Pulse Oximeter (PO2) : Kipimo cha hewa ya Oxygen kwenye damu

Bila shaka unafahamu kwamba viumbe hai, ikiwemo binaadamu, huitaji hewa ya Oxygen (O2) ili kuishi. Na pia hutoa hewa Carbon Dioxide (CO2) kama uchafu. Hewa hizi hubebwa katika damu. Binadamu huvuta hewa ya O2 kwa kutumia pua. Hewa hii huingia katika mapafu.

O2 hutoka kwenye mapafu na huingia katika damu na kupelekwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwamo ubongo. Katika damu, Oxygen na CO2 hubebwa na hemoglobini. Unaweza fikiria kwamba O2/CO2 ni abiria,  hemoglobini ni gari na mishipa ya damu ni barabara. CO2 hutoka katika damu na kuingia kwenye mapafu na kupumuliwa nje ya mwili.

Ugonjwa wowote unaoathiri mfumo wa upumuaji hupunguza kiwango cha O2 na hivyo kuhatarisha uhai wa mtu. Magonjwa kama pumu, moyo, vichomi (pneumonia), TB na hivi sasa Corona, kwa uchache huathiri mfumo wa upumuaji.

 

Namna ya kujipima Oxygen

Pulse Oximeter Inavyofanya kazi

Kipimo cha Oxygen kwenye damu - pulse oximeter
red_intro
red_finger_intro

Kifaa hiki huvaliwa kidoleni. Baada ya kukiweka vizuri, utakiwasha na kusubiri kipime kwa muda wa sekunde ~20.

Kifaa hichi hutumia miangaza kupima kiwango cha oxygen kilichobebwa na hemoglobin. Mianga iko ya aina mbili, ile ya kupima kiwango cha oxygen kwenye hemoglobin na mingine hupima kiwango cha CO2 kwenye hemoglobini. 

Mwisho, kifaa kitatoa taarifa ya kiwango cha oxygen kwenye damu kwa mfumo wa asilimia (%). Kawaida, mwanadamu anatakiwa awe na kiwango cha oxygen kati ya 95% hadi 100%

OFFER! PATA Pulse Oximeter – Kipimo cha Oxygen kwenye damu kwa Bei ya Offer 53,900 BADALA ya 75,000/= 

Je, ninahitaji Pulse Oximeter?

Kama tulivyoona, pulse oximeter hutumika kufahamu kiwango cha oxygen kwenye mwili kwa mtu mwenye magonjwa yanayoathiri mapafu.

Pulse oximeter ni kipimo ambacho ni rahisi kutumia na haraka kukufahamisha kiwango cha oxygen mwilini.

Kwa kipindi hichi ambacho covid-19 imeshamiri ni muhimu kuwa nacho angalau kimoja kwenye nyumba.

Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Pulse Oximeter: Kipimo cha Oxygen kwenye damu.?
Mimi ni Dr. Adinan