1.Kipima joto 𝐭𝐡𝐞𝐫𝐦𝐨𝐦𝐞𝐭𝐞𝐫 ni kifaa cha kawaida lakini muhimu cha matibabu kwa matumizi ya nyumbani. Inakuwezesha kufuatilia joto la mwili wako. Joto linaweza kuwa kiashiria cha mapema cha ugonjwa.
2. Kifaa cha pili ambacho ni -Muhimu sana kukaribia- LAZIMA kuwa nacho nyumbani ni kipimo cha 𝐬𝐡𝐢𝐧𝐢𝐤𝐢𝐳𝐨 𝐥𝐚 𝐝𝐚𝐦𝐮, . Shinikizo la damu linaweza kuwa muuaji wa kimyakimya, na ufuatiliaji wa mara kwa mara unaweza kusaidia kuzuia matatizo kama vile mashambulizi ya moyo na kiharusi.
3. Kifaa cha tatu kwa UMUHIMU ni kipimo cha kiwango cha sukari kwenye damu – 𝐠𝐥𝐮𝐜𝐨𝐦𝐞𝐭𝐞𝐫. Umuhimu wa kifaa hichi unaonekana pale mtu anapopoteza nguvu ghafla, kizunguzungu au kupoteza fahamu. Kitu cha kwanza kufikiri ni kwamba mtu huyo kapungukiwa sukari. Kumbuka mtu hupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu sukari ikiwa chini ndani ya muda mfupi. Hivyo unaweza kuokoa maisha kwa kuwa na kipimo cha kisukari.
Ikiwa una kisukari, glucometer ni kipimo cha lazima kuwa nacho. Kufuatilia viwango vya sukari yako ya damu mara kwa mara kunaweza kusaidia kuzuia madhara kama vile uharibifu wa mishipa ya fahamu, ugonjwa wa figo, na upofu. Ukiwa na glukometa, unaweza kuangalia viwango vya sukari ya damu kwa urahisi na haraka nyumbani na kufanya marekebisho kwenye lishe yako na dawa inapohitajika.
4. Kifaa cha nne kinasaidia sana wagonjwa wa kisukari kuepuka ulemavu. Wagonjwa wa kisukari husababishiwa ulemavu na vidonda sugu. Ni muhimu kufahamu kama uko kwenye hatari ili kuchukua hatua stahiki kuepuka vidionda. Monofilament inasaidia maelfu ya wagonjwa wa kisukari kuepuka vidonda miguuni.
5&6. Kipimo cha uzito, 𝐦𝐢𝐳𝐚𝐧𝐢 na kikotoo cha BMI inakuwezesha kufuatilia uzito wako mara kwa mara na kukusaidia kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kufuatilia maendeleo yako ikiwa unajaribu kupunguza uzito.
7. Kifaa kinachokupa nafuu haraka ya ugonjwa wa kupumua kama pumua– Nebulizer. Nebulizer inakusaidia kupata nafuu ya haraka na kuepuka madhara ya kupungukiwa na hewa safi ya oxygen. Kinafanya kazi kwa kupeleka dawa moja kwa moja kwenye mapafu.
8. Hatimaye, ni kifaa ambacho hupima kiwango cha hewa safi kwenye damu – oksijeni. , 𝐩𝐮𝐥𝐬𝐞 𝐨𝐱𝐢𝐦𝐞𝐭𝐞𝐫 ni kifaa muhimu kwa wale walio na ugonjwa katika mfumo wakupumua, pamoja na wengine ambao wanataka kufuatilia viwango vyao vya oksijeni wakati wa mazoezi.
Reviews
There are no reviews yet.