fbpx

Ni vipi kisukari husababisha ugonjwa wa figo?

Ugonjwa wa figo umekuwa ukisababisha watu wengi kufeli figo zao. Kisukari husababisha ugonjwa wa figo namna mbili.

Namna ya kwanza ni madhara ya moja kwa moja yatokanayo na uwepo wa kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu na namna ya pili ni kwa kusababisha presha.
 
Kisukari husababisha shinikizo la damu kuwa juu. Presha huaribu mishipa ya damu kwenye figo.

Cha kuzingatia ni kwamba madhara yote haya yanayotokea kwenye figo yanaweza yasiwe na dalili yeyote mpaka pale ambapo madhara yamekuwa makubwa na kuelekea kwenye figo kufeli.

Lakini habari njema ni kwamba, madhara yote haya yanaweza kugundulika na kupunguza hatari ya figo kufeli kama utafanya vipimo sahihi kwa wakati sahihi na kuchukua hatua stahiki. Lakini kuna changamoto moja.

Ugonjwa wa figo huanza taratibu kiasi kwamba wagonjwa wengi wa kisukari hugundua wakati athari imeshakuwa kubwa.

Hivyo ni muhimu kufuatilia afya yako kwa ukaribu kwa kufahanya vipimo mara kwa mara. 

Ninachomaanisha hapa ni kufanya vipimo kwa malengo mawili.

  1. Kufahamu kiwango chako cha sukari kwenye damu: kama hujagundulika una kisukari
  2. Kutathmini tiba: kupima kiwango chako cha sukari mara kwa mara kama unapata tiba ya kisukari. Lengo ni kufahamu uwezo wa tiba unayoendelea nayo kupunguza sukari kwenye damu. 

Mgonjwa wa kisukari ajikingije na  Ugonjwa wa Figo?

Madhara yote yanayosababishwa na kisukari yanaweza kugundulika na kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa figo na hivyo kupunguza hatari ya figo kufeli. 

Utaweza kujikinga na ugonjwa wa figo kama utachukua hatua stahiki kwa wakati. 

Utaweza  kuchukua hatua stahiki kama utafahamu mapema hali yako. Na njia pekee ya kufahamu ni kufanya vipimo.

Tafiti mbali mbali zinashauri mgonjwa wa kisukari kufanya yafuatayo ili kuepuka au kupunguza hatari ya kupata madhara kwenye figo.

  • Dhibiti sukari kwenye damu yako kadri uwezavyo. Namna ya kutathmini tiba yako.
  • Pata kipimo cha HBA1C angalau mara mbili kwa mwaka, mara nyingi zaidi ikiwa dawa yako itabadilika au ikiwa una hali zingine za kiafya. Shauriana na daktari wako kuhusu mara ngapi ni sawa kwako. (Fahamu vipimo muhimu kwa mgonjwa wa kisukari)
  • Hakikisha unafahamu kiwango chako cha presha ya damu. Angalau shinikizo la damu yako liwe chini ya 140/90 mm/Hg (au lengo ambalo daktari wako anaweka).
  • Weka uwiano wako wa uzito na kimo katika wastani unaoshauriwa kiafya. Kupunguza uzito – kwa watu wanene na wanene kupitiliza- angalau kwa asilimia 5 ya uzito wao hupunguza hatari ya madhara ya kisukari kwenye figo
  • Fahamu na dhibiti kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu. Fahamu zaidi kuhusu lehemu-bonyeza HAPA
  • Epuka kiwango kikubwa cha chumvi- hasa ile ya kuongeza mezani.
  • Kula matunda na mboga zaidi.
  • Fanya shughuli zinazotumia nguvu ya mwili kama vile mazoezi. Tafiti zinaonesha angalau ufanye mazoezi kwa dakika 150 kwa wiki. Ikiwa kila siku ni bora zaidi – angalau dakika 25 kila siku.
  • Fuata maelekezo ya matumizi ya dawa zako 

Siri Moja Kujilinda Dhidi ya Ugonjwa wa Figo

Kwa uzoefu wangu, mtu anapogundulika na kisukari hupata huzuni ghafla na kuanza kufikiria athari ambazo amekwisha kuziona zikiwatokea watu anao wafahamu, kama vile ugonjwa wa figo na moyo. 

Kumbe badala ya kuhuzunika, alitakiwa afurahi. Afurahi kwamba amegundua kuwa ana kisukari mapema. Na sasa anaanza kuchukua hatua stahiki mapema. 

Kufahamu hali yako ya kisukari mapema ndiyo siri. Ukishafahamu utaweza kuchukua hatua stahiki kwa wakati kudhibiti kisukari na kuepuka madhara yake.

AFYATech tunakusaidiaje? AFYATech tumekuwa tukitoa elimu kuhusu kudhibiti kisukari na presha kwa zaidi ya miaka 4 sasa kupitia maandiko na grupu za WhatsApp. Dr. Adinan amekuwa akitoa elimu sahihi kuhusu presha na kisukari na amekuwa akiongoza mijadala kati ya wagonjwa kuhusu namna sahihi ya kudhibiti presha na kisukari. 

Zaidi ya kutoa elimu, AFYATech huwapatia wahitaji vifaa na ushauri wa namna bora ya kuvitumia kudhibiti na kuepuka madhara ya presha na kisukari. 

Leo tutakusaidi kuweza kufahamu hali yako kwa uhakika na kukusaidia kudhibiti kisukari na kulinda moyo wako.

Nimeandaa video kuhusu umuhimu wa kuwa na vifaatiba hivi. Kuwa navyo nyumbani. Nimeelezea faida ya kuwa na vifaa hivi nyumbani.

Ingawa sasa umeshakuwa mtaalamu wa kisukari na namna ya kulinda moyo wako, ni muhimu kuangalia video hii itakayokufahamisha kwa kina kuhusu kuishi kwa furaha na amani huku ukiwa na kisukari.

Pia itakufahamisha umuhimu wa kuwa na vifaa na faida lukuki za kuwa na vifaa muhimu kudhibiti kisukari na presha. 

Ukifanikiwa, nitakupatia vifaa hivi kwa bei ya offer. Tafadhali bonyeza kitufe hapo chini kilichoandikwa PATA OFFER 

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Ugonjwa wa Figo: Namna 2 Kisukari huaribu figo na unavyoweza kuepuka!?
Mimi ni Dr. Adinan