Fahamu Aina za Tiba ya Kisukari

Facebook
Twitter
WhatsApp

Imeandikwa na Dr. Adinan J. MD. MSc. FDHS. F.Forgatty, mtafiti wa magonjwa na  mkufunzi wa vyuo vya Afya kwa zaidi ya miaka 10. 

Je, Kuna Tiba ya Kisukari?

Tiba ya kisukari kwa sasa ni suala lenye majibu mawili: Kuna tiba na hakuna tiba ya kisukari.

Jibu litategemea aina ya ugonjwa wa kisukari mtu anayo.

Kama unatafuta taarifa kuhusu tiba ya kisukari hii makala itakujibu maswali na kukukata kiu.

Tukusaidie Kudhibiti Kisukari?

Fahamu namna AFYAPlan inaweza kukusaidia kudhibiti kisukari!

Aina za Kisukari Zinazotibika

Kuna aina takribani kuu nne za kisukari ingawa aina mbili za kisukari ndiyo mashuhuri: Kisukari cha Aina ya 1 na Kisukari cha Aina ya 2.

Kisukari cha Aina ya 1 hakitibiki lakini kinadhibitiwa kwa kutumia insulini.

Kisukari cha Aina ya 2, kwa upande mwingine, kinaweza kudhibitiwa kwa mabadiliko ya mtindo wa maisha, lishe bora, na wakati mwingine dawa. Kwa hivyo, tiba ya kisukari cha aina ya 2 inahusisha kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu kupitia njia mbalimbali.

Kisukari cha ujauzito, aina hii ya kisukari huwapata wanawake wajawazito. Aina hii inaweza kupona baada ya mama kujifungua.

Kisukari kinachotokana na magonjwa mengine, mfano ugonjwa wa matezi kwenye figo na kwenye mayai ya uzazi ya mwanamke. Magonjwa haya husababisha kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu. Lakini yanatibika na hivyo aina hii ya kisukari hutibika.


Jinsi unavyoweza kudhibiti kisukari

Kisukari ni ugonjwa wa muda mrefu. Ingawa hakuna tiba kamili ya kuponya kisukari, kuna njia nyingi za kudhibiti na kuepuka athari zake.

Makundi ya Tiba ya Kisukari

Tiba ya ugonjwa wa kisukari imegawanyika katika makundi yafuatayo:

  • Lishe: Kuzingatia ratiba ya vyakula vyenye kiwango kidogo cha sukari na ambavyo haviongezi sukari kwenye damu kwa muda mfupi

  • Mazoezi: Kudhibiti uzito na kufanya mazoezi mara kwa mara.

  • Dawa: Kutumia dawa za kupunguza sukari kwenye damu.

  • Insulini: Kwa wagonjwa wa Kisukari cha Aina ya 1 na baadhi ya wagonjwa wa Kisukari cha Aina ya 2.

Kutathmini Tiba ya Kisukari

Namna ya kutathmini tiba ya kisukari inategemea na matokeo ya vipimo vya sukari kwenye damu na hali ya mgonjwa.

Daktari wako atakuelekeza kutoa damu kwa ajili ya kupima kipimo cha HbA1C kuweza kutathmini matibabu yako.

Hatahivyo, anaweza kutumia mashine kama unayotumia nyumbani (Kama huna hakikisha unapata yako boss kwani itakusaidia kufanya tathmini ya tiba yako ukiwa nyumbani) kupima kiwango cha sukari kwenye damu. 

Ili kusema tiba yako imekaa sawa sawa na unafikia lengo, majibu ya vipimo vyako yanatakiwa kuwa kama ifuatavyo:

  • Wagonjwa wengi wanaweza kutarajiwa kulenga HbA1c ya 7.0%

  • Lengo la HbA1c linaweza kupunguzwa (k.m. hadi <8% au  kwa watu wenye hatari ya sukari yao kushuka mara kwa mara, au ambao ni wagonjwa sana.

  • Wagonjwa wanaotibiwa na lishe, shughuli za mwili na metformin (hatari ndogo sana ya hypoglycemia) wanapaswa kuhimizwa kufikia lengo la chini la HbA1c (Chini ya 7).

  • Ikiwa kipimo cha HbA1c hakipatikani Kiwango cha sukari masaa 6 baada ya kula ya chini ya 7.0 mmol/L  na kiwango cha sukari masaa 2 baada ya kula ya chini ≤9.0 mmol/L 

Vipimo vya mara kwa mara vinaweza kusaidia kugundua jinsi tiba inavyofanya kazi. Pia, ni muhimu kufuata ushauri wa daktari na kurekebisha tiba kulingana na mahitaji ya mwili.

Kuhusu Hadithi Potofu Kuhusu Tiba ya Kisukari

Hadithi nyingi potofu zipo kuhusu tiba ya ugonjwa wa kisukari. Moja ya hadithi ni kwamba kisukari kinaweza kutibiwa kabisa kwa njia za asili pekee.

Ukweli ni kwamba, lishe bora na mazoezi ni muhimu, lakini tiba ya kisukari inahitaji mbinu nyingi kwa pamoja ili kuwa na ufanisi. Ili kudhibiti ugonjwa huu, mgonjwa anapaswa kushirikiana na mtaalamu wa afya.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti kisukari kwa kutumia vyakula, tunapendekeza ununue kitabu chetu maalumu kinachotoa mwongozo wa kina kuhusu lishe bora kwa wagonjwa wa kisukari.

Jali afya yako, jifunze zaidi na udhibiti kisukari kwa ufanisi!

Ukiwa Tayari! Namna 3 tunasaidia kuboresha afya yako

  1. AFYAPlans inakuwezesha Kudhibiti na kuepuka madhara kisukari: Ungana na Daktari wako kwa msaada na mwongozo binafsi Kuhusu dawa, VIPIMO, maarifa na ujuzi. Bonyeza HAPA kujiunga grupu letu. 

  2. Vitabu vya Elimu vinavyokuwezesha kufanya Maamuzi sahihi kuboresha afya yako. Mfano kudhibiti kisukari huku ukila Vyakula unavyovipenda. Bonyeza HAPA kufahamu zaidi

  3. Vifaa vya Matibabu ya Nyumbani vinavyokupa amani na uhakika wa afya yako muda wote. Bonyeza HAPA kuvifahamu.

Uko tayari kuboresha AFYA Yako? Tuwasiliane

Leave a Replay

Zilizosomwa zaidi

Follow Us on Facebook

Follow Us on Twitter

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Fahamu Aina za Tiba ya Kisukari?
Mimi ni Dr. Adinan