti presha na madhara yake. Hujachelewa!

Najua swali unalojiuliza ni aina gani ya mazoezi ufanye? 

Kama ndivyo, usihofu nimekuandikia makala hii kukuwezesha kudhibiti na kuepuka madhara ya presha na kisukari. Kwahiyo nitakueleza aina na namna y akufanya mazoezi. Endelea kusoma

Nifanye Mazoezi ya Aina Gani Kudhibiti Presha?

Aina ya Mazoezi Kudhbiti Presha

Mazoezi ya mwili kama vile kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea na Kuruka kamba yanatosha kukusaidia kudhibiti presha yako na kuepuka madhara yake.

Mzunguko wa Mazoezi

Fanya mazoezi ya aerobic ikiwezekana siku zote za wiki. Ukishindwa siku 3 katika wiki inatosha.

Ukali wa Mazoezi

Zoezi linapaswa kuwa angalau kwa kiwango cha wastani (k.v kutembea haraka, kukimbia kidogo, kuruka kamba nk)

Muda wa Kufanya Mazoezi

Fanya dakika 30 hadi 60 mfululizo au katika vipindi vya kupishana angalau kwa dakika 10.

Uchukue Tahadhari Gani Unapofanya Mazoezi Kudhibiti Presha?

Usifanye mazoezi mazito ikiwa hujadhibiti presha yako. 

Pia, usifanye mazoezi mepesi kwa muda mrefu sana kama hujadhibiti presha yako. 

Unapaswa kupunguza kasi na muda wa mazoezi mpaka pale utakapokuwa umedhibiti presha yako.

 

SAIDIA WENGINE

  • Tutafurahi kusikia maswali au maoni yako kuhusu makala haya. Tafadhali tuandikie hapo chini.
  • Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.
 
Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Mazoezi kuzuia au Kudhibiti Presha?
Mimi ni Dr. Adinan