fbpx

Hypertension / Shinikizo la Juu La Damu

Je, Shinikizo la Damu ni Ugonjwa?

Shinikizo la damu husaidia damu kufika sehemu muhimu za mwili wetu. Hivyo, shinikizo la damu lenyewe si ugonjwa. Hata hivyo, shinikizo la damu la juu au shinikizo la damu la chini ni magonjwa hatari.

Shinikizo la juu la damu, au presha, ni ugonjwa unaosababisha madhara makubwa kiafya na ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo nchini Tanzania.

Inakadiriwa kuwa kati ya watu 10, watu 4 wana shinikizo la juu la damu. Hata hivyo, presha haina dalili za wazi, na hivyo kufanya kuchelewa kugundulika.

Ili kudhibiti shinikizo la juu la damu, ni muhimu kugundua mapema na kuanza matibabu. Hivyo, ni vyema kupima shinikizo la damu mara kwa mara, hasa ikiwa una sababu hatarishi za kupata presha. Moja ya sababu za presha ni umri kuongezeka.

Ikiwa una umri wa miaka 30 au zaidi, uko katika hatari, na hivyo unapaswa kupima shinikizo la damu mara kwa mara. Kwa kuanza, unaweza kupima angalau mara moja kwa mwezi.

Ni muhimu kusoma makala mbalimbali ili kujifunza zaidi kuhusu ugonjwa wa presha. Kupitia makala hizi, utapata ufahamu wa kina kuhusu ugonjwa huu na kwa nini wakati wengine wanahangaika kushusha presha zao, wengine wanafurahia maisha licha ya kuwa na shinikizo la juu la damu au presha.

Tunakualika kusoma makala zote zinazohusiana na shinikizo la  damu ili kuongeza ufahamu wako na kuchukua hatua sahihi kwa afya yako.

Kwa kufanya hivyo, utaweza kufahamu tiba ya shinikizo la juu la damu kudhibiti shinikizo la juu la damu na kuishi maisha yenye afya na furaha.

Huduma ya Kwanza ya Presha ya Kupanda

Utangulizi Presha ya kupanda, au shinikizo la juu la damu, ni hali ambapo nguvu ya damu inayosukuma dhidi ya kuta za mishipa ya damu inapanda na kuwa juu zaidi ya kiwango cha kawaida. Hali hii inaweza kuwa hatari sana, kwani inaweza kusababisha matatizo kama vile kiharusi, mshtuko wa moyo, na matatizo mengine ya kiafya. Ni

Soma zaidi »
human heart scale model

Athari ya Hasira kwenye Kisukari na Presha: Namna ya Kuepuka

Je, unajua kwamba hasira inaweza kuwa na athari kubwa kwenye afya yako, hasa kwa wale wenye kisukari na presha? Soma zaidi ili kujifunza jinsi ya kudhibiti hasira na kuboresha afya yako kwa ujumla. Athari za Hasira kwenye Kisukari Hasira ni hisia ya kawaida inayoweza kutokea kwa kila mtu. Kujua jinsi ya kudhibiti hasira ni muhimu

Soma zaidi »
mwanaume anapima kama ana shinikizo la damu la juu

Presha: Kwanini Ikaitwa Muuaji wa Kimya Kimya!

Wengi wanafariki na kupata ulemavu duniani kila siku kwa sababu ya shinikizo la damu la juu. Shinikizo la damu linasababisha kiharusi, magonjwa ya moyo na figo kwa uchache. Ukisoma makala hii utafahamu kuhusu ugonjwa huu, tiba na namna ya kujikinga na madhara. Soma zaidi

Soma zaidi »
Shopping Cart
Muulize Dr. Adinan
1
Muulize Dr. Adinan
Chat na Dr. Adinan
Hello 👋.
Ungependa kuuliza nini kuhusu Shinikizo la damu?
Mimi ni Dr. Adinan