Hypertension / Shinikizo la Juu La Damu

Je, Shinikizo la Damu ni Ugonjwa?

Shinikizo la damu husaidia damu kufika sehemu muhimu za mwili wetu. Hivyo, shinikizo la damu lenyewe si ugonjwa. Hata hivyo, shinikizo la damu la juu au shinikizo la damu la chini ni magonjwa hatari.

Shinikizo la juu la damu, au presha, ni ugonjwa unaosababisha madhara makubwa kiafya na ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo nchini Tanzania.

Inakadiriwa kuwa kati ya watu 10, watu 4 wana shinikizo la juu la damu. Hata hivyo, presha haina dalili za wazi, na hivyo kufanya kuchelewa kugundulika.

Ili kudhibiti shinikizo la juu la damu, ni muhimu kugundua mapema na kuanza matibabu. Hivyo, ni vyema kupima shinikizo la damu mara kwa mara, hasa ikiwa una sababu hatarishi za kupata presha. Moja ya sababu za presha ni umri kuongezeka.

Ikiwa una umri wa miaka 30 au zaidi, uko katika hatari, na hivyo unapaswa kupima shinikizo la damu mara kwa mara. Kwa kuanza, unaweza kupima angalau mara moja kwa mwezi.

Ni muhimu kusoma makala mbalimbali ili kujifunza zaidi kuhusu ugonjwa wa presha. Kupitia makala hizi, utapata ufahamu wa kina kuhusu ugonjwa huu na kwa nini wakati wengine wanahangaika kushusha presha zao, wengine wanafurahia maisha licha ya kuwa na shinikizo la juu la damu au presha.

Tunakualika kusoma makala zote zinazohusiana na shinikizo la  damu ili kuongeza ufahamu wako na kuchukua hatua sahihi kwa afya yako.

Kwa kufanya hivyo, utaweza kufahamu tiba ya shinikizo la juu la damu kudhibiti shinikizo la juu la damu na kuishi maisha yenye afya na furaha.

mwanaume anapima kama ana shinikizo la damu la juu

Presha: Kwanini Ikaitwa Muuaji wa Kimya Kimya!

Wengi wanafariki na kupata ulemavu duniani kila siku kwa sababu ya shinikizo la damu la juu. Shinikizo la damu linasababisha kiharusi, magonjwa ya moyo na figo kwa uchache. Ukisoma makala hii utafahamu kuhusu ugonjwa huu, tiba na namna ya kujikinga na madhara. Soma zaidi

Soma zaidi »

Leave a Reply

Specify Facebook App ID and Secret in the Super Socializer > Social Login section in the admin panel for Facebook Login to work

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top