Unafahamu Malengo Haya ya Matibabu ya Presha?
Mara nyingi huwa napata majibu ya kushtusha sana ninapowajulia hali wagonjwa wangu ninaowasaidia kudhbiti shinikizo la damu.
Huwa wakinijibu presha haijashuka bado, au presha yangu sasa iko sawa nimefurahi. Wakati mwengine ninapowauliza kuhusu malengo yao ya kujiuna na programu yetu ya kudhibiti presha. Majibu yao huwa hayatofautiani.
Jibu lao daima lilikuwa, “Nimekuja kwako kwa sababu sikuweza kudhibiti shinikizo la damu yangu.” Nakubaliana kabisa na kigezo hiki ambacho wagonjwa hutumia kuamua ufanisi wa matibabu yao.
Hata hivyo, kudhibiti presha peke yake ni moja ya malengo ya matibabu ya presha. Hivyo, kudhbiiti presha pekee haiwezi kutumika kama kipimo cha mafanikio ya matibabu. Nitaelezea hili kwa kuendelea na hadithi yangu.
Lakini ninapowauliza kuhusu hali ya figo zao, moyo wao, macho yao au hali ya damu yao, mara nyingi wanashindwa hubabika au hawana jibu kabisa. Kwa kuwa wao ni wagonjwa, ni muhimu kuwafanya waelewe kwa urahisi.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuna malengo mengine ya matibabu ya shinikizo la damu! Malengo haya yanafahamika kwa wataalamu wa afya na unatakiwa uyafahamu pia kama mgonjwa wa shinikizo la damu.
Narudia, ikiwa wewe ni mgonjwa unaishi na shinikizo la damu na unaendelea na matibabu, unahitaji kujua malengo ya matibabu yako na kama umeyafikia.
Sasa hebu tuangalie ni malengo gani yanayohusika katika matibabu ya shinikizo la damu.
1. Kushusha Presha
Lengo kuu la matibabu ya shinikizo la damu ni kushusha kiwango cha shinikizo la damu mwilini. Kulingana na ukali wa presha na hali ya mgonjwa mbinu mbalimbali kutumika kushusha presha.
Mara nyingi presha hushushwa kwa dawa. Kwani huchelewa kutambulika kama wana presha hivyo hivyo hospitali wakati presha zao ziko juu sana. Hivyo ili kuzuia athari wa kushusha presha kwa dawa.
Hata hivyo kama pressure itagundulika wakati wa haiko juu sana daktari wako anaweza kukushauri kushusha presha kupitia mabadiliko ya mtindo wa maisha kama vile lishe bora, mazoezi, kupunguza msongo wa mawazo.
Kumbuka ya kwamba presha ya juu isipodhibitiwa ndiyo huleta madhara. Kwa hiyo ni muhimu kuhakikisha kwamba unagundua mapema ili kuweza kuchukua stahiki mapema kushusha presha
2. Kuchunguza Madhara
Ni muhimu kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kutambua kama kuna madhara yoyote yamejitokeza kwa sababu ya presha kuwa juu.
Madhara haya yanaweza kuwa kama uharibifu kwenye moyo, figo, ubongo, au macho. Kupitia uchunguzi wa kiafya, madhara haya yanaweza kutambuliwa mapema na hatua za kuzuia zinaweza kuchukuliwa.
Kwa hiyo, ni muhimu kufanya vipimo na uchunguzi wa mara kwa mara ili kufuatilia afya yako na kuchukua hatua za kuzuia mapema.
3. Kutibu Madhara
Ikiwa madhara yoyote yamejitokeza kwa sababu ya presha ya juu, hatua za tiba zinapaswa kuchukuliwa haraka ili kuzuia madhara zaidi.
Hii inaweza kujumuisha matumizi ya dawa za kupunguza presha, mabadiliko ya lishe, na kufuata mwongozo wa daktari.
4. Kudhibiti na Kuepuka Madhara ya Presha
Kudhibiti presha maana yake ni kuhakikisha karibia muda wote iko katika kiwango kizuri kwa afya yako.
Lengo hli ni la muhimu lakini wagonjwa wengi wamekuwa wakipatia madhara hapa. Huwa wanasahau kama presha haiumi hivyo husahau kila kitu.
Ili kufikia hatua hii unahitajika kufanya yafuatayo:
- Kudumisha matumizi ya dawa! Hakuana kuacha mpaka ushauri wa daktari
- Kuduumisha mtindo wa maisha weneye afya wakati wote
- Kuhudhuria kliniki kama mlivyokubaliana na daktari wako
- Kufanya vipimo muhimu kufuatilia afya ya viungo muhimu
- Kama una busara utakuwa na kipimo chako cha presha nyumbani
Ni muhimu kufuata maelekezo ya daktari wako na kufanya mabadiliko muhimu katika mtindo wako wa maisha ili kudhibiti presha yako na kuzuia madhara yoyote ya kiafya.
Kwa kuzingatia malengo haya, ni muhimu kwa watu wenye shinikizo la damu kufuata maelekezo ya daktari wao na kufanya mabadiliko muhimu katika mtindo wao wa maisha ili kudhibiti presha yao na kuzuia madhara yoyote ya kiafya.
Hii itawawezesha kuishi maisha yenye afya bora na kuepuka hatari za kiafya zinazohusiana na shinikizo la damu.
Katika machapisho yajayo, tutangalia changamoto zinazojitokeza katika matibabu ya shinikizo la damu na jinsi ya kuzikabili. Endelea kutembelea tovuti yetu ili kupata taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti shinikizo la damu na kuishi maisha yenye afya bora.
Dhibiti Presha & Kisukari
Wasiliana moja kwamoja na Dr. Adinan na jiunge kwenye group letu la WhatsApp lililowawezesha wengi kudhibiti kisukari na presha! Kwa mchango kidogo wa TSh. 4,900/= tu!