Lishe ya mtoto - Dondoo Muhimu
- MUAC ni kipimo cha kutathmini hali ya lishe. Inapimwa kwa mkono wa kushoto moja kwa moja, katikati katikati ya ncha ya bega na ncha ya kiwiko.
- Inabainisha utapiamlo mbaya na hutumika sana kwa watoto wenye umri wa miezi 6-59 (Miezi 6 mpaka miaka miaka 5 kasoro) na vile vile wanawake wajawazito.
MUAC ni Nini, na Kwanini ni Muhimu Kuwa nayo?
Lishe ya mtoto ni kipaumbele kwa kila mama. Unamjali mwanao. Umembeba miezi tisa. Usimuache apate shida za kiafya kwa kuwa na lishe duni. Fahamu hali ya lishe ya mwano leo kwa kutumia MUAC tape.
MUAC ni nini? MUAC ni kipimo cha kutathmini hali ya lishe. MUAC, (Mid Upper Arm Circumfrance) Inapimwa kwa mkono wa kushoto, katikati ya ncha ya bega na ncha ya kiwiko.
MUAC Inabainisha utapiamlo mbaya na hutumika kwa watoto wenye umri wa miezi 6-59 (Miezi 6 mpaka miaka miaka 5 kasoro) na vile vile wanawake wajawazito.
Tunatumia MUAC tape kupima MUAC.
Kipimo cha MUAC kinatabiri vizuri hali afya (nzuri au mbaya na hata kifo). Katika kipindi kifupi cha utafiti, MUAC iliweza kutabiri hali ya afya ya mtoto vizuri kuliko vipimo vingine kama uzito na urefu.
Nawezaje Kutumia MUAC Kufahamu Hali ya Lishe ya Mtoto Wangu?
Upimaji wa MUAC unahitaji vifaa vichache na ni rahisi kufanya hata kwa watu ambao hawajapata mafunzo ya Afya.
Ingawa ni muhimu kupata mafunzo ya jinsi ya kuchukua kipimo, mbinu sahihi inaweza kufundishwa kwa urahisi kabisa. Hivyo unaweza kufanya kipimo hichi mwenyewe nyumbani.
Kwa nini ni mkono ndo unapimwa, si sehemu ingine?: Misuli ya mkono na mafuta chini ya ngozi, haiathiriwi zaidi na mkusanyiko wa majimaji katiaka mwili (kuvimba) inayotokea kwa mtoto mwenye utapiamlo.
Namna ya kutafsiri MUAC Kufahamu Hali ya Lishe ya Mtoto Wangu?
Kipimo hichi huwa na alama tatu: Nyekundu, Njano na Kijani.
- MUAC chini ya 115 mm (Rangi nyekundu) inaonyesha utapiamlo mkali au utapiamlo mbaya wa papo hapo (SAM).
- MUAC kubwa kuliko au sawa na 115 mm na chini ya 125 mm (Rangi ya njano) inaonyesha utapiamlo wastani au utapiamlo mbaya wa lishe (MAM).
- Ikiwa umepata kipimo kikubwa zaidi ya 125 mm (Rangi ya Kijani) maana yake mtoto wako yuko vizuri.
Je, Naweza Kutumia MUAC Nyumbani na Wapi Nitaipata?
MUAC Tape zinapatikana wapi?: Kwa kukujali, AFYATech, inakupatia MUAC Tape kwa bei ya shilingi 10,000/=. Ila kwasasa tunapunguzo, UTAIPAT kwa Shs. 7,000 TU. Bonyeza HAPA kuiona na kutoa oda.
SAIDIA WENGINE
Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu. Nitafurahi ukitoa maoni yako kuhusu maboresho hapa chini