𝐔𝐥𝐭𝐫𝐚𝐬𝐨𝐮𝐧𝐝 Inafanyaje kazi?
USS-Ultrasound ni teknolojia ya upigaji picha ya kimatibabu inayotumia mawimbi ya sauti ya masafa ya juu kuunda picha za miundo ndani ya mwili.
USS haitumii mionzi, na kuifanya kuwa njia salama na yenye ufanisi ya kutambua hali mbalimbali za matibabu.
Kanuni ya msingi ya kazi ya ultrasound inahusisha matumizi ya transducer, kifaa cha mkono ambacho hutuma na kupokea mawimbi ya sauti ya juu-frequency. Transducer huwekwa kwenye ngozi juu ya eneo la mwili linalopimwa. Mpimaji hutumia kimiminika (gel) ambayo husaidia mawimbi ya sauti kusafiri kupitia ngozi.
Transducer inapotoa mawimbi ya sauti, hupenya ndani ya mwili na kuvuka tabaka tofauti za mwili, kama vile viungo, tishu, na mifupa.
Mawinmbi ya sauti inapogonga sehemu hizi za mwili huakisiwa, hurudi nyuma na hupokelewa na ransducer.
Mawimbi haya hubadilishwa kuwa mawimbi ya umeme, ambayo hutumwa kwa kompyuta ili kutengeneza picha.
Picha zilizoundwa na ultrasound zinaweza kuonyesha ukubwa, sura, na uthabiti wa viungo vya ndani na tishu, pamoja na mtiririko wa damu kupitia mishipa ya damu.
Kipimo cha ultrasound hutumika kuchunguza nini?
Ultrasound inaweza kutumika kutambua hali mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ujauzito, ugonjwa wa moyo, maumivu ya tumbo au viungo vingine vilivyomo katika mfupa wa kiuno kama vile kibofu cha mkojo.
Ni muhimu kutambua kwamba kipimo cha ultrasound kina changamoto zake- kutokuweza kupiga picha nzuri katika kila sehemu ya mwili. Hivyo, njia zingine za kupiga picha kama vile CT au MRI zinaweza kuhitajika pale ambapo kipimo cha ultrasound kitashindwa.
Mtoa huduma ya afya anafahamu kipimo bora kwa tatizo ulilonalo.
Je, kuna matumizi mengine ya kipimo cha Ultrasound?
Mbali na uchunguzi wa kimatibabu, ultrasound inaweza pia kutumika kwa madhumuni ya matibabu, kama vile kuvunja mawe kwenye figo.
Kwanini mtu haambiwa anywe maji kabla ya kipimo cha Ultrasound?
Unaweza kujaribu kujibu swali hili kwenye sehemu ya comments hapo chini.
Picha: Science ABC