Sigara ni moja ya sababu zinazochangia kuongezeka kwa shinikizo la damu (presha). Matumizi ya sigara yanaweza kuathiri mzunguko wa damu na kusababisha athari mbaya kwenye mfumo wa moyo na mishipa ya damu.
Fahamu namna 4 sigara huathiri presha na afya ya moyo na mishipa ya damu kwa ujumla:
1. Sigara inavyoongeza Shinikizo la Moyo:
Mara tu mtu anapovuta sigara, kemikali zinazoathiri mfumo wa moyo na mishipa ya damu huingia mwilini. Nikotini, kemikali inayopatikana katika sigara, husababisha kuongezeka kwa moyo kwa kasi na kuongeza nguvu ya kupiga moyo. Hii inasababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu [1]. Nikotini huathiri mfumo wa mishipa ya fahamu na kusababisha kutolewa kwa homoni na kemikali zinazosababisha mishipa ya damu kusinyaa. Kusinyaa huku kunasababisha upinzani mkubwa wa damu na kuongeza shinikizo la damu.
2. Kuharibu Uwezo wa Kutanuka kwa Mishipa ya Damu
Kuvuta sigara husababisha kuharibika kwa utando wa ndani wa mishipa ya damu, na kuifanya kuwa migumu na kusababisha kuziba kwa mishipa midogo ya damu [2]. Hii inaweza kuathiri mzunguko wa damu na kusababisha shinikizo la damu kuongezeka.
3. Sigara Huongeza Lehemu Mbaya
Matumizi ya sigara huongeza viwango vya lehemu mbaya (LDL cholesterol) na kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa mishipa ya damu kukakamaa (atherosclerosis), kwa kuongeza utando ndani ya mishipa ya damu. Hii inaweza kusababisha kuziba kwa mishipa ya damu na kupunguza mzunguko wa damu, na hivyo kuongeza presha ya damu [3] na kusababisha madhara mengine kama kiharusi.
4. Sigara Huathiri Usawa wa Kemikali katika Mfumo wa Mishipa ya Fahamu
Kuvuta sigara kunaweza kuathiri kemikali katika mfumo wa mishipa ya fahamu ambao unadhibiti shinikizo la damu, kama vile dopamine na serotonini.
Mabadiliko katika kemikali za mfumo wa mishipa ya fahamu yanaweza kusababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu [4].
Inafaa kuzingatia kuwa kuacha kuvuta sigara ni hatua muhimu katika kudhibiti na kupunguza shinikizo la damu. Kupunguza matumizi ya sigara au kuacha kabisa kunaweza kusaidia kuboresha afya ya moyo na kudhibiti shinikizo la damu.
Rejea
[1] How does smoking affect the heart and blood vessels? https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5516049/
[2] Effects of Cigarette Smoking on Cardiovascular Function, https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2092364/
[3] Smoking and hypertension: independent effects on blood viscosity and cardiovascular function, https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/2066743/
[4] Central and peripheral effects of chronic cigarette smoking on blood pressure regulation, https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/10430799/

Maji ya Chupa Yana Maelfu ya Vipande Vidogo vya Plastiki
Lengo la Utafiti Utafiti ulilenga kuchunguza uwepo na athari za nanoplastiki katika maji ya chupa. Nanoplastiki ni vipande vidogo vya

Kama Una Magonjwa Haya, Uko Hatarini Kupata Kisukari
Kisukari kinaweza kuwepo bila kuonesha dalili. Lakini watafiti wamekuja na list ya magonjwa ambayo huashiria kuwa na kisukari siku za usoni. Fahamu zaidi
𝗜𝗻𝘀𝘂𝗹𝗶𝗻 𝗺𝗮𝗿𝗮 𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗶𝗸𝗶 𝗱𝗵𝗶𝗱𝗶 𝘆𝗮 𝘀𝗶𝗻𝗱𝗮𝗻𝗼 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝘀𝗶𝗸𝘂: 𝗨𝘁𝗮𝗳𝗶𝘁𝗶 U𝗺𝗲𝗼𝗻𝗲𝘀𝗵𝗮 M𝗼𝗷𝗮 𝗻𝗶 B𝗼𝗿𝗮 K𝘂𝗹𝗶𝗸𝗼 N𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲
Katika utafiti huu uliokuwa na watu 588 wenye ugonjwa wa kisukari aina ya 2 ambao hawakuwahi kutumia insulin, Matokeo ya

Kulala kwa Muda Mfupi Mchana Kunaweza Kulinda Afya ya Ubongo Wako – Utafiti
Kulala kwa muda mfupi wakati wa mchana kunaweza kusaidia kulinda afya ya ubongo wakati unapozeeka, wanasayansi wamependekeza baada ya kugundua kwamba mazoea haya yanahusishwa na ukubwa wa ubongo.
Msongo Wa Mawazo: Namna Ya Kuudhibiti Kuboresha Afya Yako
Je, umewahi kuhisi kuwa namsongo wa mawazo? Hakuna shaka kuwa stress inaweza kuathiri afya yetu ya akili na mwili. Njia
Kiwango cha Pombe Salama kwa Binadamu: Athari, na Magonjwa Yasiyoyakuambukiza
Pombe ni nini? Pombe ni kilevi kinachotokana na usindikaji wa sukari iliyopo kwenye aina tofauti ya vyakula. Pombe huwa katika


