fbpx

Kwanini unashindwa kushusha kisukari licha ya kufuata masharti

Facebook
Twitter
WhatsApp

Imeandikwa na Dr. Adinan J. MD. MSc. FDHS. F.Forgatty, mtafiti wa magonjwa na  mkufunzi wa vyuo vya Afya kwa zaidi ya miaka 10. 

Kufahamu kwamba kisukari kudhbiti kisukari ni hatua mseto, vyakula utaratibu wa maisha na kutumia dawa ni jambo zuri kudhibiti kisukari.

Lakini huwezi kufanikiwa kama hufahamu na hujazingatia namna ya kutumia nyenzo hizi tatu kuleta matokeo chanya pamoja. Nitafafanua. 

Makala haya inalenga watu wanaopambana na kisukari, ambao pamoja na kufuata masharti ya matibabu na kutumia dawa, bado wanakabiliwa na changamoto ya kutokudhibiti viwango vya sukari katika damu.

Pia makala haya ni kwa ajili ya watu ambao wako mbioni kutafuta ufumbuzi zaidi ili kuboresha udhibiti wa kisukari na kuleta furaha kama waliyokuwa nayo kabla hawajaugua kisukari.

Lengo kuu la makala haya ni kutoa mwongozo na taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti kisukari zaidi ya matumizi ya dawa pekee.

Unapomaliza makala kusoma makala haya utafahamu hatua za ziada madhubuti za kudhibiti sukari yako.

Njia Ambazo Wagonjwa wa Kisukari wamekuwa wakijaribu kuzifuata bila mafanikio

Kwa nini njia za kawaida za matibabu ya kisukari, kama vile kutumia dawa, au nyongeza kama mabadiliko ya mfumo wa maisha, lishe, na usimamizi wa stress zinaweza zisitoshe? Na je, kuna umuhimu wa kuzingatia njia mbadala?

Wagonjwa wengi wa kisukari, hata watu wangu wa karibu , wakishaambiwa wana kisukari basi hupaniki na kuanza kufuata masharti ya tiba; kula vizuri, kufanya mazoezi na kutumia dawa.

Wengine kutumia dawa mbalimbali ikiwemo mchanganyiko wa dawa za hospitali na za kienyeji / mitishamba. Lakini bado wakienda kupima sukari iko juu. 

Nini hutokea? Je, kuna cha kufanya ili kuweza kudhibiti kisukari? Jawabu ni ndiyo, kuna njia. Lakini nikwambie tuu, huwa ni watu wachache sana wanaozifahamu, kuzifuata, na ndiyo maana ni wachache hufanikiwa.

Nafahamu umeanza kujiuliza, je nini ufanye? Kwa bahati nzuri niko kujibu swali hili. Lakini kwanza tufahamu kwanini wagonjwa hushindwa kushusha kisukari?

Kwanini wagonjwa hushindwa kushusha kisukari hata baada ya kufuata masharti?

Ilinichukua zaidi ya miezi 6 kuweza kushusha sukari ya mtu wangu wa karibu sana, hasa baada ya kuelewa nini kinatokea. Hapo ndiyo ushangae kama mimi ni daktari ilinichukua muda huu…

Ingawa yeye alisema anafuata masharti kama wagonjwa wengi, kiuhalisia yeye na wengine huwa hawayafuati. Nitafafanua 

Nitatoa mfano, mtu anaamua kuacha wali na chips lakini anakula muhogo. 

Kuna mambo manne (4) makubwa yanayokwamisha watu kuweza kudhibiti kisukari. (1) kutokuwa na elimu mahususi; (2) kutokufanya wanachokijua; na (3) kuruhusu kila mtu awe daktari wake; (4) kutokufahamu ufanisi wa kila hatua wanayopiga katika matibabu. Nitafafanua.

Wote tunakubaliana kwamba sukari hutoka kwenye chakula. Hivyo naomba nami nianze kufafanua nini hukwamisha wagonjwa kushusha sukari kwa kuanganiza chakula mwanzo.

Hatua Madhubuti za Kufuata Ikiwa Una Kisukari

Kisukari kisichodhibitiwa huathiri sana afya yako. Iwapo unakabiliwa na hali hii, hapa kuna hatua madhubuti za kuchukua kudhibiti kisukari:

1. Fahamu kiwango chako cha kawaida cha sukari

  Jua ‘baseline’ ya vipimo vyako muhimu. Kwa mfano, unapaswa kujua kiwango chako cha kawaida cha sukari kwenye damu.

Watu makini hujua vipimo vyao vya kawaida; kama vile mimi, ambaye sukari yangu ya kawaida huwa kati ya 70-130 mg/dL kabla ya kula na chini ya 180 mg/dL baada ya kula. Kufahamu hili kunakusaidia kutambua mabadiliko yoyote yanayotokea.

2. Fahamu Chanzo cha Kisukari

Ni muhimu kufahamu ikiwa kisukari chako ni cha aina ya 1, 2, au kisukari cha ujauzito, kwani kila aina ina njia yake ya usimamizi. Hii inaweza kujumuisha vipimo vya damu na ushauri wa kitaalamu.

3. Fahamu Vyakula Vyako

Uchaguzi wa vyakula una athari kubwa kwenye usimamizi wa kisukari. Jifunze kuhusu vyakula vyenye sukari nyingi na ya chini na jinsi ya kuchanganya vyakula katika mlo wako kwa uwiano.

4. Dumisha Ufuatiliaji wa Kiwango cha Sukari kwenye Damu

 Ni muhimu kuendelea kufuatilia kiwango chako cha sukari kwenye damu. Hii inakusaidia kujua kama matibabu unayoyazingatia yanafanya kazi na pia kugundua mapema iwapo kuna mabadiliko yoyote yanayoweza kuashiria matatizo mengine ya kiafya.

Kumbuka, kisukari ni hali inayoweza kudhibitiwa vizuri kwa ushirikiano wa karibu na timu yako ya afya, kufuata mpango sahihi wa lishe, na kudumisha mfumo wa maisha wenye afya.

Usisite kutafuta ushauri wa kitaalamu na kushiriki katika programu za AFYATech kielimu kuhusu kisukari ili kudumisha afya bora.

Ukiwa Tayari! Namna 3 tunasaidia kuboresha afya yako

  1. AFYAPlans inakuwezesha Kudhibiti na kuepuka madhara kisukari: Ungana na Daktari wako kwa msaada na mwongozo binafsi Kuhusu dawa, VIPIMO, maarifa na ujuzi. Bonyeza HAPA kujiunga grupu letu. 

  2. Vitabu vya Elimu vinavyokuwezesha kufanya Maamuzi sahihi kuboresha afya yako. Mfano kudhibiti kisukari huku ukila Vyakula unavyovipenda. Bonyeza HAPA kufahamu zaidi

  3. Vifaa vya Matibabu ya Nyumbani vinavyokupa amani na uhakika wa afya yako muda wote. Bonyeza HAPA kuvifahamu.

Uko tayari kuboresha AFYA Yako? Tuwasiliane

Leave a Replay

Zilizosomwa zaidi

Follow Us on Facebook

Follow Us on Twitter

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Kwanini unashindwa kushusha kisukari licha ya kufuata masharti?
Mimi ni Dr. Adinan