1. Kifaatiba cha kwanza ambacho ni -Muhimu sana kukaribia- LAZIMA kuwa nacho nyumbani ni 𝐦𝐚𝐬𝐡𝐢𝐧𝐞 𝐲𝐚 𝐬𝐡𝐢𝐧𝐢𝐤𝐢𝐳𝐨 𝐥𝐚 𝐝𝐚𝐦𝐮, . Shinikizo la damu linaweza kuwa muuaji wa kimyakimya, na ufuatiliaji wa mara kwa mara unaweza kusaidia kuzuia matatizo kama vile mashambulizi ya moyo na kiharusi.
2. Kifaa cha pili kwa UMUHIMU ni kipimo cha kiwango cha sukari kwenye damu – 𝐠𝐥𝐮𝐜𝐨𝐦𝐞𝐭𝐞𝐫. Umuhimu wa kifaa hichi unaonekana pale mtu anapopoteza nguvu ghafla, kizunguzungu au kupoteza fahamu. Kitu cha kwanza kufikiri ni kwamba mtu huyo kapungukiwa sukari. Kumbuka mtu hupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu sukari ikiwa chini ndani ya muda mfupi. Hivyo unaweza kuokoa maisha kwa kuwa na kipimo cha kisukari.
Ikiwa una kisukari, glucometer ni kipimo cha lazima kuwa nacho. Kufuatilia viwango vya sukari yako ya damu mara kwa mara kunaweza kusaidia kuzuia madhara kama vile uharibifu wa mishipa ya fahamu, ugonjwa wa figo, na upofu. Ukiwa na glukometa, unaweza kuangalia viwango vya sukari ya damu kwa urahisi na haraka nyumbani na kufanya marekebisho kwenye lishe yako na dawa inapohitajika.
3. Kipima joto 𝐭𝐡𝐞𝐫𝐦𝐨𝐦𝐞𝐭𝐞𝐫 ni kifaa cha kawaida lakini muhimu cha matibabu kwa matumizi ya nyumbani. Inakuwezesha kufuatilia joto la mwili wako. Joto linaweza kuwa kiashiria cha mapema cha ugonjwa.
4&5. Kipimo cha uzito, 𝐦𝐢𝐳𝐚𝐧𝐢 na kikotoo cha BMI inakuwezesha kufuatilia uzito wako mara kwa mara na kukusaidia kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kufuatilia maendeleo yako ikiwa unajaribu kupunguza uzito.
6. Hatimaye, ni kifaa ambacho hupima kiwango cha hewa safi kwenye damu – oksijeni. , 𝐩𝐮𝐥𝐬𝐞 𝐨𝐱𝐢𝐦𝐞𝐭𝐞𝐫 ni kifaa muhimu kwa wale walio na ugonjwa katika mfumo wakupumua, pamoja na wengine ambao wanataka kufuatilia viwango vyao vya oksijeni wakati wa mazoezi.
aa –
Excellent set
Hamidu Lema –
Big up Afya tech
This is a very good approach to reach the globe and the community at Large.
My order. Oxygen pulse (Oxymetre)
Fenick Range –
Good service