Moyo kufeli ni hali ambayo moyo hauwezi kufanya kazi yake vizuri katika kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Utakapomaliza kusoma makala hii utakuwa umefahamu kuhusu ugonjwa wa moyo kufeli, nini husababisha moyo kufeli, matibabu na kinga.

Kufeli kwa moyo husababisha matatizo mbalimbali ya kiafya na kuathiri ubora wa maisha.  vinavyosababisha moyo kufeli ni vingi na ni muhimu kuvijua ili kuchukua hatua za kuzuia na kutibu hali hii.

Takwimu za Ugonjwa wa Moyo Kufeli

Ugonjwa wa moyo kufeli ni tatizo kubwa la kiafya duniani kote. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani watu milioni 26.7 duniani kote wanaishi na ugonjwa huu.

Takwimu zinaonyesha kuwa ugonjwa wa moyo kufeli unachangia karibu asilimia 50 ya vifo vyote vinavyohusiana na magonjwa ya moyo.

Hii inafanya ugonjwa huu kuwa moja ya sababu kuu za vifo duniani. Inasikitisha kuwa idadi ya watu wanaougua ugonjwa huu inaendelea kuongezeka, na hivyo kufanya juhudi za kuzuia na kutibu ugonjwa wa moyo kufeli kuwa muhimu zaidi.

Barani Afrika, ugonjwa wa moyo kufeli ni tatizo linaloendelea kuongezeka. Tafiti zinaonyesha kuwa takribani asilimia 2 hadi 10 ya watu wazima barani Afrika wanaishi na ugonjwa huu.

Hata hivyo, idadi halisi ya watu wanaoishi na ugonjwa huu inaweza kuwa kubwa zaidi kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi na uchunguzi.

Sababu za ongezeko la ugonjwa wa moyo kufeli barani Afrika ni pamoja na mabadiliko ya mlo na mtindo wa maisha, kuongezeka kwa matumizi ya tumbaku, na kuongezeka kwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu.

Pia, upatikanaji mdogo wa huduma za afya na ukosefu wa elimu juu ya afya ya moyo ni changamoto kubwa katika kukabiliana na ugonjwa huu.

Epuka Madhara ya Presha !

Je, unajua? Tafiti zinathibitisha kwamba wanaofahamu presha zao huepuka madhara ya presha! Anza safari yako leo! 

Okoa TSh. 40,000/= Pata kipimo chako sasa!

Sababu za Moyo Kufeli

Sababu za moyo kufeli zipo nyingi. Ni muhimu kuzifahamu ili kuweza kuepuka au kuchukua tahadhari. Hapa chini nimeziorodhesha:

1. Shinikizo la Damu la juu (Hypertension):  Shinikizo la damu la juu au presha ni moja ya sababu kuu za moyo kufeli. Shinikizo la damu kubwa husababisha moyo kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kusukuma damu kupitia mishipa ya damu. Kwa muda mrefu, hii inaweza kusababisha moyo kudhoofika na hatimaye kufeli.

2. Ugonjwa wa Moyo: Ugonjwa wa moyo ni sababu nyingine ya moyo kufeli. Hii ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa mishipa ya damu ya moyo, kuziba kwa mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo, na matatizo ya valvu ya moyo. Magonjwa haya yanaweza kusababisha uharibifu kwenye miundo ya moyo na kusababisha moyo kufeli.

3. Matatizo ya Moyo Tangu Kuzaliwa: Baadhi ya watu wanaweza kuwa na matatizo ya moyo tangu kuzaliwa ambayo yanaweza kusababisha moyo kufeli. Matatizo haya yanaweza kuathiri muundo wa moyo au kazi yake na yanaweza kuhitaji matibabu ya upasuaji.

4. Matatizo ya Mapafu: Matatizo ya mapafu kama vile pumu, na ugonjwa wa kifua kikuu, yanaweza kusababisha moyo kufeli. Matatizo haya yanaweza kusababisha shinikizo kubwa kwenye moyo na kusababisha uharibifu wa muda mrefu.

5. Uvutaji wa Sigara na Matumizi ya Pombe: Uvutaji wa sigara na matumizi ya pombe yanaweza kusababisha uharibifu kwenye moyo na mishipa ya damu. Hii inaweza kusababisha moyo kufanya kazi kwa nguvu zaidi na hatimaye kufeli.

Aina za Ugonjwa wa Moyo Kufeli

  1. Moyo kufeli upande wa kushoto: Moyo hushindwa kusukuma damu kwa ufanisi kutoka kwenye chumba cha kushoto cha moyo kwenda sehemu mbali mbali za mwili.
  2. Moyo kufeli upande wa kulia: Moyo hushindwa kusukuma damu kwa ufanisi kutoka kwenye chumba cha kulia cha moyo kwenda kwenye mapafu.

Dalili za Moyo Kufeli

Dalili za moyo kufeli kutokea na uweza kuonekana na kutuama kwa maji. Unaweza ukajiuliza hii inatokeaje. 

Moyo unapokuwa unashindwa kusukuma damu kwa ufanisi ile damu kutuama kwenye mishipa na hivyo kwa sababu mishipa ina vitundu vitundu hupenya kutoka kwenye mishipa ya damu ya yesu na kwenda kwenye sehemu za mwili.

 Hii inaweza kuwa ni kwenye mapafu, kwenye misuli, au hata kwenye tumbo. Kwa hiyo mtu ambaye moyo wake umefeli anaweza kuonyesha dalili zifuatazo.

  • Kupumua kwa shida au kukosa pumzi
  • Uchovu na ulegevu haraka hasa kwa shughuli za kawaida ikiwemo kutembea au kupanda ngazi.
  • Kuvimba miguu, miguu, au sehemu nyingine za mwili
  • Kukohoa kwa shida au uwepo wa povu kwenye mapafu
  • Kupungua kwa uwezo wa kufanya shughuli za kawaida

Vipimo vya Ugonjwa wa Moyo Kufeli

Ili kuhakiki wangu cha moyo kufeli au kama yo wa mtu methali daktari wako anaweza kufanya vipimo vifuatavyo.

  • Echocardiogram: Inatumika kuangalia ufanisi wa moyo na jinsi unavyosukuma damu.
  • Electrocardiogram (ECG): Hutumika kuchunguza shughuli za umeme kwenye moyo.
  • X-ray ya kifua: Inaweza kuonyesha mabadiliko ya moyo na mapafu.

Tiba ya Ugonjwa wa Moyo Kufeli

Kama tulivyoona vinavyosababisha moyo kufeli vingi ikiwemo pressure ambayo haijalidhibitiwa, kisukari ambacho hakijadhibitiwa, pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza. Hivyo tiba ya moyo kufeli itazingatia visababishi.

Hivyo matibabu ya moyo kufeli yanaweza kujumuisha

  • Kudhibiti shinikizo la damu au kushughulikia ugonjwa wa moyo wa msingi.
  • Kupunguza mzigo kwa moyo kupitia dawa kama diuretiki na ACE inhibitors.
  • Mabadiliko ya mtindo wa maisha, kama lishe bora, mazoezi
  • kuepuka matumizi ya tumbaku na pombe.

Hujafanikiwa kudhibiti presha?

Usisononeke mwenyewe huku ukiwa na hofu. AFYAPlan imerudisha amani kwa wengi kwa kuwasaidia kudhibiti presha zao. 

Madhara ya Ugonjwa wa Moyo Kufeli

Moyo kufeli maana yake damu haifiki sehemu zingine za mwili kama inavyotakiwa. Na kwa sababu sehemu za mwili zinahitaji damu ili kupata lishe, hewa safi, kutokufika kwa damu sehemu hizo kwa kiwango kinachotakiwa huleta madhara. 

Madhara hayo hutokana na kutokuwepo kwa chakula, hewa safi na mrundikano wa uchafu. Hivyo kama mtu hajapata matibabu ya haraka ya moyo kufeli anakuwa kwenye hatari zifuatazo:

  • Kuongezeka kwa hatari ya kuzorota kwa hali ya moyo na matatizo mengine ya kiafya mfano figo kufeli.
  • Kushindwa kufanya shughuli za kawaida na kupungua kwa ubora wa maisha.
  • Kuongezeka kwa hatari ya kufariki kutokana na shida za moyo.

Kinga ya Ugonjwa wa Moyo Kufeli

Kudhibiti sababu zinazochangia, kama kudhibiti shinikizo la damu na kudhibiti ugonjwa wa kisukari.

  • Kula lishe yenye afya, yenye wingi wa matunda, mboga, na vyakula vyenye afya kwa moyo.
  • Kufanya mazoezi mara kwa mara na kuepuka kuwa na uzito uliopitiliza.
  • Kuepuka uvutaji sigara na matumizi ya pombe kupita kiasi.

Ni muhimu kukumbuka kuwa ushauri wa kitaalamu wa daktari unapaswa kutafutwa kwa ajili ya utambuzi sahihi, ushauri wa tiba, na maelekezo bora ya kuzuia na kusimamia ugonjwa wa moyo kushindwa.

Kwanini lakini?...

Hata wagonjwa hata walioko kwenye matibabu bado wanapata madhara ya presha? Fahamu uepuke

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Moyo Kufeli: Fahamu Sababu?
Mimi ni Dr. Adinan