Kisukari ni ugonjwa unaoweza kuathiri afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake. Katika makala hii, nitakueleza athari za kisukari kwenye afya ya uzazi na jinsi unavyoweza kudhibiti ili kuepuka madhara hayo.
Tukusaidie kuwa na uzazi salama?
Uliza maswali yako wakati wowote na upate majibu kutoka kwa wataalamu wa afya. Utalipia TSh. 4,900/=
Athari za Kisukari kwa Afya ya Uzazi kwa Wanawake
- Ugumba
- Wanawake wenye kisukari wako kwenye hatari kubwa ya ugumba au kushindwa kubeba mimba. Udhibiti duni wa sukari ya damu na mabadiliko katika mfumo wa homoni ni baadhi ya sababu zinazochangia.

- Matatizo wakati wa Ujauzito
- Kisukari cha ujauzito (gestational diabetes) kinaweza kusababisha matatizo kwa mama na mtoto, pamoja na uzito mkubwa wa mtoto na kujifungua mtoto njiti.

- Matatizo ya Mayai
- Wanawake wenye kisukari wanaweza kuwa na matatizo ya ovari, ikiwemo kuongezeka kwa uzalishaji wa homoni za kiume (androgens), hali inayosababisha shida za uzazi.

- Mimba kutoka
- Kisukari cha ujauzito kinaweza kusababisha mimba kutoka kutokana na uzito mkubwa wa mtoto.

- Kujifungua Kabla ya Wakati
- Wanawake wenye kisukari wako kwenye hatari kubwa ya kujifungua kabla ya wakati au watoto wenye uzito wa chini.

- Maambukizi ya Fungasi ya Ukeni
- Viwango vya juu vya sukari ya damu vinaweza kusababisha maambukizi ya fangasi ukeni (candida).
Kula bila hofu. Furahia
Fahamu aina, kiasi na namna ya kuchanganya vyakula kudhibiti kisukari
Athari za Kisukari kwa Afya ya Uzazi kwa Wanaume
- Kupungua kwa Uzalishaji wa Manii
- Kisukari kinaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa manii na mbegu za kiume, hivyo kuathiri uzazi.

- Kupungua kwa Nguvu za Kiume
- Kisukari kinaweza kusababisha matatizo ya nguvu za kiume, na kuathiri uwezo wa kufanya mapenzi na kushikisha mimba.

- Kupungua kwa Homoni za Kiume (Testosterone)
- Kisukari kinaweza kusababisha kupungua kwa viwango vya testosterone kwa wanaume, hivyo kuathiri uzazi wao.
- Kiwango cha kutopata watoto kwa wanaume wenye kisukari, kilichotathminiwa katika tafiti chache, kinatofautiana kati ya 35% hadi 51%.
- Maambukizi ya Fungasi
- Viwango vya juu vya sukari ya damu vinaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya fangasi kwenye eneo la uume.

- Hatari ya Ugonjwa wa Prostate
- Kuna uhusiano kati ya kisukari na hatari ya kuendelea kwa ugonjwa wa tezi dume. Wanaume wenye kisukari wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kuwa na ugonjwa wa tezi dume.
Namna ya Kudhibiti na Kuepuka Athari za Kisukari
Kudhibiti kisukari na kuepuka athari zake ni jambo muhimu kwa afya yako ya uzazi. Hapa kuna mambo matatu muhimu yatakayokusaidia:
- Kuwa na Elimu Sahihi
- Hakikisha unapata elimu sahihi kuhusu kisukari. Usiwe kama uwanja wa majaribio. Pata elimu kupitia kitabu chetu cha “Dhibiti Kisukari kwa Vyakula” ambacho kinaendelea kuwasaidia wengi kudhibiti kisukari kwa njia ya chakula.

- Kufuatilia Afya Yako
- Fahamu viwango vya sukari yako kila wakati na fanya vipimo vingine muhimu kwa afya yako. Jisajili kwenye AFYAPlan ili kupata vifaa na elimu ya kufuatilia afya yako kwa ukaribu.

- Kuchukua Hatua Stahiki Mapema
- Ukigundua sukari yako iko juu, boresha matibabu. Kama sukari inashuka vizuri, endelea na tiba bila kuacha. Tumia vifaa vyetu ufuatilie kiwango cha sukari kwenye damu leo.