Epuka Vidonda Vya Kisukari Unapotumia Monofilament

5/5

Usikubali kisukari kiharibu maisha yako kwa vidonda hatari. Monofilament ni suluhisho. Inakuwezesha kutambua hatari ya kupata vidonda mapema na hivyo kukuwezesha kuchukua hatua stahiki mapema kudhibiti.

Watu wenye kisukari wako katika hatari ya kuharibu mishipa yao ya fahamu, hasa katika miguu yao.

Kipimo cha monofilament ni njia rahisi na ya haraka ya kugundua ikiwa kuna upungufu wa hisia katika miguu ambao unaweza kuwa hatari ya kuunda vidonda visivyopona vizuri.

Kwa kupima hisia katika miguu na kutambua maeneo yasiyofaa, watu wenye kisukari wanaweza kuchukua hatua mapema kuepuka vidonda, maambukizi, au hata kukatwa mguu

Sh 19,900.0

Availability: In stock

Faida: Ishi na kisukari bila hofu ya kupata vidonda miguuni.

Vidonda kwa wagonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa sana inayosababisha ulemavu unaotokana eidha kwa kukatwa miguu au mikono. Haya yote yanaweza kudhibitika kama tahadhari itachukuliwa katika muda muafaka. Hatahivyo, wengi wa wagonjwa wa kisukari hawajui.

Sukari husababishaje Vidonda? Sukari inatakiwa ihifadhiwe kwenye tishu, isikae ndani ya damu. Inapokaa kwenye damu kwa kiwango kikubwa husababisha sumu inayofanya uharibifu kwa namna tatu.

1. Kwanza huaribu mishipa ya fahamu na hivyo hutoweza kuhisi. Ukosefu wa hisia husababisha mwenye kisukari kutokufahamu kama mguu unaumia-mkandamizo kwamfano kubanwa na kiatu nk.

2.  Kisukari pia huaribu mishipa ya damu na -kama tulivyoona- kusababisha hali inayoitwa artherosclerosis. Hatimaye mishipa ya damu huziba haswa ile ya pembeni ya mwili kama vile miguu. Kukosekana kwa damu maana yake sehemu husika hukosa chakula, hewa safi na kinga. Hivyo sehemu hiyo hufa na kama utapata maambukizi hutapona kwa urahisi. Mara nyingi hii imekuwa sababu kubwa ya wagonjwa wa kisukari kukatwa miguu.

3.  Njia ya tatu, sukari huathiri kinga ya mwili kwa kuharibu na kupunguza muda wa kuishi wa seli zinazopambana na magonjwa.

Suluhisho: Kifaa hichi kitakusaidia kufahamu utimamu wa mishipa yako ya fahamu pamoja na kama bado una hisia kwenye miguu. Hivyo kifaa hichi kitakusaidia katika kujikinga na vidonda vya kisukari kwa kufanya yafuatayo. Kwa kuhakikisha unapambana kushusha sukari ukiwa na uhakika wa kiwango unachotaka kukishusha na kufahamu hali yako ya hisia kwenye miguu. Haya yote yatakuongezea ufahamu na hivyo kuchukua hatua stahiki.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Epuka Vidonda Vya Kisukari Unapotumia Monofilament”

Specify Facebook App ID and Secret in the Super Socializer > Social Login section in the admin panel for Facebook Login to work

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Unahitaji maelezo zaidi?